Je, unafahamu kuwa kufanya lamination ya nyaraka zako kunaweza kuharibu thamani yake ya kisheria?

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
968
Reaction score
1,978
Inaonekana maridadi. Inaonekana salama. Lakini pindi unapofanya lamination ya nyaraka halisi, kisheria unaweza kuonekana umeziathiri au kuzibadilisha bila kujua.

Watu wengi hulaminate vyeti, hati za kiapo, risiti na nyaraka nyingine wakidhani wanazihifadhi. Ukweli ni kwamba, unapozifunika kwa plastiki, unafunga mbali kila kipengele kinachothibitisha uhalisia wake.

Kwa sasa huwezi kuelewa hadi kutokee uhitaji wa kuthibitisha mahakamani kuhusiana na uhalisia au uhalali wa nyaraka husika.

Hebu tufanye uchambuzi kwa undani madhara yake:

---

■ Lamination hubadilisha kabisa asili ya nyaraka zako

Wino, sahihi na mihuri vinakwama chini ya plastiki. Huwezi tena kuhisi ubora wa karatasi, kupima nguvu ya muhuri, au kuchunguza uhalisia wa wino.
Hivyo, endapo nyaraka zitahitaji uthibitisho, hilo linakuwa tatizo.
Kwa kifupi, umebadilisha ushahidi wa kimwili unaothibitisha uhalisia wa nyaraka yako.

---

■ Nyaraka zilizofanyiwa lamination zinaweza kukataliwa

Mahakama, benki, balozi na hata taasisi za elimu zinaweza kukataa kupokea nyaraka zilizowekewa lamination kwa sababu hawawezi kuzipima, kuzichunguza, au kupiga mihuri mipya.

Fikiria umesafiri kwa ajili ya usaili au mahojiano ya viza kisha ukaambiwa:

“Samahani, hatukubali/hatupokei nyaraka zilizowekewa lamination.”
Kitendo kidogo cha kuzilinda kinaweza kuleta hasara kubwa.
---
■ Huwezi kupata Certified True Copy (CTC) kutoka kwenye nyaraka zilizowekewa lamination.

Mara tu unapolaminate, sehemu ya nyuma ya nyaraka—ambayo hutumika kwa muhuri au uthibitisho—haiwezi tena kutumika.
Hivyo, ukihitaji CTC, itakulazimu kutafuta original mpya kabisa kutoka chanzo kilichozitoa.
---
■ Mahakamani, nyaraka zilizowekewa lamination hupoteza uzito wa kiushahidi

Kwa sababu ya plastiki, haiwezekani kuthibitisha kama nyaraka zimebadilishwa au la. Utelezi wa karatasi, nguvu ya muhuri, na namna sahihi ilivyoandikwa—vyote vinapotea.
Matokeo yake, hata kama nyaraka ni halisi, sheria inaweza kuichukulia kwa mashaka makubwa.

---
Njia sahihi na salama za kulinda nyaraka zako

◆ Scan na kuhifadhi nakala laini (soft copies) kwenye email au cloud storage.
◆ Hifadhi nyaraka(original )kwenye jalada lisilopenya maji, mbali na unyevu na joto kali.
◆ Tumia transparent sleeves zinazoweza kutolewa wakati wowote bila kuharibu nyaraka.
◆ Tumia nakala za kawaida kwa matumizi ya kila siku; asili(original )ziwekwe sehemu salama.

---
Mwisho

Lamination inaweza kufanya nyaraka zionekane mpya na nadhifu,
lakini kimyakimya inaharibu uhalisia na hadhi yake ya kisheria.

Kwa hiyo kabla hujalaminate cheti chako, hati ya kiapo au hati ya mali, kumbuka:
Sheria inaheshimu uhalisia, si uzuri wa plastiki. Hii haina maana ukaondoe lamination, hapana. Utaharibu zaidi. Acha hivyo hivyo lakini kuanzia Sasa usiwe unawekea lamination vyeti vyako.

__________
The best way to learn is to learn from the best

© Venance S William
 
Uwe na cheti kinachotiliwa shaka,au usiweke lamination ukose kabisa hiko cheti.
 
Ungemalizia kwa kusema ni Tanzania tu, uzi ungekua na maana Sana

Wazee wakoloni wapo ofisin unadhan utawaza nn zaidi ya hayo
 
Acha kudanganya watu.Unajua karatasi inaoza sasa ikioza na kupoteza mahandishi
 
Kuna star mmoja alipatwa na mkasa akashitakiwa. Katika kujitetea ikabidi alete nyaraka zake ikiwemo cheti chake cha shule alichokiwekea lamination mahakama ikakikataa na kutaka cheti original
 
Inaonekana maridadi. Inaonekana salama. Lakini pindi unapofanya lamination ya nyaraka halisi, kisheria unaweza kuonekana umeziathiri au kuzibadilisha bila kujua.

