Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Kabulala, hapa niliendesha darasa la bureI disagree with you... nadhani umekuwa katika utamaduni wa walio wengi..Tz journalists wanapenda Sana kuandika topics ambazo ni popular/rahisi kuvuna attention.. you write with your audience in mind(Ruling class in this instance)... journalists hawana muda wa kuhangaika na have nots ili kupitia wao watu wajue mbinu za kutoka ktk Hali duni..I don't blame you entirely though..maybe that channels pays you better..nimekufuatilia kitambo, every post yenye jina lako sipiti bila kusoma due to your popularity only to be frustrated with Ruling class petty stuff..am just saying you can use your popularity and brilliance to help the young and helpless society kuibua FURSA na kuwahamasisha kujikwamua kimtizamo na kimaisha..poor and unprivileged bunch needs you more than your leadership/political positions hunters club... Please take my challenge friendly..I know what you can do Pascal Mayalla..I followed you all my life and I am a sober guy.For example..Ndugai and Tulia have jobs anyone can dream of in our society..it helps this poor society little if these two exchange position and I don't think millions of poor Tzns are so interested in who has to have 8 paid government helpers or 8 government purchased and fueled V8s at their disposal.
Aisee, nimekumbuka mbali sana. Kwakweli, sijui hata nini kilitokea ila hakuna kazi nilikuwa naipenda tangu nikiwa mdogo kama UTANGAZAJI. Ilifika mahali nikawa naiba magazeti ya baba najifanya kama natangaza. Natamani siku moja nifanye hiki. Walionikatisha tamaa ni baadhi ya watangazaji. Nilitamani sana nipate nafasi hasa kwenye vipindi vya watoto, ila napo nikaambiwa lazima nikasomee. Just imagine, enzi hizo lulu anatangaza itv, alisoma chuo gani na kwa myda gani? Baadhi ya watangazaji ambao walinikatisha tamaa ji wa vituo vituatavyoWanabodi,
Mimi ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, nikitayarisha vipindi vyangu vya TV na Redio na kuvitangaza kupitia vituo mbalimbali vya Televisheni, Redio na kusambaza habari kwenye Magazeti.
Kama una kipaji cha utangazaji, au hata bila kuwa na kipaji wewe lakini unataka kuanzisha production studio yako ya kuandaa vipindi vya Redio na TV, kuna fursa ya kutengeneza pesa, hivyo karibu nitakushauri humu jf bure.
Nakiri kupandisha uzi huu, kufuatia ombi la mwana jf huyu.
Mkuu Mkaruka, ni kweli swali nililiona nikawa nakusubiria uulize, na hapa nimeliona tena, ila hujauliza, lakini kwa faida ya wengi, haya sasa naumwaga tuu huu mtama hapa jf.
Kuanzisha Kipindi Binafsi cha TV.
1.0 Kwanza uwe na wazo. Program Idea
Wazo au Program Idea ndio ndio utajiri mkubwa kuliko kitu chochote. Wazo ni kipindi kuhusu nini, maudhui ya kipindi, lenoo la kipindi ni nini?. Unataka kuonyesha nini, au watu waone nini?, jee hao watu wakiishaona hicho unachotaka kuonyesha, watapata nini?, habari, elimu, burudani, ushawishi, etc. Jee ni kipindi cha aina gani na kitaendeshwaje?.
2.0 Aina za Vipindi vya TV. Type of TV Program
Kuna aina nyingi za vipindi vya TV.
Kuna TV Documentary, TV Talk Show, TV Reality Show, TV VOX Pop, TV feature, TV Descriptive, TV Exhibition show, Live TV Broadcasting, Special TV Prog, TV Interview Prog. etc.
3.0 Mwendeshaji wa Kipindi/Mtangazaji. TV Presenter, Host, Anchor
Nani atakiendesha kipindi, Mtangazaji, kama ni wewe mwenyewe, jee una kipaji?, una uwezo?, una sauti?, unatazamika? (photogenic)
4.0 Mtayarishaji wa Kipindi /Producer
Nani atakitayarisha kipindi?, nani atakitengeneza kipindi?, yaani producers. Wako watayarishaji wa aina tatu.
