Je, Unafahamu Kukosea pia ni Makusudi ya Mungu? Fuatilia Kisa Hiki

Je, Unafahamu Kukosea pia ni Makusudi ya Mungu? Fuatilia Kisa Hiki

Pang Fung Mi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2022
Posts
6,653
Reaction score
13,919
Naamini nyote mwabuheri wa afya.
Siku moja iliwadia ya safari yangu ya kuelekea maeneo Minziro na Bus la Kampala Coach la Bukoba
Baada ya kufika ubungo nikakosea nikapanda Bus kampuni hio hio ila linaloishia Kampala Mijini pale Jinja Road mbele kidogo ya Makutano ya Kuelekea Port bell, ila kabla ya kufika City square.

Basi bwana basi la Bukoba likawahi kuondoka mapema tu saa12, la Kampala tukachelewa kuondoka. Tuliondoka kama saa 1:30 asubuhi. Muda huo huo ndio muda ambao hata Scandinavian Bus Marcopolo lilikuwa ndio time zake kuondoka.
Safari hio hadi Arusha, kufika Arusha kondokta akapigiwa simu kuna abiria kaachwa Chalinze, akahamaki mbona tulisimama Chalinze? Akaambiwa abiria alitoka alienda short call, basi akaanza kukagua seat za abiria , kufika seat no.23 akanikuta mimi akauliza Musaja akauliza Chichi Ssebo nikajibu Ndi kawaa Munange, nikauliza Okolachi buddy? Akasema seat sio yako nipe ticket nikampa kuisoma akacheka , nikasema aah Ssebo ndiwano chichi nawe!! Akasema mwanangu umekosea Bus wewe unaenda Bukoba na unashuka Minziro? nikajibu ndio akasema hii ticket ni bus lile jingine la kwanza la kwenda Bukoba, daah ikawa noma nikajibu kweli mi naenda maeneo ya Minziro baada ya Mutukula border.

Akasema usiwaze upo mpango wa Mungu. Akasalimia Tasipota nikajibu Ndi bhulunji Tasipota nawe?! Bus tukaendelea na safari.

Saa3:30 usiku tukafika Nairobi kama kawaida Nairobi haipumziki ni 24hrs kama Lusaka Zambia bus terminal.

Tukaanza safari kuondoka Nairobi kwenda Kampala kama saa5 ucku.

Chuma Issuzu inakamatia njia ya kupita Border ya Busia.(Baridi la Kericho sitasahau) Hapo nasikiliza nyimbo kadhaa za akina Jua Kali, Wirely, Nonini, Nameless, Nazizi, Ziggy Di, Raga Di, Bebe cool, Bobi wine, Juliana kanyomozi, Juma Nature, Prof J, Sam wa Ukweli, AY, Ssemakula, UB40, Madonna, GUnit, 50cent, Beanie Man etc

Mara pap tukafika Busia saa11 alfajiri, kama kawaida tukasibiri ifike saa12 raha kama zote nikala kuku chipwaa baada ya formalities za border.

Safari inaenda nikiwa Nina mawazo sana sana lakini roho nyepesi haina uzito wowote ule.

Ndani ya bus kumbe kuna abiria wanastaajbu nikaanza kuitwa mwanampotevu toka Nairobi, utani kama wote na wanna madent wa Mukono Christian University, Kyambogo, Makerere, KIU Kabalagalaa, na Nkumba University seat mate wangu ndani ya bus.

Sometimes nawaza nasema huu bila shaka ni God's plan, sometimes najiona fala sana, nakijipa hopes kati am no the first one to go astray najipa moyo.

Tulivofika Jinja wanna wa Mukono Christian University wakaanza kamanda wenzio wanakaribia kufika, nikaziba masikio kama kawa Nina headphones Kwa masikio, wakanistua Hoya endelea na juice hizi hapa acha mawazo wewe malaika hawabishiwi, nikajibu Amina Amina.

