Je, unafahamu kwanini maisha yako yameandamwa na mikosi pamoja na Mambo mabaya?

Je, unafahamu kwanini maisha yako yameandamwa na mikosi pamoja na Mambo mabaya?

What do this mean?
1608664001824.png
 
Mimi ni nani?
Hapo ulipo anza kujiuliza maswali haya na ujijibu mwenyewe,
Je hivi nilivyo ndivyo natakiwa niwe? Yaani ukijiangalia tabia zako, matendo yako ndivyo unatakiwa uwe? Jibu unalo.

Watu wanasema mimi ni nani?
Ulishwahi kuona mtu Fulani akitaka kumchumbia binti Fulani anaanza kwanza kuulizia kwa watu wanaomfahamu kama vile majirani, mrafiki ni kwasababu watu wa pembeni wanakufahamu zaidi, je leo hii wewe memba mwenzangu wa jf mtu akiuyliza jirani zako kua wewe ni nani atajibu vipi? Je unatabia nzuri, unatabia mbaya, mpole, una hekima, mwizi n.k. jibu unalo mwenyewe.
 
ukiona watu unawahutubia muda mrefu halafu wanaanza kupiga makofi mengi ujue wamekuchoka inatakiwa uondoke jukwaani
 
Nzuri Sana. Mimi nataka maisha yangu yajae furaha, huwa najipaka mafuta ya alizeti.🌻na pia hua nakaa jirani na waridi ili ninukie 🌹
Watu wanaokuzunguka Wana mchango mkubwa Sana kwenye maisha yako, eidha ya mikosi au ya baraka.
Lakini katikati ya watu wenye mikosi, nuksi na mabalaa, unaweza kuamua usiwe sehemu ya maisha Yale.
Unaweza kutokea kwenye familia fukara Sana na ukaamua ule ufukara usikufuate wewe Wala wanao.
Jitenge na Kila laana ya hao watu.
Kuna watu wanajisifia magonjwa, huu ni ugonjwa wangu. Utaponaje iwapo umeshajimilikisha?
Mwanzo 12:1
BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonesha
Hakuna mtu anayeitwa Abramu kwenye maandiko yeyote
 
harakati za siri huu uzi hope hujawah kuusoma. Upo jukwaa la dini

Je wafahamu kua kama ukisafiri ukarudi miaka ya nyuma (Time Traveling) hadi kipindi Wale mitume 12 wa Yesu bado wapo ukamwambia Petro nionyeshe JESUS CHRIST, Petro atashangaa Kisha atakuuliza JESUS ni nani? Unajua kwanini? Fuatana nami mwandishi wako Davinci nikujuze Jinsi jina YEHOSHUA lilivyobadilika kua Jesus.

Wakati malaika Gabriel alipomtokea Bikra Maria kamwambia kua atazaa mtoto na jina analotakiwa ampe mtoto, (Luke 1:31) Jina alilosikia maria kutoka kwenye lips za Gabliel lilikua linafanana, kama sio lenyewe kabisa Yehoshua ambalo linatamkwa Yeh-ho-shoo'-ah. Katikalugha ya Kiebrania cha kisasa jina "Yehoshua" inaandikwa
53ac5e922b8f171b29abaad82c96c76b.jpg

na inasomwa kutoka kulia kwenda kushoto. Jina hilo limeunganisha maneno mawili ya kiebrania. Neno la kwanza ni, "Yeh-ho", ambayo ni sehemu ya Jina la MUNGU ambalo muda mwingine linatumiwa mwanzo au mwisho wa majina ya kiebrania.Sehemu ya pili mabayo ni "shua", ni jina la kiebrania linalomaanisha OKOA hivyo jina "Yehoshua" lamaanisha kua MUNGU ANAOKOA. Jina Yehoshua liliendelea kufupishwa kutokana na matumizi ya kila siku ndivyo kama ilivyotokea kwa jina Barbara ambalo hufupishwa na kua Barb . Hivyom jina la Yehoshua lilifupishwa na kuwa Yeshua.
a7e2b600dc5bf27cc662f55c7c314c0b.jpg