4.1 TV Stations-
Vituo vya TV ndio wenye vifaa vyote vya production. Ukipeleka wazo lako kwenye TV yoyote wakiridhia TV hiyo wanaweza kukubali kuwa the producers wa kipindi chako na mkakubaliana kugawana mapato, wao watakitengeneza bure na kukirusha bure, kisha hiyo TV wakulipe wewe, au mgawane mapato.
Advantage: The easiest and the cheapest, unachohitaji wewe ni kuwa tuu na wazo la kipindi hata kama huwezi kutangaza, hiyo TV watakutafutia mtangazaji.
Disadvantage: Wazo linaweza kuibiwa, ama wanaweza kukulalia kwa kulipwa kiduchu, kisha wao ndio wakatengeneza faida.
Copyright ya Kipindi i ya TV Station, hicho lazima kirushwe na TV hiyo tuu wanayokutengenezea.
4.2 Production House/Studio.
Hizi ni makampuni ya production ambayo unapeleka wazo lako, wanakupa gharama za kukutengenezea kipindi chako, unawalipa, yaani unapewa production cost, unalipa wanakutengenezea kipindi chako. Bongo makampuni ya kutengeneza vipindi yako zaidi ya 100.
Advantage: Mkiisha kubaliana bei, kipindi kinakuwa ni mali yako na uko free kukirusha TV yoyote.
Disadvantage: Its an expensive exercise kwa sababu lazima kwanza uwe na fedha za kulipia hiyo production.
4.3 Own Production.
Hii ni baada ya kuwa na wazo, una invest kwenye vifaa, unakuwa una own a production yako mwenyewe kama mimi nilivyo na PPR.
Hivyo unatengeneza vipindi mwenyewe na kuamua utavirusha wapi. this is what I do.
Advantage: This is the best option, vipindi unatengeneza mwenyewe kwanza kwa kutafuta sponsor wa kugharimia production cost, na kuvilipia airtime cost, anakulipa wewe, kisha mwenyewe, una produce, unalipia airtime halafu pesa yote inayobakia inakuwa ni pesa yako.
Disadvantage: Its an expensive undertaking, lazima uwe na mtaji wa kununua vifaa na viko expensive, na lazima uwalipe watendakazi, ila sio lazima kuanza na kila kitu, unaweza kuanza na baadhi tuu ya vifaa vya muhimu, halafu vifaa vingine vyote ukakodisha, kila kifaa kinakodishika na gharama ni cheap kukodi kuliko kutumia pruduction house.
5.0 Vifaa vya Production.
Hivi ni vifaa muhimu kuwa navyo as Basic Equipments za Own Production
5.1 Professional Camera angalau 1 kwa kuanzia ila standard good production ni kamera 3 na kuendelea. Simple good camera ni Milioni 2, expensive ni hadi milioni 100
Kadri unavyotumia kamera nzuri, ndivyo kipindi kinakuwa kizuri zaidi. Kamera nzuri kwa Broadcast ya Tanzania ni Sony HDV ila hata SLR (hizi za still kama Canon na Nikon zina video na zinaweza), wenzetu sasa wako kwenye 4K quality, sisi bado tuko kwenye HD.
5.2 Uwe na Mic nzuri 500,000 - 2,000,000 (wireless)
5.3 Taa angalau 2, 100,000-500,000 (kwa kuanzia sio lazima sana mfano mimi vipindi vyangu vingi, navifanya nje kutumia natural light, mwanga wa jua ambao ni bure.
5.4 Editing bench ni computer ya kueditia hata any good laptop can do. Computer zinazoongoza kwa kupiga kazi ya production ni Mac (apple) ila hata Windows za kawaida zinaweza, kinachohitajika ni high specs tuu kwa upande wa graphic card
Apple Macbook Pro ya bei poa used ni 1.5 mkononi
Vifaa vyote vipya na used vinapatikana. Vyote vina faida zake na hasara zake.
Advantage and Disadvantage of New Equipments
Advantage: Vifaa vipya vina faida moja, vina good quality, vina uhakika na vina guarantee, vitadumu kwa muda mrefu kabla ya kuchoka.
Disadvantage: Vifaa vipya ni kwanza ni ghali, they are expensive lakini pia getting the genuine ones ni changamoto!, vingi ya vifaa vya producton ni famba za kutoka China na Dubai hivyo havidumu.
