Je, unafahamu kwanini maisha yako yameandamwa na mikosi pamoja na Mambo mabaya?


Mkuu mimi naona unanifundisha concept mpya kabisa kwenye uelewa wangu.

Kwa sababu kwanza mimi katika uhalisia sijawahi kuamini kuwa kuna maisha baada ya kifo (There is life after death), mimi nimekuwa nikiamini kuwa mtu akifa ndiyo habari yake imeishia hapo na hili wazo la kwamba roho inaacha mwili inaenda mahali huwa nazichukulia kama stori za vijiweni tu maana ki uhalisia ni nadharia hakuna ushahidi wenye mashiko kuwa kuna maisha baada ya kifo.

By the way nitajaribu kufatilia maada zako za nyuma nijaribu kijifunza hayo mambo ya kiroho labda huenda ukanibadili kifikra maana always I belive Unazaliwa, unaishi unakufa wengine wanaendelea kuzaliana (pepertuation of life) na hata habari za kiama bado zinathibitika kinadharia.

Nishajaribu kujiuliza maswali mengi sana kuhusu uwepo wa Super natural power (Mungu) lakini katika kutafakari niliishia kupoteza network hakuna nilicho gain za ya kujikuta na maswali juu y maswali.
 
Mungu sio supernatural power...
Kwakua hapa tunaimani kinzani basi tunaweza tusielewane. Je kama huamini katika Uwepo wa Mungu unaamini katika nini???? Unajua kua mwili wako umeumbwa katika Worship mode?? Maisha yako hayatakamilika kama huna wa kumuabudu....So upende usipende lazima uabudu kwakua mwiliwako umeumbwa namna hiyo. Kusudi lako la kwanza ni kuabudu. So hatakama usipomuabudu Mungu unaubudu kitu kingine either kwakujua au kutokujua.

Huamini katika maisa mwingine baada ya kifo..ukishakufa ndio umekufa.
Je unaamini katika Soul, spirit and body kua vipo?? Unaamini uwepo wa Mind na Brain?? Unaamini katika uwepo wa Subconscious mind na Hypothalamus??

Ni mdau wa Physics au Biology au Sayansi kiujumla?
 
Bila samahani...
Tunachukulia poa sana mambo ya kiroho..
Kama kuna kitu ungependa kuuliza??
 
Umeeleza vyema vile navyopenda.. hongera sana. Wengi hua wanakosea kwenye meditation maana hua hawaangalii back up ya meditation yao. Meditation nzuri ni ile inayotakana na imani yako -Mungu.
 

Ki ukweli mimi sina ninacho abudu kwa sasa naweza kusema hivo, ninachojua mimi ni nimezaliwa nimekuta maisha yanaendelea duniani, nikakuta elimu ya kidunia inaendelea na mimi nikasonga nayo na ninacho subiri hapa ni kufa tu full stop na ni ndicho ninachodhani binadamu wengi tuko hivo.

Nikiwa mdogo nilikuwa naenda sana sunday school nikijua ni utamaduni tu labda na ilikuwa kama amri kutoka kwa wazazi usipoenda unapigwa lakini nilipofikia umri wa kubalehe na kuanza kujitambua ki ukweli sijawahi kurudi tena kanisani ingawa wazee wangu (wazazi ndiyo huwa watu wa kusali).

Ilifikia time nilipofaulu kwenda kidato cha tano mzee wangu aligoma kunipeleka shule akanambia "mimi sisomeshi mapagani".

Baada ya hapo Mama alinitetea nikaenda shule kwa sababu shule ilikuwa ni huko mikoa mbali ikawa nimepua kidogo maana hakuna wa kuniuliza kama jumapili nimesali hata mzee alipokuwa akinipigia simu namwambia ndiyo nimesali ila kiuhalisia ilikuwa hamna, ilifikia mda mzee ananipigia siku kunambia nimeota ndotoni hausali alafu unajihusisha na mambo ya dunia, nikamwambia mzee hamna labda hizo ni ndoto zako kwa sababu mwanao niko mbali.

Ndiyo hivo maisha yangu yalikuwa ila kitu pekee ambacho mimi naweza sema nidhaifu ama ndiyo weakness yangu ilipo ni kwamba :

Mimi napenda sana kujifunza vitu vipya, yani niko addicted vibaya mno na hasa kuhusu huu ulimwengu ( Observable Universe) ulivyotokea.

Napenda sana kujifunza mambo yahusuyo sayansi na falsafa.

Wana falsafa waliostaraabika tangu kale na kuleta ustaarabu duniani (hasa wagiriki wa kale) kama kina Socrates, pilato na kina Aristotle ndiyo huwa chai yangu huwa napenda sana kuyasoma mawazo yao na walichoamini kuhusu huu ulimwengu.

Ukija watu kama kina Albert Einstein, kina Karl Max, kina Galilei Galileo (Ambaye kanisa la roma lilimuua kwa kuusema ukweli) ndiyo mara nyingi napenda kujifunza kutoka kwenye mawazo yao.

