Je, unafahamu kwanini maisha yako yameandamwa na mikosi pamoja na Mambo mabaya?

Je, unafahamu kwanini maisha yako yameandamwa na mikosi pamoja na Mambo mabaya?

Kila mwanadamu ana kitu Fulani kilchopo ndani ya kichwa chake kitaalamu wanaita Internal Monologue au self-talk au inner voice. Hii ni sauti Fulani ipo ndani ya vichwa vyetu hua ni sauti ndogo tena ya upole sana, Sauti hii imeundwa na kitu kinachoitwa Self –Concept au sense of self. Self-Concept ni ile hatua ambapo mtu anaweza kufafanua kua yeye ni nani hasa au ni hali ambapo mtu anakua ameweza kujitambua . Self-Concept imeundwa na Self-Schemas, past self (Kutambua wapi ulipotoka) present self (Kutambua wapi ulipo) na Future selves (Kutambua wapi utakapokua baada ya hapa ulipo).

Self-schemas: katika saikolojia na sayansi ya utambuzi (Cognitive science) inasema kwamba schemas huelezea muundo wa mawazo au tabia ambazo hupanga aina za taarifa na uhusiano kati ya taarifa hizo. Lakini inaelezwa pia kwamba ni muundo wa akili kupokea taarifa na kuzichambua..taarifa hizo ndio huleta maarifa ya kumuwezesha mtu kutambua self-concept.
Kama tulivyoona hapo juu kwamaba inavoice imeundwa na self-concept, self-concept ndio hupelekea mtu kuweza kujitambua kwamba yeye ni nani, hivyo basi vyote hivi humuweka mwanadamu aweze kujitambua na kujielewa.

Kusudi (Purpose)
Kila mwanadamu ameumbwa kwa “Kusudi/Purpose” Fulani, Hili ni lengo kuu lililofanya tuumbwe na kuwekwa hapa duniani, ukifungua kitabu cha Katekismu katoliki swali la kwanza kukutana nalo linauliza kwanini Mungu kaniumba? Mungu katumba ili tumwabudu na kumtumikia. Hilo ndio kusudi au lengo kuu lililofanya sisi tuumbwe na kuwekwa hapa duniani, si vinginevyo! Lakini mbali na hilo kusudi kuu pia kuna kusudi ndogo ambayo kila mtu kapewa tofauti na mwingine, Lakini pia unaweza kuta kusudi lako linafanana na mwingine.

Wakati mungu anamuumba mwanadamu mwili wa mwanadamu ulikua ni kasha tu au kama mdoli au kipande cha mgomba tu ambao haujui chochote, Mungu alimuwekea mwanadamu pumzi yake ya uhai (Roho) akapata uhia na utambuzi, kama pumzi hiyo ilitoka kwa Mungu basi nayo ina uungu ndani yake. Roho imeundwa na Mind,intellect na Impression..subconcious mind iliyopo ndani ya Mind ndio sehemu kuu ya Roho, Subconcius Mind ndio data bank yako yaani inahifadhi taarifa zako zote,imani yako,Ujuzi na utambuzi wako,kumbu kumbu zako lakini kubwa zaidi ndio sehemu inayohusika na mfumo wa kukuongoza wewe. Huko juu tumeona kwamba kila mtu ana sauti Fulani iliyopo ndani yake, yaani ndani ya Mind yake…Sauti hiyo imeundwa na self-Concept ambayo inakuwezesha kutambua wewe ni nani lakini pia tumeona kwamba Subconcious Mind ndio inahifadhi kila kitu kwa mantiki hiyo Tunaweza kusema kwamba Sauti ile ndogo ambayo tunaisikia ndani yetu inatoka ndani ya Subconscious mind ambayo ipo ndani ya Roho. Roho imewekwa na Mungu hivyo ile sauti ndogo ndio wewe (Who you are) maana muda wote kama umeisikiliza kwa makini hua inakuambia mambo mema tu, muda mwingi hukushauri na kukumbusha ulipotoka, ulipo na unakoelekea. Muda mwingine hukuonya kwa kukukumbusha adhabu ambazo unaweza kuzipata kama utaacha kuishi ndani ya kusudi kuu kwa kuhitimisha sasa tunaweza kusema kwamba ile sauti ndogo inatoka ndani ya Roho mtakatifu-Mungu aliye ndani yako.