Tafsiri.... Kiebrania kwenda Kigiriki
Mapema, Wakati injili inaandikwa habari ya Yeshua Masiah ilianza kuenezwa kwa watu wa mataifa na habari zake zikawa zinatafsiriwa kwenda kwenye lugha ya Kigiriki kutoka Kiebrania.Sasa ipo hivi kuna njia mbili ambapo jina la Kiebrania laweza tafsiriwa kutokana na changamoto ya lugha, siku zote jina la kiebrania hua limebeba maana hivyo njia ya kwanza ni kutafsiri jina kutokana na maana yake pia njia ya pili ambayo hua inatumiwa sana inaitwa transliteration, Ambapo ni kutafsiri jina kutokana na sauti ya jina linavyotamkwa, hivyo kama watafsiri wa Habari za injili walitafsiri jina Yeshua kutokana na historia basi tatafahamu kua maana yake ni MUNGU AOKOA kwani hivyo ndivyo inavyomaanisha
Kwa kesi ya jina la "Yeshua", ulimwengu wa watu wanao ongea kigiriki waritafsiri vizuri jina lake, hii inahusisha mchakato rahisi wa kuchanganya sauti za herufi ili msomaji atakapo maliza kusoma amalizie na sauti ile aliyoanza nayo wakati anaanza kusoma. Hili sio tatizo ila kwenye jina la Yeshua kuna matatizo manne kuleta katika Kigiriki. Mawili yalikua ni kwamba lugha ya kigiriki cha zamani haikua inajumuisha sauti mbili ambazo zilikua zinapatikana kwenye jina Yeshua. Hii ni ajabu kwa watu wanaongea kingereza ila ukweli ni kwamba lugha ya kigiriki cha zamani haikua na sauti "Y" kama kwenye neno YES pia haikuwa na sauti ya "Sh" kama kwenye neno SHOW
Sauti ya karibu zaidi ya mtu anayezungumza Kigiriki inaweza kuja kufanya sauti ya Y kwa kutumia herufi mbili za kigiriki ambazo ni Iota na Eta pamoja ambapo itatokea sauti ya "ee-ay", pia mtu anayezungumza kigiriki anaweza kutengeneza sauti ya sh kwa kutumia herufi sigma . Kwa mabadiliko hayo mawili jina la "Yeshua" lilitamkwa na wagiriki "ee-ay-soo-ah".
Tatizo la tatu katika kutafsri jina yoshua ni kua kiasili majina ya kiume ya kigiriki hayaishii na irabu, majina yote yaliyoishia na irabu yaliongezewa herufi sigma (S) kama kiambishi tamati chake. Hii ilitokana na sababu kua Mungu wa wagiriki Zeus jina lake linaishia na S, ndio maana hata majina ya wahusika kwenye biblia yalikua yanaishia na S. mfano Judah ilibadirika kua Judas, Cephah (ikimaanisha mwamba") ilibadirika kua Cephas, Apollo ilibadirika kua Apollo, Barnabie ilibadirika kua Barnabas, Matthew ilibadirika kua Matthias nk nk.
Hivyo basi "ee-ay-soo-ah" ilibadirika na kua "ee-ay-soo-ah-s". Tatizo la nne ni kwamba sauti za irabu mbili kabla ya s haipom wala haijawahi kuonekana kwenye mtiririko wa lugha ya kigiriki, hivyo ili kureta mtiririko unaoeleweka hivyo waliziondoa hizo irabu jina likawa "ee-ay-soos". Mbali na kuliongezea jina s ili liwe limekaa kiume hii ilifanya wagiriki kuweza kulitafsiri jina la Yeshua. Kwa hatua hii, jina Yeshua lilipoteza maana yake na 75% ya sauti yake. Kizuizi cha mwisho cha sauti hiyo kilipatikana katika "oo" (kama kwenye "soon"). Yeshua kwa watu wanaongea kigiriki ilifahamika kama "ee-ay-soos" kwa muda wa takribani miaka 400 "ee-ay-soos" inaonekana hivi katika lugha ya kigiriki
bb1b7446c1b133385c3e90a0a7f468fc.jpg

