Ni muda mrefu naona watu maeneo mbali mbali mtandaoni wako serious na haya mambo kuliko miaka ya nyuma.Nadhani ukuaji wa Technology umechangia,watu wanasoma na kufuatilia tabiri viganjani mwao tofauti na enzi hizo unazikuta kwenye magazeti ama umfuate sheikh/maalim magomeni🙃
Imefikia hatua hata katika masuala ya kutafuta wenza wanaangalia nyota,kwenye masuala ya kazi,ajira,biashara nk.
Mfano mwenye nyota ya asili ya maji,unaambiwa upo compatible na unaendana mwenye nyota Fulani yenye asili ya maji au nyota Fulani yenye asili ya udongo nk
Mwenye nyota asili ya hewa unanendana na nyota Fulani -nyota Fulani na Fulani mkioana hamtisha kuelewana uwezekano wa mahusiano kudumu ni mdogo
-kwenye masuala ya kazi na biashara pia wanaaplly asili ya nyota mfano moto,udongo,hewa,maji nk.
Kazi ama biashara inayofanya iwe inaendana na asili yako ndipo utaona mafaanikio
Kuna baadhi ya watu wanaamini ni kweli na Kuna baadhi wanaamini ni ushirikina.
Je Kwa upande wako unafuatilia masuala yahusuyo nyota?
Tabiri zake
Elimu yake Kwa ujumla?
Je ni kweli ama utapeli?
Toa Maoni yako
Astrology mara nyingi huonekana kama swali la: “Mimi ni Simba, Ng’ombe, Pisces, Ng’e au Capricorn?” Lakini hili ni swali la juu juu. Swali la chini kabisa ni: Je cosmos (ulimwengu wote) ina uhusiano wowote na consciousness inayoiangalia? Kwa sababu kuna mambo mawili: Ulimwengu unaotazamwa Na Mtu anayeutazama. Nyota zipo nje. Lakini maana ya nyota iko wapi? Je ipo kwenye nyota? Au ipo kwenye akili ya anayezitazama? Fikiria nyota mbili angani. Mwanasayansi anaona plasma, gravity, radiation na nuclear fusion. Mshairi anaona uzuri. Muumini anaona ishara ya Muumba. Mtabiri anaona destiny. Baharia anaona direction. Mtoto anaona mwanga. Nyota ni ileile. Lakini tafsiri zinatofautiana. Hivyo swali linakuwa: Je tunasoma nyota au tunasoma nafsi zetu kupitia nyota?
“Mimi ni scorpio.” Sentensi hii inaonekana ndogo. Lakini ndani yake kuna falsafa nzima ya identity. Unaposema: “Mimi ni Scorpio.” umeanza kujipa definition. Lakini kabla hujajua kwamba wewe ni Scorpio, ulikuwa nani? Kabla hujajua zodiac yako, ulikuwa na hasira? Ulikuwa mkarimu? Ulikuwa mwoga? Ulikuwa jasiri? Ulikuwa mtu wa upweke? Au ulianza kujitafsiri hivyo baada ya kupewa lugha ya kujielezea? Hapa ndipo akili inakuwa hatari. Kwa sababu mwanadamu anaweza kupewa label, akaanza kuiishi, kisha baadaye akasahau kwamba label ndiyo ilikuja baada yake. Mtu anaambiwa: “Wewe ni stubborn.” Anaanza kuiona stubbornness kila mahali. Anaambiwa: “Wewe ni emotional.” Anaanza kutafsiri maamuzi yake yote kupitia emotion. Anaambiwa: “Wewe hupaswi kuendana na mtu wa zodiac fulani.” Anaanza kuona matatizo ambayo bila hiyo imani huenda asingeyaona. Hii inatuonyesha jambo kubwa: Imani haielezi tu reality; wakati mwingine huanza kushiriki kuitengeneza.
Mtu anaweza kusema: “Mimi ni Simba, ndiyo maana nina tabia hii.” Lakini swali la Bless on ni: Je umeonyesha tabia hii kwa sababu ulizaliwa Simba au baada ya kuambiwa wewe ni Simba ukaanza kujitafsiri kupitia utambulisho huo? Hili ni swali zito. Kwa sababu akili ya mwanadamu haipokei taarifa kama kamera isiyo na hisia. Akili huchagua, huchuja, huunganisha na kutengeneza simulizi. Ukiambiwa: “Una moyo mzuri, lakini wakati mwingine unapenda kuwa peke yako.” Huenda ukasema: “Hiyo ni mimi kabisa!” Lakini watu wangapi wanaweza kujiona ndani ya sentensi hiyo? Wengi. Kwa nini? Kwa sababu sentensi hiyo ina sehemu mbili zinazogusa uzoefu mpana wa binadamu: tunataka kupendwa, lakini pia wakati mwingine tunataka kuwa peke yetu. Hapa ndipo saikolojia inapoingia kwenye mlango wa astrology. Kuna jambo linalojulikana kama Barnum effect - mwelekeo wa binadamu kuona maelezo ya jumla kama kwamba yameandikwa mahsusi kwa ajili yake. Hii haimaanishi kila mtu anayesoma horoscope ni mjinga. La. Inamaanisha tu kwamba akili ya mwanadamu ina uwezo mkubwa wa kujitambua ndani ya maelezo ambayo yanaweza kuwahusu watu wengi. Na hili ni somo kubwa sana kuhusu consciousness.
