Je, unafahamu kwanini maisha yako yameandamwa na mikosi pamoja na Mambo mabaya?

Je, unafahamu kwanini maisha yako yameandamwa na mikosi pamoja na Mambo mabaya?

Mkuu pole sana kwa hilo..
Tatizo ni kwamba mada zangu nyingi hua naandika kwa mfumo wa sequel.. mada hii ili uelewe vizuri inabidi usome nyuzi zangu kadhaa za miaka ya nyuma. Maana huko tunaaanza na kujiuliza mimi ni nani??? Ukishajua ndio unanmsoma yule uliyemjua sasa.

Je wewe mkuu Unadhani wewe ni huo mwili????maana utaupoteza soon tu utakapokufa. Je nawe utakua umepotea?? Mwenyewe si unasikia wanaita kwamba huu ni "Mwili wa fulani" kwenye misiba je fulani mwenyewe yupo wapi??? Ndio utagundua kua huo ni mwili tu wa vildamir putina ila putina mwenyewe yupo sehemu. Sasa hapa tunadeal na huyo V Putina sio mwili wake.

Kweye kuuconvice mwili kua unaweza kutembea wakati mtu huyo ameparalaizi inakua hivi...
Kama mtu kapalalaizi akiwa anatibiwa daktari nazipangilia upya neva zilizoharibika kwa madawa na upasuaji..hapo Cell zitauponyesa mwili huo uliopalalaizi mwili huo, hapo Cell zinakua zimeprogramiwa/Programmed na Daktar kujirudisha kama ilivyokua mwanzo ili mtu apone..kitendo hicho kinaitwa Cellular regeneration.

Sasa mkuu kila kitu kinaanza rohoni as a power house ya mwili...Mara nyingi tunavyotibiwa hospital tunatibiwa kutokea nje (mwilini) sio kutokea ndani ya Roho. So hivyo basi ukitaka kujitibu kupitia rohoni kama hivyo mtu aliyeparalaizi kujiconvice kwamba anaweza kutembea. Anapojikonvisi hivo anaruhusu roho yake kuachilia nguvu zake za kioho (Psychic Power) kuja kwenye mwili wake. Zinapoingia mwilini mwake in Extraordinary way mtu anajikuta ameweza kutembea. So technically mtu anakua hajatibiwa kwa cellular regeneration bali zile nguvu zake kiroho alizoziachia kuingia kwenye mwili wake...

Sijui angalau umenielewa mkuu ....?
Sio mtu wa medical labda Rebeca 83 atusaidie hapo kwenye cell regeneration

Mkuu mimi naona unanifundisha concept mpya kabisa kwenye uelewa wangu.

Kwa sababu kwanza mimi katika uhalisia sijawahi kuamini kuwa kuna maisha baada ya kifo (There is life after death), mimi nimekuwa nikiamini kuwa mtu akifa ndiyo habari yake imeishia hapo na hili wazo la kwamba roho inaacha mwili inaenda mahali huwa nazichukulia kama stori za vijiweni tu maana ki uhalisia ni nadharia hakuna ushahidi wenye mashiko kuwa kuna maisha baada ya kifo.

By the way nitajaribu kufatilia maada zako za nyuma nijaribu kijifunza hayo mambo ya kiroho labda huenda ukanibadili kifikra maana always I belive Unazaliwa, unaishi unakufa wengine wanaendelea kuzaliana (pepertuation of life) na hata habari za kiama bado zinathibitika kinadharia.

Nishajaribu kujiuliza maswali mengi sana kuhusu uwepo wa Super natural power (Mungu) lakini katika kutafakari niliishia kupoteza network hakuna nilicho gain za ya kujikuta na maswali juu y maswali.
 
Mungu sio supernatural power...
Kwakua hapa tunaimani kinzani basi tunaweza tusielewane. Je kama huamini katika Uwepo wa Mungu unaamini katika nini???? Unajua kua mwili wako umeumbwa katika Worship mode?? Maisha yako hayatakamilika kama huna wa kumuabudu....So upende usipende lazima uabudu kwakua mwiliwako umeumbwa namna hiyo. Kusudi lako la kwanza ni kuabudu. So hatakama usipomuabudu Mungu unaubudu kitu kingine either kwakujua au kutokujua.

Huamini katika maisa mwingine baada ya kifo..ukishakufa ndio umekufa.
Je unaamini katika Soul, spirit and body kua vipo?? Unaamini uwepo wa Mind na Brain?? Unaamini katika uwepo wa Subconscious mind na Hypothalamus??

Ni mdau wa Physics au Biology au Sayansi kiujumla?
 
