Mkuu ndai, haya ndio nayasikia kwako leo!. Kuna kitu kinaitwa historia ya kweli na kuna kitu kinaitwa hadithi, au simulizi za kale!, au mapokeo na kuna kitu kinaitwa uthibitisho wa kisayansi na kiteknolojia!. Naomba usichanganye simulizi na mapokeo ukayageuza ndio historia!.
Ninachokijua ambacho hata sayansi inakithibitisha, Visiwa vya Zanzibar vilikuwa ni sehemu ya bara miaka milioni nyuma!, vikamegeka na eneo la kati likasombwa na mmomonyoko!, hivyo kwa Tanzania kuishikilia Zanzibar, kuitawala kwa mlango wa nyuma na hata kuiadabisha ikibidi, ni kutimiza haki yetu on what is our rights!.
Wavamizi Waarabu walipokuja na kuvitwaa as if havina wenyewe, wakakulia, wakazaliana, wakalowea na sasa baadhi yao wameanza kujisahau kwa kudhania visiwa hivyo ni mali yao ilhali wao ni watu wa kuja tuu!.
Mapinduzi Matukufu ya 1964, vilirudisha heshima ya visiwa hiyo iliyoporwa na madhalimu wale na muungano ukavirudisha visiwa hivyo kwa wenyewe halisi.
Mapinduzi Daima!
Muungano Udumishwe!
Mungu ibariki Tanzania.
Pasco
Kweli kuna hadithi na simulizi zisizokuwa na ushahidi na hiyo inatoka na waafrika kutokuwa na utamaduni ya kuandika historia yetu lakini hadithi na simulizi nyengine huwa za kweli
Kutokana na waafrika kutokuwa na utamaduni wa kuandika mambo muhimu na yasio muhimu ndio yanatokea haya ya kutoamini chochote kinachosimuliwa na mwafrika,na ndio maana akina wanamapinduzi kama Maisara Suleiman akaigeuza historia na kuwambia wazanzibar kuwa warabu walikuwa wanawakata wazanzibar wajawazito wenye asili ya kiafrika matumbo ili waone mtoto kakaaje tumboni
Kwa upande wangu mtu yoyote anaesema mapinduzi ya zanzibar yameirejesha hadhi ya zanzibar namuona ana akili mgando,habari ya kueleza manufaa na kasoro za mapinduzi ya zanzibar ni ndefu sana lakini kwa ufupi mapinduzi ya zanzibar yameleta ubaguzi zanzibar yameirejesha zanzibar nyuma kimaendeleo, ........nk
Mfano kabla ya mapinduzi wazanzibar wenye asili yoyote akiwa mwarabu,muhindi aliweza kujiunga na polisi au jeshi kwa sasa hiyo haiwezekani..Kabla ya mapinduzi Zanzibar ilikuwa inauchumi mkubwa katika nchi za Afrika mashariki na kati,zanzibar ilkuwa na zao lake na uchumi(Karafuu,Nazi),ilkuwa na Dini yake (Islam),ilikuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa(demokrasi),ilikuwa na watu wake walikuwa (waswahili),mapinduzi yamepindua historia ya zanzibar na kuifanya zanzibar iwe nchi isiojijua....
Kabla ya mapinduzi Tulikuwa tunawaona wazanzibari wenye kila asili wakiuza vitu barabarani mfano washihiri(yemen) walikuwa wauzaji wakubwa wa kahawa barabarani,lakini tangu ujio wa mapinduzi wazanzibar wenye asili ya asia na mashariki ya kati(wahindi,warabu) ndio wamekuwa matajiri na wazanzibari wenye asili ya kiafrika ndio wamekuwa mafukara hali hii ilikuwa haipo, kabla ya mapinduzi kila mtu alikuwa na haki kama mzanzibari,wazanziabar wa asili zote walikuwa wanahaki ya kuitumikia zanzibar
Lakini sasa waafrika(wanamapinduzi) wamekamata serikali wamefanya wazanzibari wasio waafrika waingie kwenye biashara wakitaka wasitake,mapinduzi yameweka tabaka mbili kwa mzanzibar,matawala na mtawaliwa.
sasa sijui haya mapinduzi tutayatukuza kivipi
Tafakari