Je una uhakika yale unayofunga na kuomba ndio GOD'S WILL aliyo nayo juu yako?

Design Your Idea

Senior Member
Joined
Jun 3, 2024
Posts
154
Reaction score
480
“si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.” (Luka 22:42)

Setfree
Psalm_23
Psalm 103
StudentTeacher

Ni ipi siri ya maisha, ni kipi kipo nyuma ya ukweli wa maisha yetu.

Nani ni muendeshaji wa kila hatua na kuanguka katika maisha yetu?

Je kila mtu amewekewa limits na amekuwa regulated hata afanye hawezi shuka au panda zaidi ya mstali aliopigiwa?
 
Zaburi 24:1
"Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakao ndani yake"

Nadhani ni yule alie kuumba na kukukirimia zawadi ya uhai na afya bila malipo, ndie peke anae regulate maisha ya kila aliemuumba for free too 🐒
 
“si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.” (Luka 22:42)

Setfree
Psalm_23
Psalm 103
StudentTeacher

Ni ipi siri ya maisha, ni kipi kipo nyuma ya ukweli wa maisha yetu.

Nani ni muendeshaji wa kila hatua na kuanguka katika maisha yetu?

Je kila mtu amewekewa limits na amekuwa regulated hata afanye hawezi shuka au panda zaidi ya mstali aliopigiwa?
Kuna sheria za ulimwengu, arafu kuna self awareness, hivyo ndivyo vinavyoaply kwenye maisha yetu, ulivyo ni matokeo ya kile unachokijua, bahati mbaya asili inatoa matokeo kulingana na sheria zake uwe unajua au hujui. Ila wengi wetu hatujijui tupo shaped na mazingira tuliyokulia, hivyo kufunga na kuomba ni sehemu ya kujiambatanisha na asili, kwa kuwa unapoomba unakuwa unacommand vitu viwe hiyo ni nguvu ya maneno (mantra), kufunga ni kuupa mwili nguvu ya ndani na kukuongezea nidhamu ya maisha, hivyo matokeo yapo mikononi mwako mwenyewe.
 
Laws of attraction
 
“si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.” (Luka 22:42)

Setfree
Psalm_23
Psalm 103
StudentTeacher

Ni ipi siri ya maisha, ni kipi kipo nyuma ya ukweli wa maisha yetu.

Nani ni muendeshaji wa kila hatua na kuanguka katika maisha yetu?

Je kila mtu amewekewa limits na amekuwa regulated hata afanye hawezi shuka au panda zaidi ya mstali aliopigiwa?
Kufunga na kuomba sio mbadala wa Maarifa. Kuna baraka zinafunguka zenyewe effortlessly ili mradi tu uwe na ufahamu hususani wa Ki-Mungu kuzihusu. Vinginevyo utapoteza nguvu zako bure!

HOSEA 4
6 Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.

Ndio maana kila mlango una funguo zake na haziingiliani. Jambo linalohitaji Maarifa tafuta Maarifa yake tena kwa kina na sio kuliombea. Jambo linalohitaji kuliombea,liombee!. Muhimu uwe na Hekima ya kuweza kupambanua which is which.

Kwenye kuendesha maisha yetu wanadamu tuna options mbili.
1. Kutumia akili zetu wenyewe
2. Kumtumaini Mungu kwenye kila jambo

Ukichagua kuishi kwa kuzitumainia akili zako mwenyewe jiandae kwa lolote wakati wowote kwa sababu kuna mambo yapo mbali na upeo(akili) zako.

Kuchagua kumtumaini Mungu ni kuchagua kuukaribisha Uwepo na Uwezo wa Mungu uambatane pamoja nawe wakati wote,hivyo pale ambapo uweza wako wa kibinadamu unaishia,uweza wa Mungu unakuhuisha na kukuvusha kimiujiza kabisa(no limits).

Ingawa kuna wakati ili uweze kulitimiza kusudi lake kwa wakati,watu na mazingira husika, Mungu hukuandaa kabla. Maandalizi hayo kuna wakati yanahusisha maumivu mfano kufilisiwa,kuachwa,kutengwa,kudharauriwa n.k. Zote hizi zikiwa ni jitahada za makusudi kabisa tena za kimkakati za Mungu mwenyewe katika kukutengenezea mazingira ya kuupokea msimu mpya(Greater Glory). Kumbuka Mungu hakupi mambo ambayo haujawa tayari kuyapokea wala kuyatunza hata kama unayatamani kiasi gani.

Kwa kifupi,mtu aliyechagua kuishi kwa kumtumaini Mungu completely,maisha yake kwa ujumla huwa under God's control. Mungu ndiye anaamua uoe au uolewe na nani. Ufanye kazi au biashara gani,uishi nchi au mkoa gani n.k. Sio hivyo tu Mungu anakupangia mpaka marafiki wa kuambatana nao. Na uzuri ana namna yake ya kuwapima with respect to you and your life purpose!

MITHALI 3
5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.
 
“si mapenzi yangu, bali yako yatendeke.” (Luka 22:42)

Setfree
Psalm_23
Psalm 103
StudentTeacher

Ni ipi siri ya maisha, ni kipi kipo nyuma ya ukweli wa maisha yetu.

Nani ni muendeshaji wa kila hatua na kuanguka katika maisha yetu?

Je kila mtu amewekewa limits na amekuwa regulated hata afanye hawezi shuka au panda zaidi ya mstali aliopigiwa?
Asante mkuu... nitarudi baadae..
 
Back
Top Bottom