harakati za siri huu uzi hope hujawah kuusoma. Upo jukwaa la dini
Je wafahamu kua kama ukisafiri ukarudi miaka ya nyuma (Time Traveling) hadi kipindi Wale mitume 12 wa Yesu bado wapo ukamwambia Petro nionyeshe JESUS CHRIST, Petro atashangaa Kisha atakuuliza JESUS ni nani? Unajua kwanini? Fuatana nami mwandishi wako Davinci nikujuze Jinsi jina YEHOSHUA lilivyobadilika kua Jesus.
Wakati malaika Gabriel alipomtokea Bikra Maria kamwambia kua atazaa mtoto na jina analotakiwa ampe mtoto, (Luke 1:31) Jina alilosikia maria kutoka kwenye lips za Gabliel lilikua linafanana, kama sio lenyewe kabisa Yehoshua ambalo linatamkwa Yeh-ho-shoo'-ah. Katikalugha ya Kiebrania cha kisasa jina "Yehoshua" inaandikwa
na inasomwa kutoka kulia kwenda kushoto. Jina hilo limeunganisha maneno mawili ya kiebrania. Neno la kwanza ni, "Yeh-ho", ambayo ni sehemu ya Jina la MUNGU ambalo muda mwingine linatumiwa mwanzo au mwisho wa majina ya kiebrania.Sehemu ya pili mabayo ni "shua", ni jina la kiebrania linalomaanisha OKOA hivyo jina "Yehoshua" lamaanisha kua MUNGU ANAOKOA. Jina Yehoshua liliendelea kufupishwa kutokana na matumizi ya kila siku ndivyo kama ilivyotokea kwa jina Barbara ambalo hufupishwa na kua Barb . Hivyom jina la Yehoshua lilifupishwa na kuwa Yeshua.
Tafsiri.... Kiebrania kwenda Kigiriki
Mapema, Wakati injili inaandikwa habari ya Yeshua Masiah ilianza kuenezwa kwa watu wa mataifa na habari zake zikawa zinatafsiriwa kwenda kwenye lugha ya Kigiriki kutoka Kiebrania.Sasa ipo hivi kuna njia mbili ambapo jina la Kiebrania laweza tafsiriwa kutokana na changamoto ya lugha, siku zote jina la kiebrania hua limebeba maana hivyo njia ya kwanza ni kutafsiri jina kutokana na maana yake pia njia ya pili ambayo hua inatumiwa sana inaitwa transliteration, Ambapo ni kutafsiri jina kutokana na sauti ya jina linavyotamkwa, hivyo kama watafsiri wa Habari za injili walitafsiri jina Yeshua kutokana na historia basi tatafahamu kua maana yake ni MUNGU AOKOA kwani hivyo ndivyo inavyomaanisha
Kwa kesi ya jina la "Yeshua", ulimwengu wa watu wanao ongea kigiriki waritafsiri vizuri jina lake, hii inahusisha mchakato rahisi wa kuchanganya sauti za herufi ili msomaji atakapo maliza kusoma amalizie na sauti ile aliyoanza nayo wakati anaanza kusoma. Hili sio tatizo ila kwenye jina la Yeshua kuna matatizo manne kuleta katika Kigiriki. Mawili yalikua ni kwamba lugha ya kigiriki cha zamani haikua inajumuisha sauti mbili ambazo zilikua zinapatikana kwenye jina Yeshua. Hii ni ajabu kwa watu wanaongea kingereza ila ukweli ni kwamba lugha ya kigiriki cha zamani haikua na sauti "Y" kama kwenye neno YES pia haikuwa na sauti ya "Sh" kama kwenye neno SHOW
Sauti ya karibu zaidi ya mtu anayezungumza Kigiriki inaweza kuja kufanya sauti ya Y kwa kutumia herufi mbili za kigiriki ambazo ni Iota na Eta pamoja ambapo itatokea sauti ya "ee-ay", pia mtu anayezungumza kigiriki anaweza kutengeneza sauti ya sh kwa kutumia herufi sigma . Kwa mabadiliko hayo mawili jina la "Yeshua" lilitamkwa na wagiriki "ee-ay-soo-ah".
Tatizo la tatu katika kutafsri jina yoshua ni kua kiasili majina ya kiume ya kigiriki hayaishii na irabu, majina yote yaliyoishia na irabu yaliongezewa herufi sigma (S) kama kiambishi tamati chake. Hii ilitokana na sababu kua Mungu wa wagiriki Zeus jina lake linaishia na S, ndio maana hata majina ya wahusika kwenye biblia yalikua yanaishia na S. mfano Judah ilibadirika kua Judas, Cephah (ikimaanisha mwamba") ilibadirika kua Cephas, Apollo ilibadirika kua Apollo, Barnabie ilibadirika kua Barnabas, Matthew ilibadirika kua Matthias nk nk.