Mkuu umeeleweka vizuri sana. Mimi hapo ukiongelea mambo ya kiroho huwa unanigusa sana. Napenda Sana kujua na kujifunza kuhusiana na mambo ya kiroho,, ni kweli kila kitu iwe ni ugonjwa au jambo lolote lile linalotokea mwilini, source yake huwa ni rohoni, mwilini lina Manifest tu, iwe ni ugonjwa, kazi, mafanikio, uzao, akili, uchumi, laana, mikosi, n.k. Siku zote katika maisha ni muhimu sana kujua chanzo. Mambo ya kiroho ni nadra sana kusikia yakiongelewa, lakini ndio kwenye reality yetu. Wengi huwa tanaziangalia changamoto/ situation mbalimbali tulizo nazo kwenye maisha na kujaribu kuzitatua phisical kumbe ungeanzia rohoni ingekuwa ni nyepesi Sana.
Samahani kama nimetoka nje ya mada
Bila samahani...
Tunachukulia poa sana mambo ya kiroho..
Kama kuna kitu ungependa kuuliza??
 
Mkuu njia ya kwanza kuamka kiroho kwanza lazima UAMINI kuwa una uwezo na nguvu ndani yako ya kutawala maisha yako.

Kama ni mkristo sali sana ili kuimarisha hiyo nguvu. Kama ni muislamu pia swali sana ili kuimarisha hiyo nguvu.

Lengo la kusali sana ni kuongeza ukaribu na Mungu. Mungu ni roho, hivyo automatically utakuwa unaongeza uwezo wako wa kiroho na ndiyo kuiamsha.

Fanya meditation sana, hii inasaidia katika kuuelewa ulimwengu wako wa ndani na kuunganisha nafsi, akili na roho hivyo kuuelewa ulimwengu wako wa nje pia. (Kuna mengi hapa katika meditation, zaidi Fanya meditation kwa ku-focus katika nguvu yako ya ndani).

Kumbuka meditation zipo za aina tofautitofauti. Siyo lazima ukae ukunje miguu kama wale monks wa budhism.

Unaweza meditate kwa kusoma bible au Quran, kutegemeana na imani yako. Au pia unaweza tafuta sehemu tulivu na ukafanya meditation ukiwa umekaa.

Usiruhusu mtu kujua undani wako sana kupita kiasi (unafanya nini, background ya maisha yako, unaishije, yaani mambo yako wahusishe wale ambao unawaamini na nafsi yako haiwezi jihukumu ikitokea umemwambia jambo fulani.)

Jifunze kusikiliza sauti ya ndani yako. Ukitaka kufanya jambo nafsi yako ikasita, jiulize kwa undani kwanini ? Ukipata majibu ndipo uamue kufanya hilo jambo kutegemea na majibu utakayopata.

Usiidanganye nafsi yako, ukifanya jambo ovu kuwa mtu wa kukubali na kutubu. (Jitahidi kuwa mwaminifu kwa wewe mwenyewe) na usiwe mwaminifu kwasababu ya mtu fulani, Hapana. Kuwa mwaminifu kwa wewe mwenyewe.

Kama ndiyo mwanzo utahitaji muda na jitihada katika kuimarisha nguvu yako, ila practice sana.

Pia unaweza ongeza na mazoezi ya kawaida kutegemeana. Binafsi nimepitia mafunzo ya shoulin kung fu, hivyo mazoezi magumu na meditation mara kwa mara zimenisaidia sana katika kuielewa nguvu yangu ya kiroho.

Lakini yote yafanyike kwa nia njema.
Umeeleza vyema vile navyopenda.. hongera sana. Wengi hua wanakosea kwenye meditation maana hua hawaangalii back up ya meditation yao. Meditation nzuri ni ile inayotakana na imani yako -Mungu.
 
Mungu sio supernatural power...
Kwakua hapa tunaimani kinzani basi tunaweza tusielewane. Je kama huamini katika Uwepo wa Mungu unaamini katika nini???? Unajua kua mwili wako umeumbwa katika Worship mode?? Maisha yako hayatakamilika kama huna wa kumuabudu....So upende usipende lazima uabudu kwakua mwiliwako umeumbwa namna hiyo. Kusudi lako la kwanza ni kuabudu. So hatakama usipomuabudu Mungu unaubudu kitu kingine either kwakujua au kutokujua.

Huamini katika maisa mwingine baada ya kifo..ukishakufa ndio umekufa.
Je unaamini katika Soul, spirit and body kua vipo?? Unaamini uwepo wa Mind na Brain?? Unaamini katika uwepo wa Subconscious mind na Hypothalamus??

Ni mdau wa Physics au Biology au Sayansi kiujumla?

Ki ukweli mimi sina ninacho abudu kwa sasa naweza kusema hivo, ninachojua mimi ni nimezaliwa nimekuta maisha yanaendelea duniani, nikakuta elimu ya kidunia inaendelea na mimi nikasonga nayo na ninacho subiri hapa ni kufa tu full stop na ni ndicho ninachodhani binadamu wengi tuko hivo.

