Je, unaamini kuwa uchawi upo?

Kama uchawi upo mbona hatuoni wakiwa na maendeleo?,ukifuatilia wengi wao hao wanaoitwa wachawi ndio wanamaisha magumu. Na kama uchawi upo unawasaidia nini? Lol
 
Wanao wa aminisha watu kuwa uchawi haupo ni wanasiasa wa chama Tawala, kwa sababu wao ni washirikina wakubwa! Kama unakubali uongo wao, ingia kwenye SIASA UKAJIONEE MWENYEWE!
 
kimsing uchawi upo tena ni hatari mno.muamini MUNGU kwa dhat uchawi ni historia kwako.
 
uchawi upo tangu enzi za biblia - ukisoma habari za Musa wakati wa ukombozi wa wana wa israel - Farao aliwatumia wachawi

Pia wengi ambao ni waganga mchana ndio hao hao wachawi usiku.

Pia unapomwona mtu anakutokea "live" usiku - amekusimamia - naye anatoka mbali - nawe huoti - uko macho - huyo si mchawi jamani???

UCHAWI UPO - ni nguvu za giza ila DAIMA NGUVU ZA MUNGU NDIO KIBOKO YAKE
 

kwanini yanatokea uswahilini peke yake? Toka nimezitupilia mbali hizi hofu...sijawahi kabwa wala kuota mandoto ya ajabu ajabu
 
uchawi upo kabisa, kuna watu wanatuma radi na wengine huko ukerewe wanafuga mamba na kuwatumia kichawi.
 
Na ukitaka kuamini hili na kurogwa kabisa basi we kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja halafu wajuane.
Nalog off
 
wengine wanasema Mungu hayupo,but kwavile naona maajabu ya shetani basi naamini pia Mungu yupo na anatuliza
 
Uchawi ulikuwepo zamani hata maandiko matakatifu ya dini zote yanakiri hilo, ila Siku hizi imebaki mazingaombe na utapeli
 
mapenzi ni sanaa kama zile za bongo movie mtu akiishugurisha akili yake kwa nia ya kujenga penzi utasikia ooh yule jamaa kalishwa shuntama,kumbe hakuna ila ni kufuata taratibu za ndoa tu
 
Nimepatwa na majanga; nyumba yangu imewaka moto,chanzo haijulikani mpaka ndahuu,mezailiyo kuwa imebeba sabufa imeugua jumla hakuna waya ulio konectiwa kwenye umeme wala hakuna moto wowote uliokuwa ndani;
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…