Akili ya mwanadamu ina tabia moja ya ajabu: inapenda patterns. Ukiona matukio matatu yanafanana, akili yako inaanza kutafuta connection. Ukiota mtu halafu kesho akakupigia simu, unashtuka. Lakini je uliota watu wangapi ambao hawakukupigia? Ulisoma horoscope ikasema utakutana na mtu muhimu. Ukakutana na mtu muhimu. Unasema: “Ilikuwa sahihi.” Lakini horoscope ilitabiri mara ngapi kitu ambacho hakikutokea? Hapo tunagusa kitu kinachoitwa confirmation bias. Mara nyingi akili haikusanyi ushahidi wote kwa usawa. Inapenda kukumbuka kile kinachothibitisha kile ilichokwisha kuamini. Hii si kasoro ya watu wa astrology pekee. Ni udhaifu wa kawaida wa human cognition. Na hii ndiyo sababu mtu mwenye akili kubwa si yule anayesema: “Nimeona ikitokea, kwa hiyo ni kweli.” Bali yule anayesema: “Ni mara ngapi haikutokea?”
Je sayari zina nguvu juu yetu? Hili ni swali ambalo halipaswi kujibiwa kwa kejeli. Jua lina nguvu juu ya maisha duniani. Mwezi una athari halisi katika mfumo wa Dunia, ikiwemo mawimbi ya bahari. Gravity ipo. Radiation ipo. Mwendo wa vitu vya angani una madhara halisi katika mazingira ya cosmic. Lakini hapa ndipo tunahitaji kutenganisha mambo mawili: “Sayari inaweza kuniathiri.” Na “Nafasi ya sayari wakati nilipozaliwa ndiyo iliyoandika tabia yangu.” Hayo si madai yanayofanana. Kuna pengo kubwa la kimantiki kati yake. Ni kama kusema: Moto unaweza kukuchoma. Kwa hiyo: mahali moto ulipokuwa siku ulipozaliwa ndiyo panaamua personality yako (Hapana). Kuwepo kwa influence moja hakuthibitishi aina nyingine ya influence. Na hii ni kanuni muhimu sana katika kufikiri: Uhusiano unaowezekana si ushahidi wa causation.
Angalia BirtH CharT: je sekunde moja inaweza kugawa hatima? Astrology inampa umuhimu tarehe, muda na mahali pa kuzaliwa. Sasa fikiria watoto wawili. Mmoja anazaliwa saa 12:00. Mwingine saa 12:01. Dunia haikusimama. Mifumo ya anga haikufanya sherehe. Lakini chart inaweza kubadilika kulingana na mfumo na vipengele vinavyohesabiwa. Sasa jiulize: Ni nini hasa kinachobeba causal power? Dakika? Angle? Planet? House? Symbol? Au tafsiri ya mwanadamu? Swali hili halikusudii kudhalilisha astrology. Linataka kuifanya isimame mbele ya mahakama ya epistemology: “Unajuaje unachodai unakijua?” Hili ni swali ambalo kila mfumo wa maarifa lazima ulijibu.
Mapacha wanaweza kuzaliwa karibu sana. Wanaweza kushiriki mazingira ya mwanzo, genes nyingi na wakati wa kuzaliwa. Lakini hawawi watu wawili wanaofanana kabisa. Mmoja anaweza kuwa mpole. Mwingine mkali. Mmoja akapenda biashara. Mwingine akapenda sanaa. Mmoja akapata mafanikio mapema. Mwingine akahangaika kwa miaka mingi. Hii inatukumbusha: Binadamu si bidhaa ya variable moja. Maisha yana layers. Genes. Environment. Parenting. Culture. Education. Trauma. Opportunity. Choice. Chance. Relationships. Na kitu kingine kisichopimika kwa urahisi: consciousness. Kwa hiyo ukisema: “Nyota ndiyo sababu.” unapaswa kujiuliza: “Nyota imeeleza sehemu gani ya equation na ni sehemu gani nimeacha nje?”