Nikiwa mdogo nilikuwa naenda sana sunday school nikijua ni utamaduni tu labda na ilikuwa kama amri kutoka kwa wazazi usipoenda unapigwa lakini nilipofikia umri wa kubalehe na kuanza kujitambua ki ukweli sijawahi kurudi tena kanisani ingawa wazee wangu (wazazi ndiyo huwa watu wa kusali).

Ilifikia time nilipofaulu kwenda kidato cha tano mzee wangu aligoma kunipeleka shule akanambia "mimi sisomeshi mapagani".

Baada ya hapo Mama alinitetea nikaenda shule kwa sababu shule ilikuwa ni huko mikoa mbali ikawa nimepua kidogo maana hakuna wa kuniuliza kama jumapili nimesali hata mzee alipokuwa akinipigia simu namwambia ndiyo nimesali ila kiuhalisia ilikuwa hamna, ilifikia mda mzee ananipigia siku kunambia nimeota ndotoni hausali alafu unajihusisha na mambo ya dunia, nikamwambia mzee hamna labda hizo ni ndoto zako kwa sababu mwanao niko mbali.

Ndiyo hivo maisha yangu yalikuwa ila kitu pekee ambacho mimi naweza sema nidhaifu ama ndiyo weakness yangu ilipo ni kwamba :

Mimi napenda sana kujifunza vitu vipya, yani niko addicted vibaya mno na hasa kuhusu huu ulimwengu ( Observable Universe) ulivyotokea.

Napenda sana kujifunza mambo yahusuyo sayansi na falsafa.

Wana falsafa waliostaraabika tangu kale na kuleta ustaarabu duniani (hasa wagiriki wa kale) kama kina Socrates, pilato na kina Aristotle ndiyo huwa chai yangu huwa napenda sana kuyasoma mawazo yao na walichoamini kuhusu huu ulimwengu.

Ukija watu kama kina Albert Einstein, kina Karl Max, kina Galilei Galileo (Ambaye kanisa la roma lilimuua kwa kuusema ukweli) ndiyo mara nyingi napenda kujifunza kutoka kwenye mawazo yao.

Na hivi ndivyo kumenifanya mimi naishi duniani bila woga (Maana mara nyingi watu wanaosema wanaabudu huwa wanaishi kwa hofu sana hata hawana hakika kama kesho wataamka) .

Ila msingi wangu wa mimi kutokuabudu unaanziaga kwa kujiuliza swali hili kwamba "Kwanini wanadamu wanaabudu na kukiamini kitu wasichokiona kwa milango ya fahamu wala kukigusa " ? Hapa ndipo msingi wa mimi kutoabudu chochote ulipojengwa.

NB : mpaka sasa geto kwangu mimi ninapo ishi nna Biblia na huwa napenda kuisoma ninapokuwa nimemaliza shughuli zangu ila changamoto inayonikabili ni kwamba ina mafumbo mengi sana kwa mara nyingi huwa nasoma kama gazeti tu maana ki ukweli humo kuna hadithi zinanifurahishaga na kunifanya nicheke sana.

Hasa hadithi ya wana wa Israel kutoka utumwani misri wakiongozwa na Musa kuelekea nchi ya ahadi ni hadithi ambayo huwa inanifanyaga nicheke sana kwa sababu safari ilikuwa na matukio ya kufurahisha.
 
harakati za siri huu uzi hope hujawah kuusoma. Upo jukwaa la dini

Je wafahamu kua kama ukisafiri ukarudi miaka ya nyuma (Time Traveling) hadi kipindi Wale mitume 12 wa Yesu bado wapo ukamwambia Petro nionyeshe JESUS CHRIST, Petro atashangaa Kisha atakuuliza JESUS ni nani? Unajua kwanini? Fuatana nami mwandishi wako Davinci nikujuze Jinsi jina YEHOSHUA lilivyobadilika kua Jesus.

Wakati malaika Gabriel alipomtokea Bikra Maria kamwambia kua atazaa mtoto na jina analotakiwa ampe mtoto, (Luke 1:31) Jina alilosikia maria kutoka kwenye lips za Gabliel lilikua linafanana, kama sio lenyewe kabisa Yehoshua ambalo linatamkwa Yeh-ho-shoo'-ah. Katikalugha ya Kiebrania cha kisasa jina "Yehoshua" inaandikwa
53ac5e922b8f171b29abaad82c96c76b.jpg

na inasomwa kutoka kulia kwenda kushoto. Jina hilo limeunganisha maneno mawili ya kiebrania. Neno la kwanza ni, "Yeh-ho", ambayo ni sehemu ya Jina la MUNGU ambalo muda mwingine linatumiwa mwanzo au mwisho wa majina ya kiebrania.Sehemu ya pili mabayo ni "shua", ni jina la kiebrania linalomaanisha OKOA hivyo jina "Yehoshua" lamaanisha kua MUNGU ANAOKOA. Jina Yehoshua liliendelea kufupishwa kutokana na matumizi ya kila siku ndivyo kama ilivyotokea kwa jina Barbara ambalo hufupishwa na kua Barb . Hivyom jina la Yehoshua lilifupishwa na kuwa Yeshua.
a7e2b600dc5bf27cc662f55c7c314c0b.jpg