Sauti ndogo ile ndio hutuelezea kusudi la maisha yetu hapa duniani, bahati mbaya kwa ukiburi na kujifanya tuko wabize sana maishani hua hatuna muda wa Kusikiliza sauti ndogo iliyo nadani yetu ili tujue kusudi letu…. Kua makini Yule mwovu hua anatuma Virus kushambulia server zako rohoni ili kuinterupt request zote zinazotakiwa kua processed mwisho unajikuta unamsikiliza yeye. Mwovu kautawala mwili anatumia mwili wako kuivamila roho yako. Ndio maana unakuta sauti ndogo ile inataka ufanye kitu Fulani chema, kumbuka yeneyewe haiwezi tenda inategemea mwili, bahati mbaya roho inakuta Shetani kashafunga Firewall na Virus kibao kwenye mwili, mwili unakataa request za kutekeleza yale mema roho inayotaka unakua unaprocess request za kwenda kufanya yale mwili upendayo kama starehe. Cha kufanya ni kuinstall Antivirus za maombi na matumaini kwa muumba wako

Unaishi ndani ya kusudi/mpango wa Mungu?
Mfumo wa maisha yetu ya dunia ya sasa ukiangalia unaweza kujiuliza maswali mengi sana kuhusu jinsi tunavyoishi. Ukichunguza kwa makini utaona tunaishi katika mfumo Fulani ambao watu walikaa wakaunda. Kwamba mtoto akizaliwa akue aende shule, akimaliza shule atafute kazi au kuoa kisha aanzishe familia yake na kuihudumia kwa kujitafutia kipato. Lakini je hivyo ndivyo muumba aliumba tuishi? Unaweza kuona mtu maisha yake yote anayatumia kwenye mahangaiko ya kutafuta maisha, je tulikuja duniani kutafuta maisha? Jibu ni NO. hatukuja kutafuta pesa wala utajiri duniani, hatukuja kutembea hapa duniani kuna kitu Fulani tumeletwa kuja kukifanya na si kutafuta maisha wala utajiri.

Inawezekana sisi waafrika ndio tunaongoza kutokuishi ndani ya kusudi letu tuliloumbiwa kutokana na mfumo mgumu wa maisha yetu, lakini kwa kiasi Fulani tunaishi ndani ya mpango wa Mungu alivyotaka. Tunaishi kijamii baina ya mtu na mtu, shida na raha tunachangia majirani. Lakini kusudi la kila mmoja mmoja mmoja hatuliishi. Mtu anaamka saa 10 usiku kila siku kwenda kujitafutia kipato, anayatumia maisha yake yote kutafuta pesa za kujikimu. Mwisho anafika uzeeni hajapata alichosumbukia maisha yake yote, anakufa hajui kama maisha yana maana kubwa zaidi ya kutafuta pesa.
Ukipata muda kaa jichunguze mfumo mzima wa maisha yako kuanzia asubuhi mpaka usiku, toka ulipozaliwa hadi leo ulipo. Je unavyoishi ndivyo ilitakiwa iwe? Je ni kweli ulikuja

