Je, unaamini katika kuwekeza? Nina wazo la biashara kuanzia 10/20m ( kuuza unlimited internet buku tu kwa siku mteja atatumia hata gb 500 yeye tu

Hii biashara kama huna namna ya kuzuia mtu unae Muuzia kusambaza kwa mwingine basi hakuna kitu hapa

Mfano nikiwa na laptop yangu naweza gawa Wireless nyumbani kwa familia au ofisini au mtaani kwa wadau kwa buku niliyolipia...!

Una wezaje kuboresha ulinzi wa huduma ili iwe kwa aliyelipia , yani atakayelipia ndiye atakaye hudumiwa
 
Yes iko namna tayari ya kuzuia na ku monitor
 
Mkuu

Una maono mazuri sana ya fursa ubarikiwe sana kwa kushare nasi hizi fursa
Naomba kuuliza swali hapa ikiwa nime funga kifaa hicho kwa mteja endapo hajalipia au ana sua sua naweza ku-control hicho kifaa kikiwa kwake na maanisha kukizima au kupunguza speed au kutuma ujumbe wa kulipia kwenye simu yake?
 
Wazo zuri nataka nitest kwanza kwa kuanza na 1M
vipi kuhusu kupotea vifaa (90k each) bila shaka vinafungwa kwa mteja akisepa navyo??
Limitation au range ya network ikoje?
 
kwann mkuu usifungue kampuni iwe kwa share!!
Mi ningenunua hata 20% share kuweka hela yote hiyo kwa pilot ni risk
 
Huduma ni pre paid hivo mteja analipa kisha anapata huduma asipolipa anakuwa disconnected kupitia system kwaio hapati
 
Wazo zuri nataka nitest kwanza kwa kuanza na 1M
vipi kuhusu kupotea vifaa (90k each) bila shaka vinafungwa kwa mteja akisepa navyo??
Limitation au range ya network ikoje?
Kila biashara ina risk namna pekee yw kupunguza risk nikujua unafanya biashara na mtu wa aina gani huduma hii inamfaa kila mmoja ila sio kila mmoja anastahili

Kuhusu range kumbuka kila mtu anayake hivo basi minimum huwa mita kuanzia 10meter
 
Ni wazo zuri sana na linatekelezeka.

Ova
 
ANGALIZO #1: Ukivuka matumizi ya GB 1000 speed inashuka inakuwa kama kobe mpaka mwezi ujao ukilipia tena

ANGALIZO #2: hakikisha una router nzuri ya kulimit speed na matumizi kwa siku, kila mtu muwekeem limit mfano GB 3.5 kwa siku ili wasivuke GB 1000 kwa mwezi, pia router iwe ina limit speed maana kuna watu wakianza kudownload wanakomba speed yote


ANGALIZO #3 20 Mbps inaweza kuwa ndogo sana kwa watu 10,

1 Mbps = 0.125 MBps

Mbps (Megabits per second / Megabits kwa sekunde)
kipimo cha speed ya internet kwa wanaotoa huduma ya internet mfano voda.

MBps - (Megabytes per second / Megabytes kwa sekunde)
kipimo chetu watumiaji, zingatia herufi kubwa MB, huwa tunaweza kuiona tunapo download mafaili,

mfano ukitaka kudownload faili kwenye kifurushi cha 20 Mbps, ni kwamba utaweza kushusha MB 2.5 kwa sekunde ila kibongonongo ni MB 2 kwaa sekunde sababu network hazipo stable.

ukiunga watu 10 hapa kila mtu anaweza pata speed ya 0.2 MB kwa sekunde, inafaa kwa wanaochati na kucheki picha ila kwa wale wa insta, tiktok, youtube, n.k. ni ndogo.
 
Asanteh mkuu hii imezingatiwa na hili tulilenga watumiaji wa kawaida kwa heavy duty tunachofanya ni kuongeza Mbps tu hivo itatolewa kulingana na matumizi halisi ila kiufupi tumelenga ndugu zetu wenye matumizi ya kuperuzi kawaida
 
Asanteh mkuu hii imezingatiwa na hili tulilenga watumiaji wa kawaida kwa heavy duty tunachofanya ni kuongeza Mbps tu hivo itatolewa kulingana na matumizi halisi ila kiufupi tumelenga ndugu zetu wenye matumizi ya kuperuzi kawaida
ni biashara niliyowahi kuwa msaidizi miaka ya 2003 hadi 2005, enzi hizo za ttcl internet cafes zimejaa kinoma, pesa ipo watu wanapenda sana net

nikitaka kurudi hii biashara ntawekeza kwenye router zaidi, sio hizi za kawaida tunazopewa, yani kila mtu aenjoy kwa budget, router za kawaida sio nzuri kwa biashara.
 
Karibu kwenye gemu mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…