Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Katika zama hizi za utandawazi, usafiri umekuwa sehemu muhimu ya maisha yetu ya kila siku. Tunaweza kusafiri kwa ndege, treni, basi, gari, pikipiki, au hata kwa miguu. Hata hivyo, pamoja na urahisi huu wote, bado tunakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na ucheleweshaji, ajali, na huduma mbovu za vyakula.
Mwaka wa 2020, nilisafiri kutoka Mwanza kuelekea Dar es Salaam kwa basi la Kisesa. Safari hiyo ilikuwa ndefu na yenye changamoto nyingi, na hatimaye nililazimika kushukia Dodoma kutokana na matatizo ya mara kwa mara ya basi hilo. Majanga yalianzia Tinde kwenye mizani, gari lilizima na ikabidi dereva na watu wachache kusaidia kutatua tatizo, ila baada tena tukiwa Tabora gari ikazima kwa mara nyingine.
Tokea tumeanza safari Nyegezi niliona wazi kuwa Basi hili halipo sawa, sikutaka kumshawishi mtu yoyote kuteremka ila nilitumia ubinadamu kuwaomba niteremke Dodoma ingawa safari iliikuwa ni ya kwenda Dar es Salaam ili tu nisipate karaha zaidi.
Naomba kukualika kushiriki uzoefu wako wa usafiri. Ni nini kilichokuwa kibaya zaidi? Je, uliwahi kusafiri kwa gari iliyokuwa katika hali mbaya? Je, umewahi kukwama barabarani kwa muda mrefu? Je, umewahi kupata ajali ya barabarani?
Ulipata huduma ya chakula kibaya? Kusimamishwa na maafisa usalama? Unaweza kushare chochote? Hadithi yako inaweza kuwa ya kuchekesha, ya kusikitisha, au hata ya kutisha. Kama Jamii tunaomba kusikia kutoka kwako! Wapo waliopata wachumba, waliopata connection za kazi na kadhalika.
Kwa kushiriki uzoefu wako wa usafiri, tunaweza kuunganisha pamoja na kujenga jamii yenye uelewa zaidi kuhusu changamoto za usafiri. Tunaweza pia kuhamasisha mabadiliko katika sekta ya usafiri kwa kuwajibisha makampuni ya usafiri na mamlaka husika.
KARIBUNI SANA!