Je, unadhani Upinzani Tanzania umebeba matumaini ya wananchi kwa kiasi gani?

Joined
Sep 13, 2023
Posts
35
Reaction score
46
Wanamudu na kustahimili uzito wa matumaini na matarajio ya wa Tanzania?

Wanathamini na kuheshimu thamani wanayopewa na wananchi?

Unaaminika kwa kiasi gani kubeba jukumu kubwa na zito la kuongoza nchi?

Nini kifanyike upinzani uwe na sura, sauti na uelekeo moja?

Hebu njoo taratibu na kwa ustaarabu kwenye mizania hii muhimu kwa mustakabali wa Mama Tanzania.
 
Utaamini vipi vyama ambavyo havina hata sera?

Watu wachaguwe makelele ya kubwabwaja na kuhororoja hovyo?
 
Upinzani sio watu ni Ideology, sasa endelea kuzania upinzania ni Mbowe au Lisu,
 
Hizo hesabu ni za ki-expansion joint
Lazima uwe umeiva kwenye Pure Mathematics Ten
Hasa kwenye ile mada ya central tendency kama haupo sawa hutoboi
 
Inawezekana ukiwapima wapinzani bado hawatoshi..lakini jiulize CCM imebeba mategemeo na matumaini ya nani?the alternative is much worse..hao wapinzani watajifunza kazini lkni ondoa CCM kwanza
 
0%

Mtanzania anahitaji kukombolewa kiuchumi, kahawa yake, chai yake, pamba yake, korosho yake, biashara yake, utaalam wake nk;

Mtanzania anahitaji kukombolewa kiafya, matibabu mazuri, huduma Bora za nafuu na uhakika na zinazofikika;

Mtanzania anahitaji huduma Bora za miundombinu, asafiri kwa uhakika, asafirishe Mali na mzao yake, apate soko;

Mtanzania anahitaji usalama wa mazingira na maisha yake na jamii yake n.k.

Vyama vya upinzani vinapaswa kuonesha ni vipi vitaleta improvement katika Mahitaji hayo muhimu ya Mtanzania. Hiki ndicho Watanzania wanahitaji kusikia.

Kinachofanyika kwenye mikutano Yao ni kujipambania wao tu, maslahi Yao na Haki zao kama viongozi. Wao wanaongozwa na mitandao na Wana mitandao ya kijamii. Mahitaji ya huko mitandaoni ni tofauti sana na Mahitaji ya Watanzania walio wengi.

Itoshe tuu kusema vyama vya upinzani vina safari ndefu sana isiyo na hakika na iliyojawa mashaka ya kuchukua Dola.
 
asante mwalimu DATAZ kwa darasa mujarabu
 
Back
Top Bottom