, ni kama kingereza unasoma kutoka kushoto kwenda kulia


Tuendelee na tafsiri...Kutoka kigiriki kwenda kilatini
Mnamo miaka ya 400 A.D. kilatini kilikua ndio lugha ya inayotumika kwenye dini ya Ukristo na matoleo ya Kigiriki ya Agano Jipya yalitafsiriwa Kilatini. Biblia ya kilatini au Vulgate kama ilivyokua inaitwa , pia ilitafsiri kile kilichobaki cha jina la Kigiriki la Yeshua kwa kuleta sauti sawa ya "ee-ay-soos". Hii ilikuwa rahisi, kwa sababu sauti zote za kigiriki kwenye jina hili yalitamkwa hivyo hivyo kwenye kilatini. Herufi za kilatini ni tofauti na kigiriki lakini kwa kiasi Fulani zinafanana na kingereza. Hivyo basi tafsri mpya ya jina la kigiriki "ee-ay-soos" ilianza kuandikwa
0689cc7f9a0874aef8ae03b3b2ab4fa1.jpg

kwa kilatini na jinsi inavyotamkwa ilikua inafanana na wagiriki wanavyotamka, jina la Yeshua lilitamkwa hivyo kwa kilatini na wakristo karibia miaka 1000


Tafsiri ya mwisho.... Kilatini kwenda Kingereza
Wakati huo lugha ya kingereza ikiwa inaendelea kukua kabla ya karne ya 12 herufi J haikuwepo katika lugha ya kingereza , Sauti ya herufi J haikuwepo kwenye lugha ya Kiebrania,kigiriki,Kiaramu,wala kilatini. Hii inaonyesha kua hakuna mtu kipindi hicho alitamka jina la Yeshua kwa lugha ya kingereza Jesus.
Mnamo mwanzoni mwa karne ya 12 herufi J ilianza kutumika katika lugha ya kkingereza cha kati. Kuanza kutumika kwa herufi J.kwenye lugha ya kingereza kulipelekea herufi kama Y na I baadhi ya maneno nafasi yake kuchukuliwa na herufi J, Hii ilitumika san kwa majina ya kiume yanayoanza na herufi Y au I kwakua waliona sauti ya herufi J ilikua imekaa kiume zaidi, hapa ndipo baadhi ya majina yalibadilishwa mfano Iames ilibadirika kua "James", Yohan ilibadilika kua "John", na mengineo.
Mnamo waka 1384 John Wycliffe alitafsiri agano jipya kutoka kilatini kwenda Kingereza kwa mara ya kwanza na chanzo chake kikuu ilikua Biblia ya kilatini ( Vulgate). Wycliffe aliendelea kutyumia lugha ya kilatini na matamshi ya jina la Iesus. Kipindi hicho vyombo vya uchapaji vilikua havijagunduliwa, nakala chache tu za biblia alizoandika kwa mkono Wycleaf ndizo zilizalishwa.

Miaka 1450 Gutenburg aligundua Chombo cha uchapaji , kasha mwaka 1526 William Tyndale alitafsiri Agano jipya kutoka biblia ya kilatini kwenda kingereza akiwa na msaada wa maandiko ya kigiriki cha zamani. Tyndale alitaka biblia itafsiriwe kwenda kwenye lugha ya watu wengi na nakala nyingi za tafsiri yake zilichapishwa kwa msaada wa mashine ya kuchapisha. Tyndale alikua mtu wa kwanza kutumia herufi J kwenye jina la
27eed6fab8c346ed24d225ff7f53c189.jpg

. Utamkaji huu mya wa jina la yesu ulisambaa baadae jina la jesus likawa linatamkwa "Jee-zuz".Karne ya 17 herufi J iliingizwa rasmi kwenye kamusi .