Tafsiri.... Kiebrania kwenda Kigiriki
Mapema, Wakati injili inaandikwa habari ya Yeshua Masiah ilianza kuenezwa kwa watu wa mataifa na habari zake zikawa zinatafsiriwa kwenda kwenye lugha ya Kigiriki kutoka Kiebrania.Sasa ipo hivi kuna njia mbili ambapo jina la Kiebrania laweza tafsiriwa kutokana na changamoto ya lugha, siku zote jina la kiebrania hua limebeba maana hivyo njia ya kwanza ni kutafsiri jina kutokana na maana yake pia njia ya pili ambayo hua inatumiwa sana inaitwa transliteration, Ambapo ni kutafsiri jina kutokana na sauti ya jina linavyotamkwa, hivyo kama watafsiri wa Habari za injili walitafsiri jina Yeshua kutokana na historia basi tatafahamu kua maana yake ni MUNGU AOKOA kwani hivyo ndivyo inavyomaanisha
Kwa kesi ya jina la "Yeshua", ulimwengu wa watu wanao ongea kigiriki waritafsiri vizuri jina lake, hii inahusisha mchakato rahisi wa kuchanganya sauti za herufi ili msomaji atakapo maliza kusoma amalizie na sauti ile aliyoanza nayo wakati anaanza kusoma. Hili sio tatizo ila kwenye jina la Yeshua kuna matatizo manne kuleta katika Kigiriki. Mawili yalikua ni kwamba lugha ya kigiriki cha zamani haikua inajumuisha sauti mbili ambazo zilikua zinapatikana kwenye jina Yeshua. Hii ni ajabu kwa watu wanaongea kingereza ila ukweli ni kwamba lugha ya kigiriki cha zamani haikua na sauti "Y" kama kwenye neno YES pia haikuwa na sauti ya "Sh" kama kwenye neno SHOW
Sauti ya karibu zaidi ya mtu anayezungumza Kigiriki inaweza kuja kufanya sauti ya Y kwa kutumia herufi mbili za kigiriki ambazo ni Iota na Eta pamoja ambapo itatokea sauti ya "ee-ay", pia mtu anayezungumza kigiriki anaweza kutengeneza sauti ya sh kwa kutumia herufi sigma . Kwa mabadiliko hayo mawili jina la "Yeshua" lilitamkwa na wagiriki "ee-ay-soo-ah".
Tatizo la tatu katika kutafsri jina yoshua ni kua kiasili majina ya kiume ya kigiriki hayaishii na irabu, majina yote yaliyoishia na irabu yaliongezewa herufi sigma (S) kama kiambishi tamati chake. Hii ilitokana na sababu kua Mungu wa wagiriki Zeus jina lake linaishia na S, ndio maana hata majina ya wahusika kwenye biblia yalikua yanaishia na S. mfano Judah ilibadirika kua Judas, Cephah (ikimaanisha mwamba") ilibadirika kua Cephas, Apollo ilibadirika kua Apollo, Barnabie ilibadirika kua Barnabas, Matthew ilibadirika kua Matthias nk nk.
Hivyo basi "ee-ay-soo-ah" ilibadirika na kua "ee-ay-soo-ah-s". Tatizo la nne ni kwamba sauti za irabu mbili kabla ya s haipom wala haijawahi kuonekana kwenye mtiririko wa lugha ya kigiriki, hivyo ili kureta mtiririko unaoeleweka hivyo waliziondoa hizo irabu jina likawa "ee-ay-soos". Mbali na kuliongezea jina s ili liwe limekaa kiume hii ilifanya wagiriki kuweza kulitafsiri jina la Yeshua. Kwa hatua hii, jina Yeshua lilipoteza maana yake na 75% ya sauti yake. Kizuizi cha mwisho cha sauti hiyo kilipatikana katika "oo" (kama kwenye "soon"). Yeshua kwa watu wanaongea kigiriki ilifahamika kama "ee-ay-soos" kwa muda wa takribani miaka 400 "ee-ay-soos" inaonekana hivi katika lugha ya kigiriki
bb1b7446c1b133385c3e90a0a7f468fc.jpg