Advantage and Disadvantage of Used Equipments
Advantage: Vifaa used, vina faida mbili, kwanza bei yake ni cheap, pili ni vifaa genuine vya ukweli
Disadvantage: Havina guarantee na vingine vimetumika sana hadi kuchoka, hivyo unakaa navyo kidogo tuu vinachoka. technology yake imepitwa na wakati.
Yapo maduka ya vifaa vyote full iliwemo
1-Sony pale Samora.
2. Duka la Deo Filikunjombe pale NSSF Benjamin Mkapa Towers
3. AL Muntazil Mtaa wa Jamhuri.
4. Kuna duka Shoppers
5. Kuna duka Mlimani City
6. Kuna duka Quality Plaza
7. Arusha -Benson
8. Moshi-Bahsgwan
9. Mwanza-Barmedas
10. Dodoma kuna duka la Mchaga fulani Uhindini.
6.0 Gharama za Airtime, Airtime Cost
Ukifanikiwa kuanzisha studio yako na kutengeneza kipindi, ili kirushwe lazima kufanyike mambo matatu yafuatayo
6.1 Kipindi Kinunuliwe na TV Station.
Ukiishatengeneza kipindi chako, unawauzia TV Station, wao wanakupipa kiasi unachotaka na kukirusha kipindi, mapato yote ya kipindi chako ni mali ya TV Station.
Advantage: Kazi yako ni kuzalisha tuum yaani unauza kipaji, unakama fungu lako kwa ulaini.
Disadvantage: TV zetu zinatubania sana, watakulipa pesa mbuzi kisha wao ndio watazimake, ila TV za hapa wako radhi kulipia mamilioni kununua vipindi vya nje kuliko vya ndani.
6.2 Kipindi kirushwe bure na TV Stations Mgawane Mapato Co-production
Ukiisha tengeneza kipindi chako, unakipeleka TV Station kuomba kirushwe bure, kikipata wadhamini, mnagawana 50/50 na TV Stations
Advantage: Wewe unaingia ghara za kutayarisha tuu, halafu unaingiza fedha za udhamini.
Disadvantage: Ukitokea udhamini mnene, unawafaidisha TV Stations bure.
6.3 Ukirushe kwa Gharama zako.
Ukiisha tengeneza kipindi chako, unakilipia fully kukirusha kwenye TV Station
Advantage: Ukilipia kipindi, unaamua kitoke TV ngapi, unawalipa TV airtime yao wanakurushia, fedha zote ulizopata zinakuwa zako.
Disadvantage:You have to be good kupata mdhamini mzuri atakayelipa pesa za production, airtime na faida ukabaki.
Rates za Kurusha kipindi cha 30 min.
The cheapest ni TBC -TZS 2,000,000
The highest ni ITV -TZS 5,000,000
TV nyingine zote zina range hapo katikati
Ushauri kama huu niliwahi kuutoa kwa JF
Vipindi Maalum vya JF kwenye TV: Naomba Maoni Yako!
Thanks.
Pascal
Update
Wanabodi huu ni msimu wa Saba Saba. Nimejitolea kutangaza fursa za utangazaji kwa Watanzania wenye vipaji vya Utangazaji. Kama unajihisi una kipaji cha Utangazaji wa Redio na TV, mimi nimejitolea kufanya screening bure kule kwenye viwanja vya Saba Saba. Unachotakiwa kufanya ni kuwa na Kiingilio chako kwenye Saba Saba. Zoezi la Screening litafanyika Siku ya Jumamosi Tarehe 8/7/2017 kuanzia saa 8:00 mchana ndani ya ofisi za PPR ambazo ziko ndani ya viwanja vya Maonyesho.
Paskali
Habari mkuuNiko poa
Pascal Mayalla,
Katika mtandao wa YouTube inaonesha hufanyi vizuri pamoja na kuwa ni mkongwe mwenye network ya watu mashuhuri ktk jamii ya kiTanzania.