Mwaka 1611 Biblia ya King James ilirahisisha baadhi ya majina katika kuyatamka kama tunavyolitamka jina la Jesus leo hii, kila jina katika biblia linaloanza na herufi J lilikuja kwa njia hii. Majijna kama Jeremiah, Jerusalem, Jew, Judah, John na kadhalika
Pamoja na utamkaji huu rasmi wa jina "Jee-zuz", sauti ya mwisho iliyobakia kwenye jina la Yeshua", (sauti ya oo kama kwenye neno "soon"), ilitoweka. Si sauti walamaana iliyobakia inatumbulisha jina la Yeshua. Lakini itambulike pia kua neno "Christ" sio jina bali ni cheo. Ilitokana na tafsiri ya kigiriki ya cheo kinachoitwa Messiah ikimaanisha mpakwa mafuta ". Hivyo hayo yote yaliacha utamkaji wa jina Yeshua the Messiah isambapo inatafsiriwa na kutamkwa kwa lugha ya kingereza na "Jee-zuz Chr-i-st".
Hivi ndivyo jina la Jesus lilivyopatikana kutoka kwenye jina Yeshua.. Ikumbukwe kua jina la Yeshua limeishi karibia miaka 1500 duniani huku jina la Jesus likiwa limetokea miaka kama 300 iliyopita.

Maoni ya mwandishi
Upande wangu naona sisi watanzania na Kiswahili chetu tunatamka vizuri jina la yesu sawasawa na waebrani, lakini haijalishi jina lake masia ni lipi aitwe Juma, Diamond, Hasani,Raymond, Magufuli, Gudume, Nkuruziza, Da'Vinci, Muhamad nakadharika cha muhimu ni ule wokovu wa uzima wa milele aliotuletea wanadamua hapa duniani.
Tchao..
Writtten and Prepared by
DaVinci..
JF Expert Member
 
SALUTE

Maisha ni safari ndefu yenye mabonde na mashimo tu Yenye matumaini tu huku raha zikiwa chache mateso na taabu yamejaa! Kuna mambo yanaweza au yanatokea kwenye maisha yako hadi ukabaki unashanga. Yaani jambo fulani baya au zuri linakufata wewe tu kila siku hadi unajiuliza Why me?

Mfano uko mtaani kila tukio baya likitokea basi unahusishwa, unaweza kuta yaani wewe kila mwanaume anayekufata ni ni wa aina fulani usiyoipenda, labda mwizi, muhuni, mweusi, mfupi, mjinga nk.

Kwa upande wa wanaume nadhani hii inawatokea sana utasikia kabisa mtu anasema "Aisee mimi nina bahati na wanawake weupe/walimu/manesi/wanawake washamba nk nk. Yote haya ni maisha yetu ya kila siku ya sisi wanadamu, wengi hatuelewi kwanini hii inatokea hivi lakini ni vitu ambavyo vinahusiana na mambo ya kiroha na Kiasili (nature).

Lakini hadi mtu yanamtokea mambo haya bila yeye mwenyewe kujua hua nini kinafanyika? Hapa nitaenda kuelezea zaidi jinsi mambo mabaya yanavyokua yanaambatana nasi pasipo sie kupenda. Ili nieleweke vizuri nitatumia terminologies za kwenye mambo ya teknoloji.

Kwenye Computer Processors kuna kitu kinaitwa Caches, hii ni sehemu ambapo ukifinya kitu fulani kwenye computer basi kile kitu kinahifadhiwa huko ndani ili ukitaka kukitumia tena basi kinafanyiwa kazi kwa haraka zaidi. Pia kuna kitu kingine kinaitwa HTTP Cookie hizi zinafahamika pia kama Web cookie, browser cookie, internet cookie. Hizi ni data ndogondogo ambazo huchukuliwa kwenye web, internet, browser n.k na kuhifadhiwa kwenye Computer wakati mtumiaji yuko anaperuzi. Kazi yake ni kurekodi mambo yote ambayo mtumiaji (user) anayafanya kwenye internet mfano. Zinarekodi Password, page ipi umetembelea, Majina, nk. Hayo yote yanakusaidia wewe mtumiaji wa internet utakapotaka kuperuzi mitandaoni basi iwe rahisi kutumia.

Kwa upande wa Google huko wao wana project yao wanaita Hummingbird, hii ni alogarithm ambayo inafanya kazi ya kumwezesha mtumiaji wa huduma za google (Hasa YouTube na Google as Search engine) kupata huduma hizo kwa urahisi na kwa haraka...wanasema Google inakujua kuliko mama yako mzazi, Ni kweli.

