MR.NOMA
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 339
- 505
Karibuni wakuu, tushirikishane juu ya jambo lolote la hovyo ,ambalo umewahi kulifanya maishani mwako ,hasa kipindi Cha ujana/ utoto na badae ulijutia. Nianze Mimi,; wakati nipo darasa la 2 nikiwahi kufungulia radio ya mzee , nikaweka Kanda ya lackdube nikasililiza mwanzo mwisho. Lakini bahati mbaya tape ilinasa nikashindwa kuitoa ilibidi niivute nikate na baada ya hapo nilijua viboko vitanihusu mzee akirudi home,nikaamua kwenda kuifukia shambani hiyo kanda yote. Mzee aliporudi alitafta akaikosa.Na alisikitika sana maana alipenda sana kuisikiliza. Huwa najuta , ingekuwa Sasa ningeomba msamaha tu na sio kufanya nilichofanya. Lete stori yako unayojutia , tujifunze