Je nitalifahamu vipi kusudi langu..?
Kwanza kabisa ili ujue kusudi lako inabidi uelewe kwamba wewe ni nani? Ulitoka wapi? Upo wapi na kwa sababu ipi? Na nitaelekea wapi? Majibu ya maswali haya yote yanajibiwa kwamba “kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vionekanovyo na visivyonekana na vyote viliumbwa kwa kusudi yake na kwa ajili yake” Wakolosai 1:16
Kama unataka kujua kwanini upo duniani hapa inabidi uanze kumkiri Mungu muumba wako kua ndie aliyekuumba,ulizaliwa kwa kusidi lake wazazi wako hawakupanga wewe uzaliwe ni yeye ndio aliyepanga uzaliwe. Hukutokea duniani hapa bahati mbaya, huwezi kulifahamu au kutambua kusudi la maisha yako kama hutoanza Kumtanguliza muunmba wako kukuonyesha kusudi alilokuumbia. Kila mtu kaumbwa na kusudi lake hapa duniani bahati mbaya wengi hatuishi ndani ya kusudi letu maana hatumuweki mbele Muumba wetu atujulishe kusudi letu, Lakini pia kwa hali ya ajabu kabisa usishangae kusudi lako likawa lipo tofauti na wengine kwa kiasi Fulani..Kuna watu wameletwa hapa duniani wao kusudi lao kuu ni kusaidia watu wengine wanatimiza makusudi yao. Kwa mfano Yohana mbatizaji alikuja duniani kwa ajili ya kukahakikisha kusudi la Yesu Kristo linatimia kwa kumuandalia njia. Pia mitume wa Kristo kusudi lao ilikua kusambaza kusudi la Kristo kwa walimwengu wote. Mungu ndie aliyekuumb naye ndio anayejua kusudi lako ni lipi, mwambie akuonyeshe kusudi lako.

Maana ya maisha yako hapa duniani utaijua kama utalijua kusudi la maisha yako, kusudi la maisha yako linatoka kwa Mungu. Muombe Mungu akujulishe kusudi lako atakueleza kwa kupitia ile sauti ndogo iliyopo ndani ya roho yako. Chukua muda wako sikiliza sauti ndogo iliyo ndani yako inakueleza nini, siku zote kusudi lako hua ni jema machoni pa watu wanaokuzunguka na mbele za Mungu muumba wako. Sikiliza ile sauti inakuambia ufanye nini, kitu chema..anza kukiishi.Binafsi nilikua nikiona watu wanaoomba barabarani naogopa kukutana nao pengine nawakwepa, nikiona watu wanashida roho inaniuma sana ndio nikajua roho yangu inataka nifanye nini kuhusu watu wenye shida.I pledged and dedicated my life to those who need help, hatakama itakost uhai. Bahati mbaya bado sijafika hatua nayotaka hasa.moja ya kitu nifanyacho ni kushare na wenzangu chochote kile kilichopo ndani ya akili yangu-for free.

Nyie hamuwaonei wivu baadhi ya watu waliosihi ndani ya kusudi lao, wameacha alama duniani mpaka leo tunawakumbuka. Namuonea wivu sana Nyerere,yesu,newton,Da’Vinci,Mother Teresa,Paulo,St.stephano nk nk. Natamani siku moja niishi ndani ya kusudi langu kwa asilima japo 60% hata nikifa niwe nimekufa kihalali. Maana dunia na wakazi wake watakua wamefaidika uwepo wangu hapa duniani.

“Mungu anasema Nilikuumba katika fikra zangu kwanza kabla ya kukuweka tumboni mwa mama yako, nilikujali toka siku unazaliwa. Nitakujali ukiwa kijana mpaka ukiwa mzee na siku zote za maisha yako. Maana mimi ndio nilikuumba na nitakujali”
Ahadi za Mungu ni timilifu, akisema anatenda. Japo tunamkosea pakubwaaa ila anatujalia mengi sana tuliyomuomba na mabayo hatujamuomba. Usiokope kumuuomba muumba wako akujuze kusudi lako, yeye ni muumba wako na baba yako, Onyesha utii japo kidogo juu yake uytaaona neema nyingi maishani mwako. Hukuumbwa uje kubeti,kuibia watu, kua karaha na kikwazo kwa wenzako, kuja kuua watu, kuja kuonyesha umahiri wako wa kua na wanawake/wanaume wengi kwa wakati mmoja.
Miasha ni mafupi mno, ukiyaangalia unaweza kuona hayana maana tumekuja kupoteza muda tu hapa duniani bora tusingezaliwa. Huwezi kuona maana ya maisha yako kama hujajitambua. Ukijitambua utajua kusudi la maisha yako na maisha yako utayaona yana maana kubwa. Hivyo basi tusikilize sauti ndongo iliyo rohoni mwetu inayotoka kwa Mungu inatuambia kusudi jema la maisha yetu, tukishajua kusudi letu tutajitambua na maisha yetu yatakua yenye maana kubwa hapa duniani.
Be Humble,Be kind. Life is too short and full of surprises.
-The End...
{comment,like n share}
Purpose1-1.jpg
~Da'Vinci

Mkuu nashukuru kwa udadavuzi wako, ingawa umeongea mambo mengi mno kwa wakati mmoja kiasi kwamba ni machache tu nimeyaelewa.