, ni kama kingereza unasoma kutoka kushoto kwenda kulia

Tuendelee na tafsiri...Kutoka kigiriki kwenda kilatini
Mnamo miaka ya 400 A.D. kilatini kilikua ndio lugha ya inayotumika kwenye dini ya Ukristo na matoleo ya Kigiriki ya Agano Jipya yalitafsiriwa Kilatini. Biblia ya kilatini au Vulgate kama ilivyokua inaitwa , pia ilitafsiri kile kilichobaki cha jina la Kigiriki la Yeshua kwa kuleta sauti sawa ya "ee-ay-soos". Hii ilikuwa rahisi, kwa sababu sauti zote za kigiriki kwenye jina hili yalitamkwa hivyo hivyo kwenye kilatini. Herufi za kilatini ni tofauti na kigiriki lakini kwa kiasi Fulani zinafanana na kingereza. Hivyo basi tafsri mpya ya jina la kigiriki "ee-ay-soos" ilianza kuandikwa
0689cc7f9a0874aef8ae03b3b2ab4fa1.jpg

kwa kilatini na jinsi inavyotamkwa ilikua inafanana na wagiriki wanavyotamka, jina la Yeshua lilitamkwa hivyo kwa kilatini na wakristo karibia miaka 1000

Tafsiri ya mwisho.... Kilatini kwenda Kingereza
Wakati huo lugha ya kingereza ikiwa inaendelea kukua kabla ya karne ya 12 herufi J haikuwepo katika lugha ya kingereza , Sauti ya herufi J haikuwepo kwenye lugha ya Kiebrania,kigiriki,Kiaramu,wala kilatini. Hii inaonyesha kua hakuna mtu kipindi hicho alitamka jina la Yeshua kwa lugha ya kingereza Jesus.
Mnamo mwanzoni mwa karne ya 12 herufi J ilianza kutumika katika lugha ya kkingereza cha kati. Kuanza kutumika kwa herufi J.kwenye lugha ya kingereza kulipelekea herufi kama Y na I baadhi ya maneno nafasi yake kuchukuliwa na herufi J, Hii ilitumika san kwa majina ya kiume yanayoanza na herufi Y au I kwakua waliona sauti ya herufi J ilikua imekaa kiume zaidi, hapa ndipo baadhi ya majina yalibadilishwa mfano Iames ilibadirika kua "James", Yohan ilibadilika kua "John", na mengineo.
Mnamo waka 1384 John Wycliffe alitafsiri agano jipya kutoka kilatini kwenda Kingereza kwa mara ya kwanza na chanzo chake kikuu ilikua Biblia ya kilatini ( Vulgate). Wycliffe aliendelea kutyumia lugha ya kilatini na matamshi ya jina la Iesus. Kipindi hicho vyombo vya uchapaji vilikua havijagunduliwa, nakala chache tu za biblia alizoandika kwa mkono Wycleaf ndizo zilizalishwa.

Miaka 1450 Gutenburg aligundua Chombo cha uchapaji , kasha mwaka 1526 William Tyndale alitafsiri Agano jipya kutoka biblia ya kilatini kwenda kingereza akiwa na msaada wa maandiko ya kigiriki cha zamani. Tyndale alitaka biblia itafsiriwe kwenda kwenye lugha ya watu wengi na nakala nyingi za tafsiri yake zilichapishwa kwa msaada wa mashine ya kuchapisha. Tyndale alikua mtu wa kwanza kutumia herufi J kwenye jina la
27eed6fab8c346ed24d225ff7f53c189.jpg

. Utamkaji huu mya wa jina la yesu ulisambaa baadae jina la jesus likawa linatamkwa "Jee-zuz".Karne ya 17 herufi J iliingizwa rasmi kwenye kamusi .

Mwaka 1611 Biblia ya King James ilirahisisha baadhi ya majina katika kuyatamka kama tunavyolitamka jina la Jesus leo hii, kila jina katika biblia linaloanza na herufi J lilikuja kwa njia hii. Majijna kama Jeremiah, Jerusalem, Jew, Judah, John na kadhalika
Pamoja na utamkaji huu rasmi wa jina "Jee-zuz", sauti ya mwisho iliyobakia kwenye jina la Yeshua", (sauti ya oo kama kwenye neno "soon"), ilitoweka. Si sauti walamaana iliyobakia inatumbulisha jina la Yeshua. Lakini itambulike pia kua neno "Christ" sio jina bali ni cheo. Ilitokana na tafsiri ya kigiriki ya cheo kinachoitwa Messiah ikimaanisha mpakwa mafuta ". Hivyo hayo yote yaliacha utamkaji wa jina Yeshua the Messiah isambapo inatafsiriwa na kutamkwa kwa lugha ya kingereza na "Jee-zuz Chr-i-st".
Hivi ndivyo jina la Jesus lilivyopatikana kutoka kwenye jina Yeshua.. Ikumbukwe kua jina la Yeshua limeishi karibia miaka 1500 duniani huku jina la Jesus likiwa limetokea miaka kama 300 iliyopita.

Maoni ya mwandishi
Upande wangu naona sisi watanzania na Kiswahili chetu tunatamka vizuri jina la yesu sawasawa na waebrani, lakini haijalishi jina lake masia ni lipi aitwe Juma, Diamond, Hasani,Raymond, Magufuli, Gudume, Nkuruziza, Da'Vinci, Muhamad nakadharika cha muhimu ni ule wokovu wa uzima wa milele aliotuletea wanadamua hapa duniani.
Tchao..
Writtten and Prepared by
DaVinci..
JF Expert Member
Mkuu asante kwa andiko hili nami ni mmoja wa ambao hatukuliona mapema..