Watu wengi hulaminate vyeti, hati za kiapo, risiti na nyaraka nyingine wakidhani wanazihifadhi. Ukweli ni kwamba, unapozifunika kwa plastiki, unafunga mbali kila kipengele kinachothibitisha uhalisia wake.

Kwa sasa huwezi kuelewa hadi kutokee uhitaji wa kuthibitisha mahakamani kuhusiana na uhalisia au uhalali wa nyaraka husika.

Hebu tufanye uchambuzi kwa undani madhara yake:

---

■ Lamination hubadilisha kabisa asili ya nyaraka zako

Wino, sahihi na mihuri vinakwama chini ya plastiki. Huwezi tena kuhisi ubora wa karatasi, kupima nguvu ya muhuri, au kuchunguza uhalisia wa wino.
Hivyo, endapo nyaraka zitahitaji uthibitisho, hilo linakuwa tatizo.
Kwa kifupi, umebadilisha ushahidi wa kimwili unaothibitisha uhalisia wa nyaraka yako.

---

■ Nyaraka zilizofanyiwa lamination zinaweza kukataliwa

Mahakama, benki, balozi na hata taasisi za elimu zinaweza kukataa kupokea nyaraka zilizowekewa lamination kwa sababu hawawezi kuzipima, kuzichunguza, au kupiga mihuri mipya.

Fikiria umesafiri kwa ajili ya usaili au mahojiano ya viza kisha ukaambiwa:

“Samahani, hatukubali/hatupokei nyaraka zilizowekewa lamination.”
Kitendo kidogo cha kuzilinda kinaweza kuleta hasara kubwa.
---
■ Huwezi kupata Certified True Copy (CTC) kutoka kwenye nyaraka zilizowekewa lamination.

Mara tu unapolaminate, sehemu ya nyuma ya nyaraka—ambayo hutumika kwa muhuri au uthibitisho—haiwezi tena kutumika.
Hivyo, ukihitaji CTC, itakulazimu kutafuta original mpya kabisa kutoka chanzo kilichozitoa.
---
■ Mahakamani, nyaraka zilizowekewa lamination hupoteza uzito wa kiushahidi

Kwa sababu ya plastiki, haiwezekani kuthibitisha kama nyaraka zimebadilishwa au la. Utelezi wa karatasi, nguvu ya muhuri, na namna sahihi ilivyoandikwa—vyote vinapotea.
Matokeo yake, hata kama nyaraka ni halisi, sheria inaweza kuichukulia kwa mashaka makubwa.

---
Njia sahihi na salama za kulinda nyaraka zako

◆ Scan na kuhifadhi nakala laini (soft copies) kwenye email au cloud storage.
◆ Hifadhi nyaraka(original )kwenye jalada lisilopenya maji, mbali na unyevu na joto kali.
◆ Tumia transparent sleeves zinazoweza kutolewa wakati wowote bila kuharibu nyaraka.
◆ Tumia nakala za kawaida kwa matumizi ya kila siku; asili(original )ziwekwe sehemu salama.

---
Mwisho

Lamination inaweza kufanya nyaraka zionekane mpya na nadhifu,
lakini kimyakimya inaharibu uhalisia na hadhi yake ya kisheria.

Kwa hiyo kabla hujalaminate cheti chako, hati ya kiapo au hati ya mali, kumbuka:
Sheria inaheshimu uhalisia, si uzuri wa plastiki. Hii haina maana ukaondoe lamination, hapana. Utaharibu zaidi. Acha hivyo hivyo lakini kuanzia Sasa usiwe unawekea lamination vyeti vyako.

__________
The best way to learn is to learn from the best

© Venance S William
Haya yameanza lini? I laminated my certificate since 90's lakini siajwahi kuulizwa huu ujinga! Kwani unapotoa photocopy na kutaka wakili athibitishe anataka original iwe ya karatasi? Wacha hizo mwamba! Vyuo vya Ulaya wenyewe wanakuletea kabisa chetu ambacho kiko laminated sasa unataka kusema wao ni wajinga?
 
Bila kuweka lamination mbna karatasi ya cheti, itaharibika.
Lol
 
Back
Top Bottom