Naendelea kujiuliza maswali lakini roho iko kwatu kbsa. Najishangaa

Nikajipa moyo isiwe shoo ndio ishatokea, basi bhana tukafika Kampala city nikashuka, wana wanauliza sasa inakuwaje nikawajibu Kampala mimi home nimesoma Najja Schools na St.Marrys pia, Kwa hio hapa nimekubali wito wa Mungu, basi nikakumbuka kuna msela wangu mkenya anakaa Akamwesi Hostel mwana anasoma Electrical engineering Makerere, pap mwana kapokea, niaje Mtzi nikajibu poa niaje Overland Pirate? akacheka sana, hapo naelekea ATM pale Bank of Baroda, Benki Ina mataa ya madoido kuliko zote ikifika usiku enzi hizo lazima utaijua tu USP watu wa Economics tunaita hivo.

Akauliza hio nikajibu Niko Baroda hapa nachukua minoti ya Zimbabwe ya M7.

Nikamwambia njoo tukutane Chicken tonight nione Manzi tamutamu kwanza ndio twende Deep Blue, hio ni Wandegeya moja.

Bus tukapata msosi pale chicken tonight kisha tukahamia Deep Blue, mimi nilikuwa natumia pilsners larger tamu sana enzi hizo. Pirate anakunywa Nile larger safari larger ya waganda enzi hizo.

Back to the story nikampea story ya kachanganya bus msela wangu Pirate akacheka kwanza, akauliza niaje hio, nikajibu nadhani malaika wa east Africa kaamua, hivi unajua demu wako yule wa MUBS - Uliemuacha class moja anakutafuta sana anataka hata akuje akufuate TZ? Nikaduwaa nikauliza nani Maggie akajibu si ndio huyo.

Nikasema ebuu nipee namba hio, nikamcall Maggie wangu, alifurahi sana, so akakuja fasta pale Deep Blue mabusu kama yote yote,

Mungu akiamua hapangwingwi that was a day, this Manzi mkenya wa pwani mazee alinibamba na yeye akabambika kwangu.

Remember safari yangu ya Minziro haijafa, napaswa kuendelea the next day, Manzi akasema tena Leo ni Wednesday ni Ladies night Angenoir Club, I need a romantic setup with you ndio vile nafsi yake iweze shiba.

Nikamwambia sina pesa Bado sijapata kazi, akasema wewe wanijua acha hizo mimi ni wewe na wewe ni mimi Kampala ni ya Wakenya na watzed nakupenda sana.
So shortly after kupata bia tatu tatu tukashuka Akamwesi Hostel uzuri Manzi wangu nae alikuwa na chumba pale,

The next day nikaenda na demu wangu mkenya nyumbani Minziro.

Surprisingly mbele kidogo ya Masakaa si nikaona that very same bus ambayo ilikuwa nipande Jana imedoda kumbe the bus was in suspense by the immigration officers watu wamedoda pale wakikaguliwa, mimi huyoo na Manzi wangu nikamsimulia akasema all this is a product of my monthly prayers and my Godly wish to have you around me.

Hii story ni maudhui ya subra, ustahimilivu, kutojutia, kushukuru Kwa kila jambo, kuna mambo Mungu anapanga na sisi tunafanya ukaidi.

Kisa Hiki ni funzo kwenye mahusiano, mapenzi na ndoa ukiachwa sio kosa ni Rehema na Neema za Mungu ni kama umepitisha kwenye mapito kisha Mungu akamvua shetani nafsini, mwilini na rohoni.

Huwezi kuwa na shetani na roho mtakatifu Kwa wakati mmoja ndio kisa kama changu, kutopanda gari la Bukoba ni mpango wa Mungu kabisa na amefanya kuwa ilivyokuwa.

Ndio huyumchumba wangu mixer ya Mjikenda na Mkunya, pamoja nae amekuja na Neema na baraka za Mungu, imagine imagine real name yangu ya TikTok ndio imenikutanisha nae tena.

Tuamini Mungu yupo yupo na kila jaribu lina mlango wake.

Sisi sote tumebarikiwa mimi leo, wewe, yule, wale baraka pia zaja

The horizon hides heaven for each of us collectively or individually.

Blessings 💋🙏🙏
 
Back
Top Bottom