Nina swali..
Tafsiri ya majina ya Jesus na God katika lugha za makabila yetu ilifanywa na nani? Tukianza na Jesus kuwa ndio Yesu na God ndio Mungu...
 
Hapo kwenye kuogea chumvi au maji ya baharini naweka imani yangu huko maana hata kwenye biblia ipo.

Nitaenda baharini kutoa mikosi na gundu zinazoniandama
 
Mkuu nimetafuta sana kwenye Bible naomba kama una kumbukumbu nikumbushe hilo andiko
Ezekieli : 43
24 Nawe utawaleta karibu mbele za BWANA, na makuhani watamwaga chumvi juu yao, nao watawatoa wawe sadaka za kuteketezwa kwa BWANA.
 
Mkuu nimetafuta sana kwenye Bible naomba kama una kumbukumbu nikumbushe hilo andiko
2 wafalme : 2
21 Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, BWANA asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza.
 
Mkuu nimetafuta sana kwenye Bible naomba kama una kumbukumbu nikumbushe hilo andiko
Natumaini umeelewa kwanini RC tunatumia chumvi

Mambo ya walawi : 2
13 Tena, kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia chumvi; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la Mungu wako; utatoa chumvi pamoja na matoleo yako yote.
 
Nimeelewa mkuu,asante sana
 
Hapa sijakuelewa mkuu.. please maelezo zaidi
Oooh mkuu, nilivyopitia uzi wako unaoelezea jinsi introverts wanavyoteseka kuchangamana na jamii,..., naam niliyopitia ufafanuzi wako, nilikuelewa mno. Kwa sababu kwa muda mrefu nilikuwa sijitambui, ila baada ya kusoma ule Uzi, nilijitambua kwa kiasi kikubwa. Naam nikifikiria, naifurahia mno hali niliyonayo, hivyo nikifanya imagination... Ya baadhi ya tabia za introverts, naam nikiangalia na mambo unayoandika jinsi yalivyoshiba ingawa sijayafuatilia sana, walakini nimeamua kwamba, miezi michache ijayo nitafuatilia nyuzi zako za nyuma, maana najua Nina mengi ya kujifunza, kwa kuwa ndiyo kwanza nipo kwenye hatua za awali katika safari hii ya kujifunza mambo haya.

Hivyo, Mimi kuandika kwa kifupi hivyo, nilimaanisha kwamba; umejawaa na maarifa na maneno ya fahamu moyoni mwako, naam yakini yaweza kuwa tofauti na unavyoonekana. Kama wanenavyo "Quite(introverts) people have the loudest minds", naam watu wenye mengi mioyoni mwao kuliko wanavyoonekana.

Hongera sana mkuu.
 
2 wafalme : 2
21 Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, BWANA asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza.
Mkuu, hivi naweza kujifunza habari za Mungu, nikaelewa kwa kina na kuwa karibu naye bila kufundishwa na watu wenye mwili?
 
Oooh mkuu, nilivyopitia uzi wako unaoelezea jinsi introverts wanavyoteseka kuchangamana na jamii,..., naam niliyopitia ufafanuzi wako, nilikuelewa mno. Kwa sababu kwa muda mrefu nilikuwa sijitambui, ila baada ya kusoma ule Uzi, nilijitambua kwa kiasi kikubwa. Naam nikifikiria, naifurahia mno hali niliyonayo, hivyo nikifanya imagination... Ya baadhi ya tabia za introverts, naam nikiangalia na mambo unayoandika jinsi yalivyoshiba ingawa sijayafuatilia sana, walakini nimeamua kwamba, miezi michache ijayo nitafuatilia nyuzi zako za nyuma, maana najua Nina mengi ya kujifunza, kwa kuwa ndiyo kwanza nipo kwenye hatua za awali katika safari hii ya kujifunza mambo haya.

Hivyo, Mimi kuandika kwa kifupi hivyo, nilimaanisha kwamba; umejawaa na maarifa na maneno ya fahamu moyoni mwako, naam yakini yaweza kuwa tofauti na unavyoonekana. Kama wanenavyo "Quite(introverts) people have the loudest minds", naam watu wenye mengi mioyoni mwao kuliko wanavyoonekana.

Hongera sana mkuu.
Gratitude mate...nipo tofauti na nionekanavyo. Knowledge is my my hobby and all thanks to the Almighty who made me to be this way ✌️

Ukitaka kuanza kuzifuatilia utasema nikuelekeze yakuanza nayo. Maana nyingine zipo jukwaa la dini sijui Kama una Access
 
Mkuu asante kwa andiko hili nami ni mmoja wa ambao hatukuliona mapema..

