Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kimsing uchawi upo tena ni hatari mno.muamini MUNGU kwa dhat uchawi ni historia kwako.Siku nyingi nimekuwa siamini kama kweli kuna uchawi katika Tanzania hii, achilia mbali huko kwa wengine. Nimekuwa siamini kwa sababu makosa yote hapa nchini yana adhabu zake isipokuwa la uchawi hii ikimaanisha kuwa Serikali inaamini kuwa hakuna uchawi. Hatahivyo, siku za hivi karibuni imani yangu imeanza kupungua baada ya Kiongozi mmoja katika Serikali hiyo hiyo inayoamini kuwa hakuna uchawi kudai kuwa amegundaua mbinu kuwa anarogwa ili awe zoba auwawe kirahisi. Sasa nikajiuliza, huyu mtu yumo ndani ya Serikalini inayoamini kuwa hakuna uchawi, akiwa pekee yake kuna uchawi, inakuwaje hapa?
Aidha, jana tarehe 28/03/2011 nilikuwa nasikiliza Redio Wapo FM kuanzia saa 1.30 jioni kipindi cha yaliyotufikia nikasika kuwa kuna fisi ameshambulia watu huko Mto wa Mbu, akauawa na askari wa wanyama pori, baada ya kuuawa, wakakuta ametobolewa masikio kama alikuwa anawekewa hereni.
Je, huyu fisi alikuwa anashiriki mashindano ya Miss Mto wa Mbu au ni fisi wa wachawi?
Sasa wana JF wenzangu ni kweli kuna uchawi? Au ni njama za wajanja kutishia wenzao.
Jamani nawakaribisha huku uswazi mjionee .Uchawi umekua kero kubwa huku ni kawaida watu kuona wazee waliofariki maeneo ya chooni,kelele za wanyama ambazo zinafanana na sauti ya binadamu,watu kukabwa usiku ,kuugua magonjwa ambayo hospitalini hayaonekani na kadhalika.
Na ukitaka kuamini hili na kurogwa kabisa basi we kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja halafu wajuane.
Nalog off
hao wana zali kinoma.watu wana wake wanne na hawarogani labda km uoe wachawi
Uchawi ulikuwepo zamani hata maandiko matakatifu ya dini zote yanakiri hilo, ila Siku hizi imebaki mazingaombe na utapeli
Ya labda umeoa wachawi,ila mpaka wote wawili waolewe na wakakubali nadhani watakuwa wanapendana tuwatu wana wake wanne na hawarogani labda km uoe wachawi
Mazingaombwe na uchawi vinatofautianaje!?
Mazingaombwe na uchawi vinatofautianaje!?