And by the way inaonekana mambo unayonambia aither yapo katika ama mwisho, kwa sababu kwa point zako inaonesha dhahiri kabisa huenda kuna mambo ya mwanzo kabisa napaswa kuyajua kama msingi kabla hatujaanza kuipandisha nyumba juu.

Ni jambo zuri umenambia kwamba inabidi nianzie kwenye kujiuliza mimi nani, natoka wapi na kwenda wapi, kwanini naishi hapa duniani e.t.c.

I think I need to format and restore my life first, that's the only way to copy with your ideas.
 
SALUTE

Maisha ni safari ndefu yenye mabonde na mashimo tu Yenye matumaini tu huku raha zikiwa chache mateso na taabu yamejaa! Kuna mambo yanaweza au yanatokea kwenye maisha yako hadi ukabaki unashanga. Yaani jambo fulani baya au zuri linakufata wewe tu kila siku hadi unajiuliza Why me?

Mfano uko mtaani kila tukio baya likitokea basi unahusishwa, unaweza kuta yaani wewe kila mwanaume anayekufata ni ni wa aina fulani usiyoipenda, labda mwizi, muhuni, mweusi, mfupi, mjinga nk.

Kwa upande wa wanaume nadhani hii inawatokea sana utasikia kabisa mtu anasema "Aisee mimi nina bahati na wanawake weupe/walimu/manesi/wanawake washamba nk nk. Yote haya ni maisha yetu ya kila siku ya sisi wanadamu, wengi hatuelewi kwanini hii inatokea hivi lakini ni vitu ambavyo vinahusiana na mambo ya kiroha na Kiasili (nature).

Lakini hadi mtu yanamtokea mambo haya bila yeye mwenyewe kujua hua nini kinafanyika? Hapa nitaenda kuelezea zaidi jinsi mambo mabaya yanavyokua yanaambatana nasi pasipo sie kupenda. Ili nieleweke vizuri nitatumia terminologies za kwenye mambo ya teknoloji.

Kwenye Computer Processors kuna kitu kinaitwa Caches, hii ni sehemu ambapo ukifinya kitu fulani kwenye computer basi kile kitu kinahifadhiwa huko ndani ili ukitaka kukitumia tena basi kinafanyiwa kazi kwa haraka zaidi. Pia kuna kitu kingine kinaitwa HTTP Cookie hizi zinafahamika pia kama Web cookie, browser cookie, internet cookie. Hizi ni data ndogondogo ambazo huchukuliwa kwenye web, internet, browser n.k na kuhifadhiwa kwenye Computer wakati mtumiaji yuko anaperuzi. Kazi yake ni kurekodi mambo yote ambayo mtumiaji (user) anayafanya kwenye internet mfano. Zinarekodi Password, page ipi umetembelea, Majina, nk. Hayo yote yanakusaidia wewe mtumiaji wa internet utakapotaka kuperuzi mitandaoni basi iwe rahisi kutumia.

Kwa upande wa Google huko wao wana project yao wanaita Hummingbird, hii ni alogarithm ambayo inafanya kazi ya kumwezesha mtumiaji wa huduma za google (Hasa YouTube na Google as Search engine) kupata huduma hizo kwa urahisi na kwa haraka...wanasema Google inakujua kuliko mama yako mzazi, Ni kweli.

Unapotafuta kitu Google chochote Hummingbird inarekodi kila kitu baadae ukitaka kuitumia tena inakuletea vitu kama vile ulivyotafuta mwanzo. Ndio maana ukitafuta kitu fulani YouTube ukaangalia ukamaliza labda ukatoka huko baadae ukirudi tena youtube utakuta video mbalimbali zinazoshabihiana na zile ulizoangalia mwanzo.

Yes kwakua Google wanakua washajua ni vitu gani unapendelea ili usisumbuke kuandika wanakuletea hapo kwenye homepage as suggestion posts.

