Je, umeshawahi kusikia kijiji cha Nyeregenge kilichopo Musoma?

Je, umeshawahi kusikia kijiji cha Nyeregenge kilichopo Musoma?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Nyeregenge ni kijiji kinachopatikana Musoma vijijini mkoani Mara.

Kijiji hiki hakina shule, hakikuwa na msikiti wala kanisa, na kimepata kanisa lake la kwanza miaka ya hivi karibuni, 2017 ambapo Wakatoliki wamejenga kanisa.

Kijiji hiki kina watu waliobobea kwenye mila na tamaduni ambapo hadi leo watoto mapacha, albino, walemavu na njiti hutupwa kwenye msitu wa kafara.

Huwezi kuingia Nyeregenge kama umebeba nyama mbichi, una jeraha, wanawake wakiwa kwenye siku zao nao hawawezi kuingia, kwani lazima utakufa.

Mama wenye ujauzito na wenye watoto hawaruhusiwi kuingia ndani ya Nyeregenge.

Hakika Tanzania ni kubwa sana na ina mengi sana hayajaandikwa
 
Huruhusiwi kuingia na WATOTO...kwa hiyo ukiwa na watoto unahama hicho kijiji? na hurudi mpaka wakue !!!

Kama ndivyo kinawezaje kuendelea kuwa na kizazi kipya mpaka sasa?!!!
 
Huruhusiwi kuingia na WATOTO...kwa hiyo ukiwa na watoto unahama hicho kijiji? na hurudi mpaka wakue !!!

Kama ndivyo kinawezaje kuendelea kuwa na kizazi kipya mpaka sasa?!!!
Huko hamna hospitali hivyo huwa wanavuka kwenda Musoma mjini wakitaka kujifungua.

Akitoka kujifungua inabidi akae kwa miezi kadhaa mpaka mtoto akue, vinginevyo ni lazima watoe sadaka ya kuteketeza
 
Back
Top Bottom