Destiny vs Free Will: Hapa ndipo astrology inakutana na moja ya vita vya zamani kabisa vya falsafa. Je maisha yameandikwa au tunaandika maisha? Kama kila kitu kimeamuliwa: Kwa nini nijitahidi? Kwa nini nijifunze? Kwa nini nibadilike? Kwa nini nichague? Lakini kama kila kitu kiko mikononi mwangu: Kwa nini nimezaliwa kwenye familia ambayo sikuchagua? Kwa nini nimepewa mwili ambao sikuchagua? Kwa nini nimezaliwa katika karne hii? Kwa nini nimekutana na watu ambao sikuwapanga? Kwa nini matukio mengine yametokea bila ruhusa yangu? Hapa tunagundua kitu cha ajabu: Huenda hatuchagui uwanja ambao tunacheza. Lakini tunaweza kuwa na kiwango fulani cha uchaguzi ndani ya uwanja huo. Huwezi kuchagua jana. Lakini unaweza kuchagua unachofanya na jana. Huwezi kuchagua ulivyozaliwa. Lakini unaweza kuchagua sehemu ya kile utakachokuwa. Huwezi kuamuru upepo. Lakini unaweza kurekebisha tanga. Na labda hii ndiyo maana halisi ya freedom: Si uwezo wa kudhibiti kila kitu; ni uwezo wa kuitikia kile usichoweza kudhibiti.
Kama nyota zinaandika destiny, basi mwanadamu ni nini? Hili ni swali la kuchoma. Kama kila tabia yako imeandikwa na nyota... wewe ni nani? Kama hasira yako ni Mars... Kama mapenzi yako ni Venus... Kama bahati yako ni Jupiter... Kama vikwazo vyako ni Saturn... Basi mhusika halisi ni nani? Je wewe ni mwili unaotekeleza script ya cosmos? Au kuna consciousness ndani yako inayoweza kuiona script, kuihoji na hata kuibadilisha? Kwa sababu ukisema: “Mimi nimeandikiwa kuwa hivi.” umeshaanza kupoteza kitu muhimu: responsibility. Na pale destiny inapogeuka kuwa kisingizio, spirituality inaweza kuwa kifungo. Kuna tofauti kati ya kusema: “Hii ni pattern ninayoweza kuitafakari.” na: “Hii ndiyo mimi, siwezi kubadilika.” Ya kwanza inaweza kufungua akili. Ya pili inaweza kuifunga. Usiseme: “Siwezi kuwa na relationship nzuri kwa sababu zodiac zetu haziendani.” Labda tatizo si nyota. Labda hamjui kuwasiliana. Usiseme: “Mimi ni mtu wa hasira kwa sababu ya sign yangu.” Labda unahitaji emotional regulation. Usiseme: “Destiny yangu ni umasikini.” Labda hujapata opportunity. Usiseme: “Mimi siwezi kubadilika.” Hapo tatizo si astrology. Tatizo ni kwamba umeanza kuabudu definition yako mwenyewe.
Astrology inaweza kuwa kioo. Na hapo ndipo ninapoona eneo la kuvutia sana. Kioo hakikuumbi. Kioo kinakupa taswira. Ukijitazama kwenye kioo na kuona umechoka, kioo hakikuchoshi. Ukiona umezeeka, kioo hakikukuzeesha. Ukiona umefurahi, kioo hakikufurahishi. Kioo kinaonyesha. Kwa mtazamo huu, astrology inaweza kuchukuliwa na baadhi ya watu kama lugha ya symbolism inayowasaidia kutafakari nafsi. Lakini kuna tofauti kubwa kati ya: “Hii imenisaidia kujitafakari.” na: “Hii imethibitisha kwamba universe imeamua maisha yangu.” La kwanza ni tafakuri. La pili ni claim ya cosmology. Na claims kubwa zinahitaji ushahidi mkubwa. Kwani horoscope inaweza kubadilisha maisha bila kubadilisha nyota. Hii ndiyo paradox. Mtu anaambiwa: “Leo usiogope kuanza.” Anaanza biashara. Anafanikiwa. Anasema: “Nyota zangu zilijua.” Lakini labda nyota hazikufanya chochote. Taarifa ilibadilisha mindset. Mindset ikabadilisha decision. Decision ikabadilisha action. Action ikabadilisha outcome. Kwa hiyo wakati mwingine kitu tunachokiita: “utabiri” kinaweza kufanya kazi kupitia behavioral pathway. Si lazima prediction yenyewe iwe na nguvu ya supernatural. Huenda nguvu ilikuwa kwenye kile mtu alichofanya baada ya kuamini prediction. Na hapa kuna swali ambalo linapaswa kukaa kichwani: Je unachokiita “destiny” wakati mwingine ni matokeo ya maamuzi ambayo uliyaanza kwa sababu uliamini destiny? Hii ni paradox yenye sumu tamu.