Je, uliwahi kusingiziwa jambo gani la aibu ugenini?!

Restless Hustler

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2017
Posts
5,150
Reaction score
20,025
Habari za muda huu Wana Jf!

Dunia hii imejawa na changamoto mbalimbali lakini leo tuongee kuhusu kusingiziwa Mambo ya aibu. Karibu tushee uzoefu huo na jinsi gani uli-recover.

Binafsi mwaka flani Nilienda kwa watu wakanisingizia nimejamba tena mbele ya mabinti wakubwa tu[emoji28]. Sasa uswahilini hawana maneno ya ustaarabu Wala kupunguza makali ya maneno. Kuna kawimbo kao wanaimba huku wanazungusha kidole.

Wanaamini wimbo utakapoishia na aliyepointiwa na kidole ndo huyo kajamba. Ebwana ee wimbo uliishia kwangu nikiwa nimenyooshewa kidole. Watu wote wakashika pua zao wakaniambie niende nje nikapulizwe na upepo kidogo[emoji28] huu Ni Mwaka wa 6 sijawatembelea hao waswahili. Pia nimekoma matembezi yasiyo na manufaa.
 
Ni kakifala kale kwasababu sometime mjambaji ndiye anakaanzisha utasikia

Ana
Ana
Anado

Kajambila pasto

Kajamba

Ushuzi unanuka

Tena sana

Sana kabisa
[emoji23][emoji1787][emoji28][emoji1787][emoji23]
 
Dada yangu anabiashara yake Kariakoo. Mambo yalipokua mazuri akaamua kufuata mwenyewe mzigo Dubai

Bahati nzuri kuna dada yetu binamu anamakazi yake huko kwa hiyo wakakubaliana atafikia kwake

Alipokwenda akakuta kuna wadada wengine wawili Wazanzibari na watoto wao watatu. Hao wadada walikua ni wageni wa mara kwa mara nyumbani kwa huyo dada binamu. Siku ya pili tangia sister afike dada mmoja Mzazibari akalalamika kua haioni pochi yake na ilikua na pesa!

Sister anasema kilikua ni kipindi kigumu sana katika maisha yake maana watu wote walikua wanazungumza kua " hii tabia mbona haikuwepo hapa!!!!?" Hawakua wakimtaja lakini kila mtu aliashiria kua huyu aliyekuja ndio suspect number one!

Baada ya muda wa masaa mawili binti wa huyo mwanamke "aliyeibiwa" alikuja akiwa ametoka matembezini akiwa na pochi ya mama yake!

Sister hakusubiri siku igeuke. The same day akabeba mizigo yake na kwenda hotelini pamoja na jitihada kubwa alizofanya binamu za kumuomba radhi na kumbembeleza abakie hapo nyumbani
 
Hahaha hii huwa inakata stim mbaya. Au unafika ugenini ile umekaa siku ya kwanza ya pili mara kitu kimeharibika mfano TV na vitu vingine vya hivyo halafu wenyeji wanaanza kusema "mbona haijawahi kuharibika" hapo moja kwa moja mgeni unaonekana ndio mtuhumiwa.
 
Back
Top Bottom