Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Najua wapo wengi ambao mmewahi kusikia kuhusu HUBS na Co working Space
Je, unafahamu ni nini?
Hubs au Co working space ni aina ya Ofisi za kufanyia shughuli zako ambayo inakuwezesha kufanya kazi zako katika mazingira tulivu na kupata huduma za ziada kama vile internet na pai fursa ya kufanya NETWORKING na chumba cha sehemu ya vikao.Vile vile maeneo haya huweza pia kutumika kama sehemu ya anuani ya kibiashara na yakuwezesha pia kuwa na huduma ya mapokezi,call forwarding n.k.Kimsingi ni sehemu ambayo inawezeshawatu kufanya shughuli za kibiashara kisasa na kwa uhakika.
Sio kila aina ya biashara inaweza kufanyika katika Co-Working Space lakini biashara na huduma kama za Wanasheria,Washauri waelekezi,Wahasibu,Watengenezaji wa mifumo ya Computer,Wataalamu wa masoko,Waandishi wa habari,Wakufunzi wa njia ya mtandao na watu wanaotoa huduma za aina hizo wanaweza kutumia mfumo huo.Mfumo huu unaweza pia kutumiwa na wamiliki wa viwanda vidogo ambavyo vipo majumbani kwao kutumia maeneo haya kama sehemu ya kiutwala na nyumbani kuwa sehemu ya uzalishaji.
Aina hizi za huduma zinapunguza gharama za uendeshaji na usimamizi na hivyo kukuwezesha kuwekeza muda na akili na fedha zako kwa ajili ya shuguli za msingi za kibiashara unazofanya.
Uzuri wa Hubs unaweza kuzitumia pale tu unapohitaji na sio kila siku au kila mara na hii inakuwezesha kusimamia biashara kwa gharama nafuu.
Je nani anaweza kuaqnzisha HUB?
Mtu yeyote anaweza kuanzisha HUB cha muhimu na awe na mtaji,eneo na utaalamu wa kusimamia uendeshaji wa HUB.Ili kuendesha HUB ni lazima uwe na uwezo wa kuwapa wajasiriamali na wafanyabiashra support na mazingira wezeshi ya kufanya shughuli zao.Eneo liwe sehemu inayofikika kirahisi na gharama zako ziwe rafiki kwa startup.
Karibuni tujadili zaidi kuhusu shemu za coworking unazozifahamu na fursa na changamoto zilizopo.