Nina swali..
Tafsiri ya majina ya Jesus na God katika lugha za makabila yetu ilifanywa na nani? Tukianza na Jesus kuwa ndio Yesu na God ndio Mungu...
Kwanza upande wa Yesu kwenye makabila yetu sidhani kama kuna kabila lenye kutumia jina lingine kuwakilisha Yesu. Makabila Mengi niliyowahi kufahamu wanamuita Yesu kama Yesu....nitaeleza mbeleni Why.

Makabila Mengi Tanzania jina la Mungu linatamkwa tofauti tofauti na kila kabila. Japo kwasababu ni kibantu kunakua kuna mzizi unaofanana kutoka kwenye kabila moja na lingine nadhani makabila mengi ambayo ni wabantu jina Mungu wanatumia mzizi wa -MANA-(kama sijakosea) Je mkuu kabila lenu mnamwitaje Mungu?

Sababu ni kwamba kabla ya ukoloni kila jamii ilikua na taratibu zake za kuabudu hapa tanzani kutokana na mila na tamaduni za kabila husika. Hivyo basi wamisionari walivyokuja kumtangaza God makabila mengi walilichukua jina la God na kulibadiri kutokana na wao kwenye kabila lao walikua waniita vipi Kitu wanachoabudu wakiwa wanatambika. Kama ni msufi ndio uliabudiwa walikua wanauita Imana basi GOD nae wakamuita Imana.. nk nk.

Lakini pia ukumbuke kua Maeneo mengi TZani jamii ziliunganishwa kwa kiswahili so kitu kilichokua kinaabudiwa haijalishi ni mti,msitu, mto nk kwa pamoja vitu hivyo wiviita Mungu kwa kiswahili.

Sasa upande wa Yesu anaitwa hivyo hivyo Yesu kwasababu kwenye dini zao za asili kulikua hakuna utatu mtakatifu..hivyo Yesu lilikua neno jipya.

Kama bado una swali Usiache kuuliza
 
Ki ukweli mimi sina ninacho abudu kwa sasa naweza kusema hivo, ninachojua mimi ni nimezaliwa nimekuta maisha yanaendelea duniani, nikakuta elimu ya kidunia inaendelea na mimi nikasonga nayo na ninacho subiri hapa ni kufa tu full stop na ni ndicho ninachodhani binadamu wengi tuko hivo.

Nikiwa mdogo nilikuwa naenda sana sunday school nikijua ni utamaduni tu labda na ilikuwa kama amri kutoka kwa wazazi usipoenda unapigwa lakini nilipofikia umri wa kubalehe na kuanza kujitambua ki ukweli sijawahi kurudi tena kanisani ingawa wazee wangu (wazazi ndiyo huwa watu wa kusali).

Ilifikia time nilipofaulu kwenda kidato cha tano mzee wangu aligoma kunipeleka shule akanambia "mimi sisomeshi mapagani".

Baada ya hapo Mama alinitetea nikaenda shule kwa sababu shule ilikuwa ni huko mikoa mbali ikawa nimepua kidogo maana hakuna wa kuniuliza kama jumapili nimesali hata mzee alipokuwa akinipigia simu namwambia ndiyo nimesali ila kiuhalisia ilikuwa hamna, ilifikia mda mzee ananipigia siku kunambia nimeota ndotoni hausali alafu unajihusisha na mambo ya dunia, nikamwambia mzee hamna labda hizo ni ndoto zako kwa sababu mwanao niko mbali.

Ndiyo hivo maisha yangu yalikuwa ila kitu pekee ambacho mimi naweza sema nidhaifu ama ndiyo weakness yangu ilipo ni kwamba :

Mimi napenda sana kujifunza vitu vipya, yani niko addicted vibaya mno na hasa kuhusu huu ulimwengu ( Observable Universe) ulivyotokea.

Napenda sana kujifunza mambo yahusuyo sayansi na falsafa.

Wana falsafa waliostaraabika tangu kale na kuleta ustaarabu duniani (hasa wagiriki wa kale) kama kina Socrates, pilato na kina Aristotle ndiyo huwa chai yangu huwa napenda sana kuyasoma mawazo yao na walichoamini kuhusu huu ulimwengu.

Ukija watu kama kina Albert Einstein, kina Karl Max, kina Galilei Galileo (Ambaye kanisa la roma lilimuua kwa kuusema ukweli) ndiyo mara nyingi napenda kujifunza kutoka kwenye mawazo yao.

Na hivi ndivyo kumenifanya mimi naishi duniani bila woga (Maana mara nyingi watu wanaosema wanaabudu huwa wanaishi kwa hofu sana hata hawana hakika kama kesho wataamka) .

