Je, Una Kipaji cha Utangazaji? Jinsi ya Kujiajiri Utayarishaji na Utangazaji Vipindi Vyako vya TV

Mkuu Kabulala, hapa niliendesha darasa la bure
P
 
Aisee, nimekumbuka mbali sana. Kwakweli, sijui hata nini kilitokea ila hakuna kazi nilikuwa naipenda tangu nikiwa mdogo kama UTANGAZAJI. Ilifika mahali nikawa naiba magazeti ya baba najifanya kama natangaza. Natamani siku moja nifanye hiki. Walionikatisha tamaa ni baadhi ya watangazaji. Nilitamani sana nipate nafasi hasa kwenye vipindi vya watoto, ila napo nikaambiwa lazima nikasomee. Just imagine, enzi hizo lulu anatangaza itv, alisoma chuo gani na kwa myda gani? Baadhi ya watangazaji ambao walinikatisha tamaa ji wa vituo vituatavyo
RFA, STARTV, LIVING WATERS, CLOUDS (walikuwa na kipindi cha watoto maarufu kama chuchuchu academy kikiongozea na marehemu Amina Chifupa, Masoud Kipanya na jamaa mmoja sijui aliishia wapi aliitwa Kaka Bonda) ndoto ikawa imekufa hapo. Nikaamini Tanzania bila connection hata mkate utahitaji shoka kuukata. pascal mayala kama ningekufahamu enzi hizo may be leo ningekuwa naziishi ndoto zangu.
 
Pascal Mayalla,

Katika mtandao wa YouTube inaonesha hufanyi vizuri pamoja na kuwa ni mkongwe mwenye network ya watu mashuhuri ktk jamii ya kiTanzania.

Swali ni nini kina kukwanisha pamoja na nondo zote ktk huu uzi ulioanzisha ili tusije kushindwa ktk fani hii? Woga wa waandishi, kukosekana interaction kati ya mwandishi na mhojiwa, uploading video clip zisizomvutia mtazamaji kuanzia sekunde ya 1 mpaka sekunde hata ya 60 kwa kuweka power presentation badala ya kuanza moja kwa moja na mahojiano, mwandishi kuwa msikilizaji zaidi, matayarisho hafifu ya mwandishi anapokwenda field au ktk mahojiano n.k

Pascal Mayalla naona Tanzania haina news ktk lugha ya Kiingereza, je fursa hii huwezi kuichukua maana penye ombwe kama hili mkongwe kama wewe ungeweza kufunika kwani YouTube imejaa waTanzania wanaorusha habari kwa KiSwahili tu na kwa lugha ya kigeni ni sawa na hakuna.

Source: Pascal Mayalla
 
Mkuu Bagamoyo, kwanza it's true mimi sifanyi vizuri kwenye you tube kwasababu page yangu ya YouTube ni personal na sio online tv ndio maana haina promo yoyote, haina subscribe wala matangazo. Najipanga ku launch on line TV huko ndio nitamwaga mavitu ya kuonyeshea ukongwe wangu.

Kwa sasa mimi bado nafanya TV Programs na corporate communications kwa wateja mbalimbali. Kuna wakati niomba ushauri huu humu jf


P
 

Wakongwe ktk fani kama wewe huwa tunawafuatilia kama role model wetu hivyo hatuoni sababu yoyote kushindwa kupata views za kutosha YouTube hasa tukiangalia tv presenters wengine wana channel zao YouTube ambapo pia huwa wana views nyingi.

Hivyo ushauri wangu ktk post yangu ya mwanzo inaweza kukusaidia wakati unapanga mikakati hiyo ya ujio mpya ktk online TV.
Nakutakia kila la heri tunafuatilia jinsi wanahabari wa kiTanzania wanavyo ingia ktk mapinduzi ya kurusha habari ktk mtindo wa online.
 
Wewe ni mtu ulieshiba madini sana hongera sana,nisaidie haya jee radio zinazorusha matangazo ya radio km dw, VOA,BBC kwa hapa nchini zinalipwa? Na sasa TV zimeanza kurusha matangazo nisaidie hilo ahsante sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka mayalla, mimi na demo ya kipindi cha tv toka mwaka 2015 ninacho mkononi. Till leo nipo wenge tu sielew nifanye nn au nimuone nani. Mana nishafanya attempts za kufika media houses (Eatv, cloudstv, Azamtv) , naambiwa demo niiache getini kwa mlinzi. Naomba MSAADA WA KUMEET THE RIGHT PERSONELs.
 
Aisee kumbe nilipishana na furusa hii. Hata hivyo nashukuru kwa kunipatia abcd za mambo haya kwenye post hii.
 
Kaka mkubwa Pascal Mayalla
Nimepitia, kwa kweli nondo zenye kufaa zote umeziweka bayana.

Kama itakupendeza naomba kuuliza swali moja
Mtu sahihi wakuonana nae kwenye hizi media kwa ajili ya kufikisha vipindi ni nani

Programu meneja, meneja masoko au nani hasa ndie anausika moya kwa moya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…