Na hivi ndivyo kumenifanya mimi naishi duniani bila woga (Maana mara nyingi watu wanaosema wanaabudu huwa wanaishi kwa hofu sana hata hawana hakika kama kesho wataamka) .

Ila msingi wangu wa mimi kutokuabudu unaanziaga kwa kujiuliza swali hili kwamba "Kwanini wanadamu wanaabudu na kukiamini kitu wasichokiona kwa milango ya fahamu wala kukigusa " ? Hapa ndipo msingi wa mimi kutoabudu chochote ulipojengwa.

NB : mpaka sasa geto kwangu mimi ninapo ishi nna Biblia na huwa napenda kuisoma ninapokuwa nimemaliza shughuli zangu ila changamoto inayonikabili ni kwamba ina mafumbo mengi sana kwa mara nyingi huwa nasoma kama gazeti tu maana ki ukweli humo kuna hadithi zinanifurahishaga na kunifanya nicheke sana.

Hasa hadithi ya wana wa Israel kutoka utumwani misri wakiongozwa na Musa kuelekea nchi ya ahadi ni hadithi ambayo huwa inanifanyaga nicheke sana kwa sababu safari ilikuwa na matukio ya kufurahisha.
 
Mkuu asante kwa andiko hili nami ni mmoja wa ambao hatukuliona mapema..

Nina swali..
Tafsiri ya majina ya Jesus na God katika lugha za makabila yetu ilifanywa na nani? Tukianza na Jesus kuwa ndio Yesu na God ndio Mungu...
 
Hapo kwenye kuogea chumvi au maji ya baharini naweka imani yangu huko maana hata kwenye biblia ipo.

Nitaenda baharini kutoa mikosi na gundu zinazoniandama
 
Mkuu nimetafuta sana kwenye Bible naomba kama una kumbukumbu nikumbushe hilo andiko
Ezekieli : 43
24 Nawe utawaleta karibu mbele za BWANA, na makuhani watamwaga chumvi juu yao, nao watawatoa wawe sadaka za kuteketezwa kwa BWANA.
 
Mkuu nimetafuta sana kwenye Bible naomba kama una kumbukumbu nikumbushe hilo andiko
2 wafalme : 2
21 Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, BWANA asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza.
 
Mkuu nimetafuta sana kwenye Bible naomba kama una kumbukumbu nikumbushe hilo andiko
Natumaini umeelewa kwanini RC tunatumia chumvi

Mambo ya walawi : 2
13 Tena, kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia chumvi; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la Mungu wako; utatoa chumvi pamoja na matoleo yako yote.
 
Natumaini umeelewa kwanini RC tunatumia chumvi

Mambo ya walawi : 2
13 Tena, kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia chumvi; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la Mungu wako; utatoa chumvi pamoja na matoleo yako yote.
Nimeelewa mkuu,asante sana
 
Hapa sijakuelewa mkuu.. please maelezo zaidi
Oooh mkuu, nilivyopitia uzi wako unaoelezea jinsi introverts wanavyoteseka kuchangamana na jamii,..., naam niliyopitia ufafanuzi wako, nilikuelewa mno. Kwa sababu kwa muda mrefu nilikuwa sijitambui, ila baada ya kusoma ule Uzi, nilijitambua kwa kiasi kikubwa. Naam nikifikiria, naifurahia mno hali niliyonayo, hivyo nikifanya imagination... Ya baadhi ya tabia za introverts, naam nikiangalia na mambo unayoandika jinsi yalivyoshiba ingawa sijayafuatilia sana, walakini nimeamua kwamba, miezi michache ijayo nitafuatilia nyuzi zako za nyuma, maana najua Nina mengi ya kujifunza, kwa kuwa ndiyo kwanza nipo kwenye hatua za awali katika safari hii ya kujifunza mambo haya.

Hivyo, Mimi kuandika kwa kifupi hivyo, nilimaanisha kwamba; umejawaa na maarifa na maneno ya fahamu moyoni mwako, naam yakini yaweza kuwa tofauti na unavyoonekana. Kama wanenavyo "Quite(introverts) people have the loudest minds", naam watu wenye mengi mioyoni mwao kuliko wanavyoonekana.

Hongera sana mkuu.
 
2 wafalme : 2
21 Akatoka akaenda mpaka chemchemi ya maji, akatupa ile chumvi humo ndani, akasema, BWANA asema hivi, Nimeyaponya maji haya; hakutatoka huko tena kufa wala kuzaa mapooza.
Mkuu, hivi naweza kujifunza habari za Mungu, nikaelewa kwa kina na kuwa karibu naye bila kufundishwa na watu wenye mwili?
 
Gratitude mate...nipo tofauti na nionekanavyo. Knowledge is my my hobby and all thanks to the Almighty who made me to be this way ✌️

Ukitaka kuanza kuzifuatilia utasema nikuelekeze yakuanza nayo. Maana nyingine zipo jukwaa la dini sijui Kama una Access
 
Mkuu asante kwa andiko hili nami ni mmoja wa ambao hatukuliona mapema..

