Je umeshawahi kukumbana na kadhia hii kutoka kwa watu?

Je umeshawahi kukumbana na kadhia hii kutoka kwa watu?

Marcy

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2013
Posts
2,430
Reaction score
5,910
Ni pale mpo katika kundi kutekeleza kazi fulani Katika lile kundi wapo watakao kaa pembeni kuangalia hawagusi chochote, Wapo watakao papasa tu ili mradi waonekane nao walishiriki kwenye hiyo kazi Na yupo mhanga atakae jitolea kuitekeleza ile kazi kikamilifu.

Endapo kazi itatiki vyema basi sifa hutopewa wewe uliyeshiriki kikamilifu atapewa mtu mwingine tofauti yaani mtu wao wanayemkubali wakati yeye alipapasa tu na wanajifanya kama vile hawaoni mchango wako yaani kama ni asante au asante atapewa huyo waliyempaisha.

Ila kazi ikibuma utasikia fulani huyo ndio kaharibu nashindwa kuelewa hii ina maana.gani ni chuki au ni roho za kwanini?

Je ulipo kumbana na hali hii ulichukua hatua gani kupambana nao ili iaminike wewe ndiye uliye fanya hiyo kazi?
 
Tenda wema nenda zako usingoje shukrani.

Ukifika mahala ukawa unafanya vitu bila kuathiri hisia zako kwa namna jamii itakuchukulia, utakuwa kwenye hali ya kufanya bila kujali watasemaje au watanionaje na pia hutojali hata wasipoona kujitoa kwako. Ndani ya nafsi yako unakuwa na amani na tabasamu jepesii unapoona ulichofanya ni chema na chapendeza machoni pa Muumba.

Si wote wanaweza hii, Linda sana Moyo wako Kuliko vyote Ulindavyo. Maana Ndiko zitokako Chemchem za Uzima.

Bibi Kasinde.
 
"Nice guy" ni mtu mkarimu na mwepesi kuyumbishwa, anakubali kubali kila kitu bila kuwa na msimamo, lengo aonekane mwema au awafurahishe wengine hata kama jambo hilo halifai, mara nyingi hua kinafiki.

"Good guy" ni mtu mwenye maadili mema, hufanya yaliyo sahihi, na anasimamia haki haijalishi mazingira gani, hayumbishwi, hana mda wa kuridhisha wengine ili wamuone bora, hachekei ujinga au yale yanayoenda tofauti na mapendeleo yake, sio kinafiki.

Ukiwa nice guy utatumika vibaya sana na watu, kama ni kazini kila kitu utasikia mpe fulani.

Situation kama hiyo kama siku nyingine, pima kazi gawa kwa idadi, fanya ile nguvu yako tu, kisha tulia muendee kuangaliana.

Don't be Nice, Be good.
 
Ni pale mpo katika kundi kutekeleza kazi fulani Katika lile kundi wapo watakao kaa pembeni kuangalia hawagusi chochote, Wapo watakao papasa tu ili mradi waonekane nao walishiriki kwenye hiyo kazi Na yupo mhanga atakae jitolea kuitekeleza ile kazi kikamilifu.

Endapo kazi itatiki vyema basi sifa hutopewa wewe uliyeshiriki kikamilifu atapewa mtu mwingine tofauti yaani mtu wao wanayemkubali wakati yeye alipapasa tu na wanajifanya kama vile hawaoni mchango wako yaani kama ni asante au asante atapewa huyo waliyempaisha.

Ila kazi ikibuma utasikia fulani huyo ndio kaharibu nashindwa kuelewa hii ina maana.gani ni chuki au ni roho za kwanini?

Je ulipo kumbana na hali hii ulichukua hatua gani kupambana nao ili iaminike wewe ndiye uliye fanya hiyo kazi?
Mkuu, binadam ni kiumbe mtata sana, ukishatimiza majukum yako, endelea na mambo mengine wala usisubiri ahsante wala kusifiwa.
 
Kama kazi haina malipo huwa sioni umuhimu wa mimi kuwa kimbelembele kujituma, kama ina malipo nitachapa kazi malipo tu yanatosha kunifariji.
Na Bado mnalalamika Viongozi wa nchi hii ni wabinafsi na mafisadi?!

Kumbuka, Pilipili haiwezi kuota kwenye mkomamanga.

Mtoa Mada; Just be You, the rest of the World will adjust. Never put out your candle for the fear of outshining a gasoline lamp! Piga kazi wahusika halisi wanaona, trust me.
 
Back
Top Bottom