Ila msingi wangu wa mimi kutokuabudu unaanziaga kwa kujiuliza swali hili kwamba "Kwanini wanadamu wanaabudu na kukiamini kitu wasichokiona kwa milango ya fahamu wala kukigusa " ? Hapa ndipo msingi wa mimi kutoabudu chochote ulipojengwa.

NB : mpaka sasa geto kwangu mimi ninapo ishi nna Biblia na huwa napenda kuisoma ninapokuwa nimemaliza shughuli zangu ila changamoto inayonikabili ni kwamba ina mafumbo mengi sana kwa mara nyingi huwa nasoma kama gazeti tu maana ki ukweli humo kuna hadithi zinanifurahishaga na kunifanya nicheke sana.

Hasa hadithi ya wana wa Israel kutoka utumwani misri wakiongozwa na Musa kuelekea nchi ya ahadi ni hadithi ambayo huwa inanifanyaga nicheke sana kwa sababu safari ilikuwa na matukio ya kufurahisha.
Nikupongeze kwa kupenda kufuatilia wanafalsafa..mimi pia ni mgonjwa sana saikolojia na falsafa. Yaani napenda sana tukae na mtu tuanze kudadavua falsafa za mtu mmoja mmoja. Hebu jaribu kusoma falsafa za Stoic kutoka kwa mwanafalsafa Zeno wa Citium...Utakutana na mafunzo fulani hivi ya masha anatamani tuishi. Kama tungeyaishi basi dunia isingekua uwanja wa fujo wa kuhombea mali tutakazo ziacha...BTW wanafalsafa ambao nimependa wawe Mentor wagu ni Thomas Aquinas, Paulo,Carl max, Socrates,Yesu,Nyerere, Fransisco wa Asizi, Leonard da vinci.

Turudi kwenye mada yetu!!
Kwanza kabisa Surrender your Ego...ukitaa kujifunza habari za Mungu ni maswala ya imani. Imani haithibitishwi kwa Sayansi wala historia. Imani ni imani.

Hizi ni nyakati za kusikia na kuamini zilikuwepo nyakati za kuona na kuamini bahati mbaya hatujaziishi..so ukitaa kujifunza imani ya Mungu acha kila unachodhani unafahamu kisha mruhusu yule roho aliyeko ndani yako afanye kazi

Ni kweli kuna sehemu zingine biblia inachekesha kweli inakuacha maswali kibaoo
 
Ndgu yangu nimesoma vizuri uzi wako,
Na umesema nyumbani kwako Biblia takatifu unayo,
Jaribu kutenga muda wako uisome vizuri neno kwa neno mstari kwa mstari,
Mungu ana makusudi na wewe kuna jambo anahitaji akushirikishe kiroho na bado hujachelewa,
 
Mkuu ujumbe huu unanihusu mimi???
Naomba uongeze maelezo kama unanihusu labda ndio Mungu anakutumia ili nifahamu jambo analotaka kunsihirikisha
 
Nikupongeze kwa kupenda kufuatilia wanafalsafa..mimi pia ni mgonjwa sana saikolojia na falsafa. Yaani napenda sana tukae na mtu tuanze kudadavua falsafa za mtu mmoja mmoja. Hebu jaribu kusoma falsafa za Stoic kutoka kwa mwanafalsafa Zeno wa Citium...Utakutana na mafunzo fulani hivi ya masha anatamani tuishi. Kama tungeyaishi basi dunia isingekua uwanja wa fujo wa kuhombea mali tutakazo ziacha...BTW wanafalsafa ambao nimependa wawe Mentor wagu ni Thomas Aquinas, Paulo,Carl max, Socrates,Yesu,Nyerere, Fransisco wa Asizi, Leonard da vinci.

Turudi kwenye mada yetu!!
Kwanza kabisa Surrender your Ego...ukitaa kujifunza habari za Mungu ni maswala ya imani. Imani haithibitishwi kwa Sayansi wala historia. Imani ni imani.

Hizi ni nyakati za kusikia na kuamini zilikuwepo nyakati za kuona na kuamini bahati mbaya hatujaziishi..so ukitaa kujifunza imani ya Mungu acha kila unachodhani unafahamu kisha mruhusu yule roho aliyeko ndani yako afanye kazi

Ni kweli kuna sehemu zingine biblia inachekesha kweli inakuacha maswali kibaoo

"Hizi ni nyakati za kusikia na kuamini,zilikuwepo nyakati za kuona na kuamini ila sisi hatujaziishi" 😁😁😁

Hii sentensi imenifanya nicheke tu.

Mkuu Umenena vyema kuwa nikitaka kujifunza mambo ya kiroho inabidi niache kila kitu ninachodhani najua alafu nimruhusu roho aliyeko ndani yangu atende kazi, swali langu lipo kwenye huyu aliyeko ndani yangu, Je nitampaje go ahead atende kazi, yani nitawasiliana nae vipi kwamba bhan nimesalimu amri sasahivi niongoze wewe ili niijue kweli ni ipi.
 
Back
Top Bottom