Ukiniuliza Serikali ya sasa imefanikiwa vipi kwa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii naweza kusema kwa 50% imefanikiwa kwa baadhi yake ila kwa 50% bado nina Deni nayo. Je, na Wewe kama Mdau na 'Great Thinker' unadhani ni 'Maendeleo' gani muhimu yamesahaulika katika Maeneo mbalimbali ya nchi ya Tanzania kuanzia Mjini na Vijijini?
Karibuni katika kutoa Michango yenu tafadhali.
Maendeleo hayaletwi na serikali wala mwanasiasa.
Ni kama refa kwenye mchezo wa mpira, yeye hafungi magoli.
Watanzania siyo maiti, mizoga wala mizigo ombaomba.
Wanapambana kila siku wanafanya kazi kujenga taifa lao.
Serikali iwe kama refa na isimamie vizuri michango yao ( kodi ) kwa ajili ya kuwawekea mazingira mazuri zaidi ya wao kuwajibika.
Iache kuwapora korosho, mkonge, ufuta, mbaazi, madini, misitu n.k
Wale vijana waliojihangaisha kutafuta vijikazi vya mikataba mifupi ili wapate mitaji wajiajiri wasidhulumiwe FAO LA KUJITOA. Wapewe pesa zao kama wao wanasiasa wanavyppeana kila mara baada ya miaka 5.
Jambo la msing kabisa iheshimu UHAI wa kila mtu, na siyo KUUA watu kiholela kwa ajili ya kuridhisha takataka mmoja ambaye naye atakufa tu.
Watanzania ni wachapakazi, wanachohitaji ni kutoporwa kwa kazi ya JASHO lao. Basi