Unapotafuta kitu Google chochote Hummingbird inarekodi kila kitu baadae ukitaka kuitumia tena inakuletea vitu kama vile ulivyotafuta mwanzo. Ndio maana ukitafuta kitu fulani YouTube ukaangalia ukamaliza labda ukatoka huko baadae ukirudi tena youtube utakuta video mbalimbali zinazoshabihiana na zile ulizoangalia mwanzo.

Yes kwakua Google wanakua washajua ni vitu gani unapendelea ili usisumbuke kuandika wanakuletea hapo kwenye homepage as suggestion posts.

Sasa turudi kwenye mada kuu, mada yetu inahusu kwanini mambo fulani (upande wa ubaya) yanaweza kua yanakufata wewe tu!. Kwenye moja ya post zangu zilizopita nilieleza kua Roho ya binaadamu ndio inabeba taarifa ya kila kitu kukuhusu wewe, so nikachukulia kwamba Roho ya binaadamu ni kama BIOS CHIP (ROM) iliyopo kwenye Motherboard ya Computer halafu mwili wetu ni kama kasha la nje la Computer. Unapokufa Mungu anachomoa Bios chip tu iliyo na taarifa zako!

Leo twende tofati kidogo, tuchukulie Roho ni HummingBird au Cookie au Cache japo mimi nitapendelea tuichukulie kama HummingBird. Roho (Soul) imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Mind, Intellect na Impression. Mind ndio inahusika kwenye kufikiria, hasa kwenye kutambua lipi baya na lipi zuri. Kwenye Mind kuna kitu kinaitwa Subconcious Mind hii ndio sehemu kuu ya Roho (Soul) ambayo kazi yake ni kurekodi shughuli zetu za kila siku ziwe za kimwili au kiroho.

Sasa kwenye maisha halisi ipo hivi, unapofanya kitu fulani roho(subconcious mind) yako inarekodi. Labda siku moja uliwahi kuwa na mahusiano/ Kutongozwa/za na mwanaume au mwanamke ambao kwako wewe ambae wewe unaona hakufai, roho yako inahifadhi taarifa kwamba uko interested na watu wa namna hiyo. Au siku moja imetokea umeiba kitu roho itahifadhi taarifa. Siku umeenda jela basi roho itasevu. siku ukitembea na mtu aliekuzidi umri roho itahifadhi nk. Kwa upande wa Psychology roho tunasema kwamba Roho (Subconcious mind) inafanya kazi kwa ukaribu zaidi au inashirikiana katika kutenda kazi na Nature.

Kwa hiyo sasa unapofanya kitu fulani roho yako ikakihifadhi, baadae Roho itawasiliana na Nature kwamba unapenda vitu fulani hivyo nature itakua inakuletea vitu hivyo mara kwa mara. Hiki kitendo nature kuwasiliana na roho kisha kukuletea yale usiyoyapenda ndio tunaita MKOSI.

Mfano: Mbaba aliyekuzidi umri kakutongoza wewe kwa kua unashida zako ukamkubalia roho inahifadhi. Baadae itawasiliana na nature kua fulani anapenda wanaume wa umri fulani kisha nature itakuletea mwingine kama suggestion. ukikubali tena na tena basi ndio itakua tabia yako kabisa. Hii ipo kwa kila kitu iwe kibaya au kizuri.

Je, tufanyaje ili kuepuka mambo mabaya yanayotuandama?

Kwenye Computer ili kuziepuka cookies baada ya kutumaliza kuperuza mitandaoni inatakiwa uende upande wa setting kisha chagua Clear Cookies ili kuondoa kumbukumbu zote zote za kuperuzi siku hiyo. Kwa upande wa Google kubaki na taarifa zako. Huwa tunashauri kutumia Search Engine ya Duck Duck Go, Hii web ni nzuri zaidi maana hua ina clear taarifa zako zote baada ya kumaliza kuitumia..ina mengi mazuri ya kiusalama hasa kwenye taarifa za utumiaji wa kila siku (Browsing History). Jamani siipigii debe hii web, ni kuwaweka sawa tu na mada yetu hii. Sasa kuclear cookies au kuondoa mikosi kwenye maisha kuna mambo kadha ambayo tutayafanya.

