Raymanu KE
JF-Expert Member
- Jan 20, 2022
- 8,611
- 16,118
Waslaam wakuu,
Kuna hili suala ambalo limenitokea mara kadha naomba kuwashirikisha, sijui huwa linawatokea na nyie ama ni mimi pekee yangu tu. Kuna muda ambao una rafiki yako ama mpenzi wako huwa mnaaminia sana, ila ikatokea siku mkaahidiana mambo fulani ila mmoja wenu haswa rafiki/mpenzi wako akayeyusha dili.
Baada ya hiyo ukakasirika sana ukaamua kufuta na namba yake kwenye simu yako, ukaapa kamwe hutokaa umtafute na wala yeye asikutafute tena. Yaani uhusiano uishi hivyo.
Kwa mfano, kama mpenzi wako alikuahidi kwamba atakutembelea kwenye maskani yako jamaa ukaboycott kila kitu ili umsubiri aje, siku inaisha hajatimba gheto na ukimtafuta kwenye simu hapatikani kabisa. Sasa hasira zinakujaa unaamua kukata mawasiliano naye kwa kufuta namba zake kwenye simu yako.
Sasa baada ya wewe kuifuta namba yake muda mfupi baada unaona anakupigia simu pamoja na kututumia ujumbe eti anataka aje. Jamaa unajikuta umeihifadhi namba yake Ttna kwa tabasamu.😂
Kisa cha pili una mshikaji wako mnaelewana sana, siku moja unamuomba akupige tafu na pesa kiasi fulani, hapa tunafikiria ulishamfanyiaga na pesa ndiyo maana unamuomba. Sasa jamaa anakupigia kalenda kwamba atakutumia kama muamala kwenye simu unasikilizia.
Siku inafika umetegea sana ila jamaa hajiongezi na ukipiga simu hapokei wala kujibu ujumbe. Unaona umepigwa fix. Unakasirika unafuta namba yake kwenye simu yako ukaapa kamwe hutokaa umtafute tena. Baada ya siku moja unaona muamala unaingia kwenye simu yako, tena ni maradufu ya ile pesa uliomuomba. Jamaa unabaki kutabasamu na kuhifadhi namba ya jamaa kwenye simu. 😂
Je, wewe ushawahi kufuta namba ya mtu kwenye simu yako na ukarudi kuihifadhi tena?