Je, umewahi kutambua kwamba mfumo uleule uliomuuwa Yesu ndio uleule uliotengeneza dini ya kuzungumzia juu yake

Unahoja usikilizwe yesu alikuja kuwasanua watu.
Watu vichwa ngumu huyu ajaye wafu wataomba poo maana atakuwa mfalme wa milele
 

Kuhusu "Neno likawa mwili" (Yohana 1:14), muktadha hauzungumzii mawazo yanayogeuka kuwa vitu (mind becomes matter), bali unadai kwamba Neno wa Mungu lilidhihirika kwa Yesu. Kuingiza falsafa ya "law of attraction" katika mstari huo ni tafsiri ya mtu binafsi, si maana ya maandiko.

Na kuhusu "Mkiamini mtapokea" (Mark 11:24), Yesu hakusema imani peke yake inatosha. Biblia pia inasema: "Ikiwa tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia." (1 John 5:14). Hivyo maombi yanategemea mapenzi ya Mungu, si nguvu ya mawazo ya mwanadamu.

Qurani nayo inafundisha wazi kuwa uwezo wa kuumba ni wa Mwenyezi Mungu pekee:

"Hakika amri Yake anapotaka jambo ni kuliambia tu: 'Kuwa', nalo likawa." (Qurani 36:82)
Mwanadamu anaweza kupanga na kuomba, lakini Muumba ni Mwenyezi Mungu peke yake.

Kwa hiyo, mafundisho ya kwamba Yesu alikuja kufundisha "code za kuumba uhalisia" hayapatikani katika Injili wala Qurani. Ni falsafa ya kisasa iliyowekwa juu ya maandiko, si mafundisho ya Yesu mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…