Hivi ulishawahi kujiuliza kwanini mtu akitoka jela au mahabusu (kituoni) zile nguo alizoenda nazo huwa zinatupwa, pia itabidi aoge kabisa kabla hajaingia ndani, wengine huenda mbali zaidi kwa kuogeshwa dawa za mitishamba ili kuondoa mikosi. Hapo sasa ndio kitendo cha kuclearcookies. Wanafuta taarifa zote zilizomo kwenye roho zihusuzo jela. ni mfano tu huu ila hizi hapa chini ni njia zangu amabazo mimi kwa ufahamu wangu nadhani tukizitumia tutaweza kuondoa mshikamano wa mambo mabaya kwenye maisha yetu (Mikosi)
  • Kujua Preferences zako
Ili kuondoa kushikamana na mambo mabaya maishani inabidi mtu ujitambue wewe binafsi unapenda nini hasa. Je unapenda Kuwa mwema? Unapenda kuiba?unapenda mwanamke wa namna fulani?unapenda mwanaume wa aina fulani nk nk.. ukishajua ukipendacho basi futa yale uyapendayo nawe yatakua yanashikamana nawe.

Hatima yako ipo mikononi mwako, usiache Nature ikuchagulie Hatima yako kwa vitu ambavyo hupendi. Hivyo basi tukisha tambua yale tunayoyapenda na kuayafuata tutaifanya nature ituletee yale pia mabayo tunayapenda.Hapo tutakua tumekwepa kufuatwa na mabaya.
  • Kujiondoa kwenye mikosi. (Kuclear Cookies maishani)
Jamani maishani huwezi kua smart muda wote Nature always win!!!, ipo siku utanasa tu. Sasa hapa labda tuseme umeshavuruga mambo maisha yamejaa mikosi na mabaya yanakuandama. Hapa sasa tutaangalia jinsi ya kuondoa hayo mambo.

1. Tutumie Chumvi na maji, Usishangae sio uganga wala uchawi. Chumvi ni dawa nzuri sana kwa binaadamu nadhani member wengi wameielezea sana humu, sina haja ya kueleza zaidi. Cha msingi chukua chumvi ile ghafi ambayo haijapita kiwandani changanya na maji kisha nuia unavyotaka kisha oga. Hata nabii Ezra aliambiwa na Mungu achanganye maji naNchumvi kisha kuwapatia wana wa Israel wajitakase, ndio maana kwetu RC kuna maji ya baraka yenye Chumvi.

Kama utakua karibu na bahari itapendeza kabisa wewe ni kwenda na kujitupa tu majini maana huko chumvi kibao

2. Mshirikishe Mungu unayemuamini hata kama ni mzimu, hapo inabidi uombe toba kabisa, mweleze mapungufu yako na mahitaji yako kua unataka kuwa mtu mpya, mambo mabaya hutaki kushirikiana nayo. Piga sala sana na ibada kadri uwezavyo. Almighty atakuelewa na kukusafisha uwe mpya.

Maisha bana is all about determing yourself akina mshana jr na wenzake, manabii na mashehe Sharifu wanatuibia tu kwa kuwa wanajua elimu tunayo kidogo, hatujitambui. Tujifunzeni kujitambua hatutasubiria kuombewa na nabii. Wao wanacheza na Psychology ambapo huko watu wengi ni watupu sa tunapigwa tuuu!!!

NOTE. Ahsante Mungu kwa yote uliyonijalia hasi umeniwezesha kuandika mada hii.
End....

Kama umepende Like, Comment then share kwa wenzio.

~Da'Vinci
el maestro.

Uzi huu ndio nausoma leo na nimeuelewa, labda ni kwa sababu ya uelewa wangu mzuri kuhusu nadharia za computer na internet uliohusisha. Kilichobaki unclear ni maji ya chumvi kuondoa mikosi, naomba nieleweshe mechanism ipoje hapo?
 
Back
Top Bottom