Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,891
Ndiyo.
Kuna jamaa yangu mmoja alihamia kwe nye nyumba moja na baada ya muda alikuwa akikutana na mauza uza ndani mwake,kama vile kuamka asubuhi na kukuta sebuleni kuna mabaki ya chakula ambacho wao hawakupika usiku wa kuamkia siku hiyo n.k
Aliamua kuhama na nilikwenda kumsaidia kuhamisha vitu,siku ya kuhamisha na mimi nikiwemo tulianza kuhamisha vitu na kikabaki kitanda na sofa moja chumbani,wakati niko mimi na jamaa yangu huyu tukikifungua kitanda ili tukipeleke kwenye gari sofa iliyokuwemo mule ndani ilianza kuwaka moto wa ghafla tena moto mkubwa ajabu
Ilibidi tuanze kulizima kwanza na kisha tukaendelea kufungua kitanda ni kukihamisha,kumbuka mule ndani tulikuwa wawili tu na lile sofa lilikuwa mbali na mlangoni na dirishani pia
Unaweza kuniambia kilichosababisha hilo tukio achilia mbali jamaa yangu kuamka karibia kila asubuhi na kukuta watu wamekula pilau na kuacha vipande vya kuku sebuleni?