Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 35,812
- 107,628
- Thread starter
- #461
DeliveranceNakupinga sana kwa jambo moja tu, hapo ulipoagiza watu wanuie kwa kutumia chumvi na kuogea ili kuondoa nuksi. Kwa kuwa wewe ni mkristo ngoja nikuthibitishie nakupinga kwa kutumia maandiko katika Biblia.
Kwa sababu nyakati hizi zimebadilika, na sheria ya maongozi ya Mungu yamebadilika. How?
Tangu kuwepo kwa mwanadamu katika uso wa dunia mpaka sasa, Mungu ameiongoza dunia kwa nyakati tatu tofauti.
1. Kaiongoza Yeye mwenyewe kipindi cha Agano la kale kwa Torati na sheria.
2. Kaiongoza kupitia Yesu Kristo kwa miaka 33 Yesu alipokuwa duniani.
3. Anaiongoza kupitia Roho Mtakatifu hata sasa.
Kwanini nakupinga?
Nyakati za Yesu na Roho Mtakatifu tunaendeshwa na sheria ngumu kuliko ya Musa, nyakati za Musa, ukizini ukikamatwa ndipo unahesabiwa dhambi, usipokamatwa huna dhambi. Nyakati hizi ukimtizama tu mwanamke au mwanaume kwa kumtamani tu, umekwisha kuzini naye moyoni, na unahesabiwa dhambi.
Nyakati za kale, ili utubu dhambi zako lazima ufanye tendo, uchinge ng'ombe au mbuzi kadhaa mwenye(wenye) sifa flani kulingana na dhambi unayoitubia. Nyakati hizi hatuchinji tena kwa sababu yuko aliyechinjwa(Yesu Kristo). Hivyo kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Siku hizi tunatumia kafara la damu ya Yesu na tunahesabiwa haki.
Yohana 1:16 - 17
"Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.
Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo."
Kutumia chumvi au tendo lolote la kiimani sio nyakati zake hizi. Kuna watu hadi wanatumia fruto wanaifananisha na damu ya Yesu, hadi ukienda maduka ya wahindi wanadhihaki wanauliza hununui damu ya Yesu? Ni dhambi mbele ya Mungu kugeuza utukufu wake na kufananisha na vitu vilivyotengenezwa na mwanadamu.
Mwisho kabisa badala ya kufanya matendo hayo ya kiimani ya kuondoa nuksi, tuongozwe na neno la Mungu tu.
"Neno la Mungu ni mamlaka ya juu na ya mwisho kabisa kwa mkristo".
Sasa kuna wakati wewe mzaliwa wa kwanza unaweza kua umeyafanya mambo mawili niliyoainisha hapo juu au hukuwahi kufanya kabisa maishani mwako na maisha yako yamekua totally miserable huoni pa kutokea maisha yako yamejaa giza ila unatamani kutoka huko ulipo utembee katika njia ya kusudi lako, Fear not God got you coverd!
Mwalimu Mkuu/lecture (Yesu Kristo) ni mzaliwa wa kwanza katika familia ya BWwana Joseph na Bibi Mariamu, yeye ndio kiongozi wa wazaliwa wa kwanza wote hapa duniani. Anajua kamba Yule mwovu anawatafuta kwa kila hali ili msiweze ku-pursue kusudi lenu, baada ya kumaliza mkataba wake wa kufundisha hapa Darasani(Duniani) akaondoka zake kwenda kuandaa mataji na vyeti (kupaa mbinguni) kwa wote ambao watakaofaulu masomo yake alijua kabisa hawa wanafunzi wangu wanakumbukumbu hafifu na wakiona mwalimu hayupo hawajisomei tena (kuishi katika maagizo ya Kristo) wanabaki kupiga fujo darasani. Hivyo alipofika huko alipoenda alimtuma Tutorial Assistance wake (Roho mtakatifu) aje kutukumbusha na kutufundisha maagizo ya Kristo kwa wale ambao tulikuja muhula ambao kristo hayupo.
Tutorial Assistance alitufundisha kitu kipya kwa sisi tulioingia muhula mpya mwalimu mkuu akiwa hayupo, Alitufundisha kitu kinaitwa deliverance kwa Kiswahili rahisi ni kupokelewa Upya. Wewe mzaliwa wa kwanza Ukishafika ile sehemu tunaita the point of no Return maisha yako yamejaa taabu na mahangaiko Yesu kristo kupitia roho mtakatifu anatoa huduma hiyo ya kuwapokea upya wale wote ambao wamepote maana yeye ni mchungaji mwema kondoo wake mmoja akipotea atahakikisha anamtafuta na kumrudisha kundini…Hivyo Yesu kristo kupitia Roho mtakatifu amewaagiza watumishi wake kuwa na siku maalumu au vituo mbalimbali vya kupokea wale wote waliopotea. Ukienda hapo wataformat Had Disk Drive yako (roho) na kufuta cockies na caches (roho za giza) zote zisiweze kukufuata tana.