Je, umewahi Kujiuliza nini lengo la mfuko mdogo mbele ya Suruali ya Jeans?

Je, umewahi Kujiuliza nini lengo la mfuko mdogo mbele ya Suruali ya Jeans?

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Je unaujua mfuko mdogo katika suruali yako ya Jeans? Ndiyo, ule ambao umeshonwa juu kidogo ya mfuko mkubwa wa kulia.

Umewahi hata mara moja kusimama na kujitafakari kwa nini huo mfuko mdogo mbele ya suruali yako ya jeans upo hapo ulipo na nini hasa lengo la mfuko huo zaidi ya pengine kudumbukiza sarafu au jojo ambayo unataka kuja kuitafuna baadae au kuwaza kama ni fasheni tu katika nguo?

Kama hujawahi kujiuliza hilo swali na bado hujui chanzo na lengo la mfuko huo mdogo mbele ya suruali yako ya Jeans usijali kwani tovuti hii itakueleza chanzo na lengo la mfuko huo.

Mfuko huu ulikuwa unatekeleza jukumu muhimu sana miaka ya nyuma na ndio sababu kubwa iliyopelekea watengenezaji wa suruali za Jeans kuweka mfuko huo juu kidogo ya mfuko wa mbele wa suruali.

“Ni mfuko maalum wa kuhifadhi saa. Ndiyo, inasemekana miaka ya nyuma ya 1,800, watu wengi walikuwa wanapenda kuvaa saa zao katika cheni na kuzifungia katika viuno vyao. Ili kuweza kuweka salama saa zao zisivunjike na kuharibika, Levi, watengenezaji wa kwanza kutengeneza suruali za Jeans wakaamua kuweka mfuko huo mdogo mahali ambapo watu hao wangeweza kuhifadhi saa zao salama na kwa wepesi zaidi.

Hivyo ulianza kama mfuko wa kuhifadhi salama saa za mifukoni, japo baadae ukaanza kupata matumizi mengine kama kuhifadhia sarafu, tiketi za safari, kondomu, na viberiti hasa kwa watumia sigara.

Tangu hapo suruali za Jeans za aina zote zimekuwa zikitengezwa na mfuko huo mdogo bila kujali fasheni iliyopo kwa wakati huo
 
Kuna siku nimeingiza huko laini ya cm kuitoa ilinibidi niukate kwa chini na wembe
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Nikiwa na hela nyingi naweka kwenye Wallet, lakini nikibaki na noti moja tu huo mfuko unahusika maana usalama unakuwa upo juu
 
Sio jeans zote zina hicho kimfuko. Nowdays kuna jeans mifuko ya mbele pembeni imekaa kama mifuko ya suruali za kawaida( tunaita suruali za kitambaa) hizo jeans mara nyingi huwa hazina hicho kimfuko. All in all maelezo uliyotoa kuhusu hio mfuko ni sawa.
 
Mm huweka pesa ambayo sipendi iibiwe wakati wa safari, hasa kwenye daladala
 
Back
Top Bottom