Swali ni nini kina kukwanisha pamoja na nondo zote ktk huu uzi ulioanzisha ili tusije kushindwa ktk fani hii? Woga wa waandishi, kukosekana interaction kati ya mwandishi na mhojiwa, uploading video clip zisizomvutia mtazamaji kuanzia sekunde ya 1 mpaka sekunde hata ya 60 kwa kuweka power presentation badala ya kuanza moja kwa moja na mahojiano, mwandishi kuwa msikilizaji zaidi, matayarisho hafifu ya mwandishi anapokwenda field au ktk mahojiano n.k
Pascal Mayalla naona Tanzania haina news ktk lugha ya Kiingereza, je fursa hii huwezi kuichukua maana penye ombwe kama hili mkongwe kama wewe ungeweza kufunika kwani YouTube imejaa waTanzania wanaorusha habari kwa KiSwahili tu na kwa lugha ya kugeni ni sawa na hakuna.
Source: Pascal Mayalla
Mkuu Bagamoyo, kwanza it's true mimi sifanyi vizuri kwenye you tube kwasababu page yangu ya YouTube ni personal na sio online tv ndio maana haina promo yoyote, haina subscribe wala matangazo. Najipanga ku launch on line TV huko ndio nitamwaga mavitu ya kuonyeshea ukongwe wangu.
Kwa sasa mimi bado nafanya TV Programs na corporate communications kwa wateja mbalimbali. Kuna wakati niomba ushauri huu humu jf
Vipindi Maalum vya JF kwenye TV: Naomba Maoni Yako!
Wanabodi, Salaam. Hapa jf tuko wanachama wengi wenye shughuli mbalimbali. Kikubwa tunachokifanya ni kujadili tuu issues na kuishia kutoa maoni ambayo japo mengi huishia kutekelezwa mengi ya maoni mazuri ya humu huishia humu humu bila kufanyiwa chochote kwa vile mwisho wa uwezo wetu ni...www.jamiiforums.com
P
Nakutakia kila la heri tunafuatilia jinsi wanahabari wa kiTanzania wanavyo ingia ktk mapinduzi ya kurusha habari ktk mtindo wa online.Post #88 Swali ni nini kina kukwanisha pamoja na nondo zote ktk huu uzi ulioanzisha ili tusije kushindwa ktk fani hii? Woga wa waandishi, kukosekana interaction kati ya mwandishi na mhojiwa, uploading video clip zisizomvutia mtazamaji kuanzia sekunde ya 1 mpaka sekunde hata ya 60 kwa kuweka power presentation badala ya kuanza moja kwa moja na mahojiano, mwandishi kuwa msikilizaji zaidi, matayarisho hafifu ya mwandishi anapokwenda field au ktk mahojiano n.k
Mkuu Bagamoyo, kwanza it's true mimi sifanyi vizuri kwenye you tube kwasababu page yangu ya YouTube ni personal na sio online tv ndio maana haina promo yoyote, haina subscribe wala matangazo. Najipanga ku launch on line TV huko ndio nitamwaga mavitu ya kuonyeshea ukongwe wangu.
Kwa sasa mimi bado nafanya TV Programs na corporate communications kwa wateja mbalimbali. Kuna wakati niomba ushauri huu humu jf
Vipindi Maalum vya JF kwenye TV: Naomba Maoni Yako!
Wanabodi, Salaam. Hapa jf tuko wanachama wengi wenye shughuli mbalimbali. Kikubwa tunachokifanya ni kujadili tuu issues na kuishia kutoa maoni ambayo japo mengi huishia kutekelezwa mengi ya maoni mazuri ya humu huishia humu humu bila kufanyiwa chochote kwa vile mwisho wa uwezo wetu ni...www.jamiiforums.com
P
Aisee kumbe nilipishana na furusa hii. Hata hivyo nashukuru kwa kunipatia abcd za mambo haya kwenye post hii.Wanabodi huu ni msimu wa Saba Saba. Nimejitolea kutangaza fursa za utangazaji kwa Watanzania wenye vipaji vya Utangazaji. Kama unajihisi una kipaji cha Utangazaji wa Redio na TV, mimi nimejitolea kufanya screening bure kule kwenye viwanja vya Saba Saba. Unachotakiwa kufanya ni kuwa na Kiingilio chako kwenye Saba Saba. Zoezi la Screening litafanyika Siku ya Jumamosi Tarehe 8/7/2017 kuanzia saa 8:00 mchana ndani ya ofisi za PPR ambazo ziko ndani ya viwanja vya Maonyesho.