Nina swali..
Tafsiri ya majina ya Jesus na God katika lugha za makabila yetu ilifanywa na nani? Tukianza na Jesus kuwa ndio Yesu na God ndio Mungu...
Kwanza upande wa Yesu kwenye makabila yetu sidhani kama kuna kabila lenye kutumia jina lingine kuwakilisha Yesu. Makabila Mengi niliyowahi kufahamu wanamuita Yesu kama Yesu....nitaeleza mbeleni Why.

Makabila Mengi Tanzania jina la Mungu linatamkwa tofauti tofauti na kila kabila. Japo kwasababu ni kibantu kunakua kuna mzizi unaofanana kutoka kwenye kabila moja na lingine nadhani makabila mengi ambayo ni wabantu jina Mungu wanatumia mzizi wa -MANA-(kama sijakosea) Je mkuu kabila lenu mnamwitaje Mungu?

Sababu ni kwamba kabla ya ukoloni kila jamii ilikua na taratibu zake za kuabudu hapa tanzani kutokana na mila na tamaduni za kabila husika. Hivyo basi wamisionari walivyokuja kumtangaza God makabila mengi walilichukua jina la God na kulibadiri kutokana na wao kwenye kabila lao walikua waniita vipi Kitu wanachoabudu wakiwa wanatambika. Kama ni msufi ndio uliabudiwa walikua wanauita Imana basi GOD nae wakamuita Imana.. nk nk.

Lakini pia ukumbuke kua Maeneo mengi TZani jamii ziliunganishwa kwa kiswahili so kitu kilichokua kinaabudiwa haijalishi ni mti,msitu, mto nk kwa pamoja vitu hivyo wiviita Mungu kwa kiswahili.

Sasa upande wa Yesu anaitwa hivyo hivyo Yesu kwasababu kwenye dini zao za asili kulikua hakuna utatu mtakatifu..hivyo Yesu lilikua neno jipya.

Kama bado una swali Usiache kuuliza
 
Nikupongeze kwa kupenda kufuatilia wanafalsafa..mimi pia ni mgonjwa sana saikolojia na falsafa. Yaani napenda sana tukae na mtu tuanze kudadavua falsafa za mtu mmoja mmoja. Hebu jaribu kusoma falsafa za Stoic kutoka kwa mwanafalsafa Zeno wa Citium...Utakutana na mafunzo fulani hivi ya masha anatamani tuishi. Kama tungeyaishi basi dunia isingekua uwanja wa fujo wa kuhombea mali tutakazo ziacha...BTW wanafalsafa ambao nimependa wawe Mentor wagu ni Thomas Aquinas, Paulo,Carl max, Socrates,Yesu,Nyerere, Fransisco wa Asizi, Leonard da vinci.

Turudi kwenye mada yetu!!
Kwanza kabisa Surrender your Ego...ukitaa kujifunza habari za Mungu ni maswala ya imani. Imani haithibitishwi kwa Sayansi wala historia. Imani ni imani.

Hizi ni nyakati za kusikia na kuamini zilikuwepo nyakati za kuona na kuamini bahati mbaya hatujaziishi..so ukitaa kujifunza imani ya Mungu acha kila unachodhani unafahamu kisha mruhusu yule roho aliyeko ndani yako afanye kazi

Ni kweli kuna sehemu zingine biblia inachekesha kweli inakuacha maswali kibaoo
 
Ndgu yangu nimesoma vizuri uzi wako,
Na umesema nyumbani kwako Biblia takatifu unayo,
Jaribu kutenga muda wako uisome vizuri neno kwa neno mstari kwa mstari,
Mungu ana makusudi na wewe kuna jambo anahitaji akushirikishe kiroho na bado hujachelewa,
 
Ndgu yangu nimesoma vizuri uzi wako,
Na umesema nyumbani kwako Biblia takatifu unayo,
Jaribu kutenga muda wako uisome vizuri neno kwa neno mstari kwa mstari,
Mungu ana makusudi na wewe kuna jambo anahitaji akushirikishe kiroho na bado hujachelewa,
Mkuu ujumbe huu unanihusu mimi???
Naomba uongeze maelezo kama unanihusu labda ndio Mungu anakutumia ili nifahamu jambo analotaka kunsihirikisha
 

"Hizi ni nyakati za kusikia na kuamini,zilikuwepo nyakati za kuona na kuamini ila sisi hatujaziishi" 😁😁😁

Hii sentensi imenifanya nicheke tu.

Mkuu Umenena vyema kuwa nikitaka kujifunza mambo ya kiroho inabidi niache kila kitu ninachodhani najua alafu nimruhusu roho aliyeko ndani yangu atende kazi, swali langu lipo kwenye huyu aliyeko ndani yangu, Je nitampaje go ahead atende kazi, yani nitawasiliana nae vipi kwamba bhan nimesalimu amri sasahivi niongoze wewe ili niijue kweli ni ipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…