Hivyo basi "ee-ay-soo-ah" ilibadirika na kua "ee-ay-soo-ah-s". Tatizo la nne ni kwamba sauti za irabu mbili kabla ya s haipom wala haijawahi kuonekana kwenye mtiririko wa lugha ya kigiriki, hivyo ili kureta mtiririko unaoeleweka hivyo waliziondoa hizo irabu jina likawa "ee-ay-soos". Mbali na kuliongezea jina s ili liwe limekaa kiume hii ilifanya wagiriki kuweza kulitafsiri jina la Yeshua. Kwa hatua hii, jina Yeshua lilipoteza maana yake na 75% ya sauti yake. Kizuizi cha mwisho cha sauti hiyo kilipatikana katika "oo" (kama kwenye "soon"). Yeshua kwa watu wanaongea kigiriki ilifahamika kama "ee-ay-soos" kwa muda wa takribani miaka 400 "ee-ay-soos" inaonekana hivi katika lugha ya kigiriki
, ni kama kingereza unasoma kutoka kushoto kwenda kulia
Tuendelee na tafsiri...Kutoka kigiriki kwenda kilatini
Mnamo miaka ya 400 A.D. kilatini kilikua ndio lugha ya inayotumika kwenye dini ya Ukristo na matoleo ya Kigiriki ya Agano Jipya yalitafsiriwa Kilatini. Biblia ya kilatini au Vulgate kama ilivyokua inaitwa , pia ilitafsiri kile kilichobaki cha jina la Kigiriki la Yeshua kwa kuleta sauti sawa ya "ee-ay-soos". Hii ilikuwa rahisi, kwa sababu sauti zote za kigiriki kwenye jina hili yalitamkwa hivyo hivyo kwenye kilatini. Herufi za kilatini ni tofauti na kigiriki lakini kwa kiasi Fulani zinafanana na kingereza. Hivyo basi tafsri mpya ya jina la kigiriki "ee-ay-soos" ilianza kuandikwa
kwa kilatini na jinsi inavyotamkwa ilikua inafanana na wagiriki wanavyotamka, jina la Yeshua lilitamkwa hivyo kwa kilatini na wakristo karibia miaka 1000
Tafsiri ya mwisho.... Kilatini kwenda Kingereza
Wakati huo lugha ya kingereza ikiwa inaendelea kukua kabla ya karne ya 12 herufi J haikuwepo katika lugha ya kingereza , Sauti ya herufi J haikuwepo kwenye lugha ya Kiebrania,kigiriki,Kiaramu,wala kilatini. Hii inaonyesha kua hakuna mtu kipindi hicho alitamka jina la Yeshua kwa lugha ya kingereza Jesus.
Mnamo mwanzoni mwa karne ya 12 herufi J ilianza kutumika katika lugha ya kkingereza cha kati. Kuanza kutumika kwa herufi J.kwenye lugha ya kingereza kulipelekea herufi kama Y na I baadhi ya maneno nafasi yake kuchukuliwa na herufi J, Hii ilitumika san kwa majina ya kiume yanayoanza na herufi Y au I kwakua waliona sauti ya herufi J ilikua imekaa kiume zaidi, hapa ndipo baadhi ya majina yalibadilishwa mfano Iames ilibadirika kua "James", Yohan ilibadilika kua "John", na mengineo.
Mnamo waka 1384 John Wycliffe alitafsiri agano jipya kutoka kilatini kwenda Kingereza kwa mara ya kwanza na chanzo chake kikuu ilikua Biblia ya kilatini ( Vulgate). Wycliffe aliendelea kutyumia lugha ya kilatini na matamshi ya jina la Iesus. Kipindi hicho vyombo vya uchapaji vilikua havijagunduliwa, nakala chache tu za biblia alizoandika kwa mkono Wycleaf ndizo zilizalishwa.
Miaka 1450 Gutenburg aligundua Chombo cha uchapaji , kasha mwaka 1526 William Tyndale alitafsiri Agano jipya kutoka biblia ya kilatini kwenda kingereza akiwa na msaada wa maandiko ya kigiriki cha zamani. Tyndale alitaka biblia itafsiriwe kwenda kwenye lugha ya watu wengi na nakala nyingi za tafsiri yake zilichapishwa kwa msaada wa mashine ya kuchapisha. Tyndale alikua mtu wa kwanza kutumia herufi J kwenye jina la
. Utamkaji huu mya wa jina la yesu ulisambaa baadae jina la jesus likawa linatamkwa "Jee-zuz".Karne ya 17 herufi J iliingizwa rasmi kwenye kamusi .
Mwaka 1611 Biblia ya King James ilirahisisha baadhi ya majina katika kuyatamka kama tunavyolitamka jina la Jesus leo hii, kila jina katika biblia linaloanza na herufi J lilikuja kwa njia hii. Majijna kama Jeremiah, Jerusalem, Jew, Judah, John na kadhalika
Pamoja na utamkaji huu rasmi wa jina "Jee-zuz", sauti ya mwisho iliyobakia kwenye jina la Yeshua", (sauti ya oo kama kwenye neno "soon"), ilitoweka. Si sauti walamaana iliyobakia inatumbulisha jina la Yeshua. Lakini itambulike pia kua neno "Christ" sio jina bali ni cheo. Ilitokana na tafsiri ya kigiriki ya cheo kinachoitwa Messiah ikimaanisha mpakwa mafuta ". Hivyo hayo yote yaliacha utamkaji wa jina Yeshua the Messiah isambapo inatafsiriwa na kutamkwa kwa lugha ya kingereza na "Jee-zuz Chr-i-st".
Hivi ndivyo jina la Jesus lilivyopatikana kutoka kwenye jina Yeshua.. Ikumbukwe kua jina la Yeshua limeishi karibia miaka 1500 duniani huku jina la Jesus likiwa limetokea miaka kama 300 iliyopita.
Maoni ya mwandishi
Upande wangu naona sisi watanzania na Kiswahili chetu tunatamka vizuri jina la yesu sawasawa na waebrani, lakini haijalishi jina lake masia ni lipi aitwe Juma, Diamond, Hasani,Raymond, Magufuli, Gudume, Nkuruziza, Da'Vinci, Muhamad nakadharika cha muhimu ni ule wokovu wa uzima wa milele aliotuletea wanadamua hapa duniani.
Tchao..
Writtten and Prepared by
DaVinci..
JF Expert Member