Je, uliwahi kuwa maarufu shuleni?

Je, uliwahi kuwa maarufu shuleni?

Nilimpa bangi mwalimu wa biology kilichofuata sijui hata anakumbuka
Lakini hawatanisahau especially headmaster maana kila akiniona anacheka
Hiyo ilikuwa form 2


Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] mimi primary nilikuwa mkali wa English, halafu lilikuwa somo linalowatoa jasho wengi si unajua shule za vijijini, basi nikawa star mpaka shule za jirani wananijua
Safi sanaaa
 
jamaa mjinga kabisa sijui anadhani BBC SWAHILI IMEANZA NA KIKEKE hahaha

Nakumbuka tokea kitambo nilikua msikilizaji mzuri sana wa radio. Ilikua inaanza Channel Afrika, inakuja DW kisha BBS namalizia na Sauti ya Amerika. hapo mchana sipitwi na DW ile saa saba. Sijutii ule muda, ulinifanya nijifunze na kujua mambo mengi sana.
Ukizingatia tumekulia ndani ndani huko hata kuliona gari ni muujiza.
 
Atakuwa ameanza kusikiliza radio za FM zilipokuja, zikawa zinajiunga na matangazo hayo.

Nakumbuka DW kina Umrikheri (spelling sizijui haya) ana sauti yake hatujui ni mwanaume wala mwanamke.

Yule ni mwanamama mwanamke mkuu, sauti yake yenye madoido hauwezi badili stesheni asilani. Kulikua na Ramadhan Ali akitangaza michezo, Wajir Sheikh, Othman Miraji, Shangama kwakweli timu ilikua imekamilika.
 
Primary nilikua napiga namba moja tu from darasa la pili mpk la saba naongoza lakini kwa muda wote huo nilikua sio maarufu sijui nyota yangu nani aliiba darasa la saba ndo kidogo nkawa maarufu baada ya mtihan wa mock...
Olevel..nikakutana na vipanga wenzangu japokuwa kwenye top ten nilikua sitoki hilo likanipa umaarufu kidogo lakini kilichonipa umaarufu zaid ni kipaji changu cha uchekeshaji aisee hii kitu ilinifanya nipendwe sana hasa na mademu..

Advance nilikua smart sana kiuvaaji na comedy ndo ikanifanya niwe maarufu sana kila nikipita watu wananiangalia wengne wanaanza kucheka bila kuwachekesha wakikumbuka maneno yangu ta stand up comedy niliyokuwa nafanya katika talent show za shule..pia hapa nikaanza kujifunza kuishi kigangsta baada ya kukutana na watoto wa chuga wakanifundisha kuvaa macheni mengi shingoni pamoja na kutupia pamba kama za mbele ingawa zilikuwa zinakatazwa shule tulivaa kibishi hivyo nikawa maarufu kwa staili hiyo..
Chuo..kila mtu na mishe zake ila staili yangu ya cheni nyingi na kutupia pamba pamoja na pete kibao vidolen ikazid kunipa umaarufu nikapendwa na mademu kinoma na lifestyle yangu ya kimarekani[emoji39]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shule ya msingi nilikua naongoza, darasa la kwanza hadi la sita ni namba moja tu.
O level, nilikua nasifika kwa ucha Mungu na nidhamu, pia nilikua vizuri sana kwenye Physics.
A' Level kama kawaida Physics hasa mechanics ilikua ndio eneo langu la kujidai.

Huko kote nilikua nachaguliwa kuwa monitor, kiranja au kiongozi.
 
Yule ni mwanamama mwanamke mkuu, sauti yake yenye madoido hauwezi badili stesheni asilani. Kulikua na Ramadhan Ali akitangaza michezo, Wajir Sheikh, Othman Miraji, Shangama kwakweli timu ilikua imekamilika.

Ramadhani Ali akitangaza Bendesligaaa!

Alikuwa na kipindi cha Jumamosi mchana cha Science na Technolojia, wale watu walikuwa ni timu hasa.
 
Nakumbuka tokea kitambo nilikua msikilizaji mzuri sana wa radio. Ilikua inaanza Channel Afrika, inakuja DW kisha BBS namalizia na Sauti ya Amerika. hapo mchana sipitwi na DW ile saa saba. Sijutii ule muda, ulinifanya nijifunze na kujua mambo mengi sana.
Ukizingatia tumekulia ndani ndani huko hata kuliona gari ni muujiza.

Hii ni Sauti ya Amerika ikikutangazia moja kwa moja kutoka Washington DC, mtangazi wako ni Momoyo Hamza.
 
Back
Top Bottom