Sasa turudi kwenye mada kuu, mada yetu inahusu kwanini mambo fulani (upande wa ubaya) yanaweza kua yanakufata wewe tu!. Kwenye moja ya post zangu zilizopita nilieleza kua Roho ya binaadamu ndio inabeba taarifa ya kila kitu kukuhusu wewe, so nikachukulia kwamba Roho ya binaadamu ni kama BIOS CHIP (ROM) iliyopo kwenye Motherboard ya Computer halafu mwili wetu ni kama kasha la nje la Computer. Unapokufa Mungu anachomoa Bios chip tu iliyo na taarifa zako!

Leo twende tofati kidogo, tuchukulie Roho ni HummingBird au Cookie au Cache japo mimi nitapendelea tuichukulie kama HummingBird. Roho (Soul) imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Mind, Intellect na Impression. Mind ndio inahusika kwenye kufikiria, hasa kwenye kutambua lipi baya na lipi zuri. Kwenye Mind kuna kitu kinaitwa Subconcious Mind hii ndio sehemu kuu ya Roho (Soul) ambayo kazi yake ni kurekodi shughuli zetu za kila siku ziwe za kimwili au kiroho.

Sasa kwenye maisha halisi ipo hivi, unapofanya kitu fulani roho(subconcious mind) yako inarekodi. Labda siku moja uliwahi kuwa na mahusiano/ Kutongozwa/za na mwanaume au mwanamke ambao kwako wewe ambae wewe unaona hakufai, roho yako inahifadhi taarifa kwamba uko interested na watu wa namna hiyo. Au siku moja imetokea umeiba kitu roho itahifadhi taarifa. Siku umeenda jela basi roho itasevu. siku ukitembea na mtu aliekuzidi umri roho itahifadhi nk. Kwa upande wa Psychology roho tunasema kwamba Roho (Subconcious mind) inafanya kazi kwa ukaribu zaidi au inashirikiana katika kutenda kazi na Nature.

Kwa hiyo sasa unapofanya kitu fulani roho yako ikakihifadhi, baadae Roho itawasiliana na Nature kwamba unapenda vitu fulani hivyo nature itakua inakuletea vitu hivyo mara kwa mara. Hiki kitendo nature kuwasiliana na roho kisha kukuletea yale usiyoyapenda ndio tunaita MKOSI.

Mfano: Mbaba aliyekuzidi umri kakutongoza wewe kwa kua unashida zako ukamkubalia roho inahifadhi. Baadae itawasiliana na nature kua fulani anapenda wanaume wa umri fulani kisha nature itakuletea mwingine kama suggestion. ukikubali tena na tena basi ndio itakua tabia yako kabisa. Hii ipo kwa kila kitu iwe kibaya au kizuri.

Je, tufanyaje ili kuepuka mambo mabaya yanayotuandama?

Kwenye Computer ili kuziepuka cookies baada ya kutumaliza kuperuza mitandaoni inatakiwa uende upande wa setting kisha chagua Clear Cookies ili kuondoa kumbukumbu zote zote za kuperuzi siku hiyo. Kwa upande wa Google kubaki na taarifa zako. Huwa tunashauri kutumia Search Engine ya Duck Duck Go, Hii web ni nzuri zaidi maana hua ina clear taarifa zako zote baada ya kumaliza kuitumia..ina mengi mazuri ya kiusalama hasa kwenye taarifa za utumiaji wa kila siku (Browsing History). Jamani siipigii debe hii web, ni kuwaweka sawa tu na mada yetu hii. Sasa kuclear cookies au kuondoa mikosi kwenye maisha kuna mambo kadha ambayo tutayafanya.

Hivi ulishawahi kujiuliza kwanini mtu akitoka jela au mahabusu (kituoni) zile nguo alizoenda nazo huwa zinatupwa, pia itabidi aoge kabisa kabla hajaingia ndani, wengine huenda mbali zaidi kwa kuogeshwa dawa za mitishamba ili kuondoa mikosi. Hapo sasa ndio kitendo cha kuclearcookies. Wanafuta taarifa zote zilizomo kwenye roho zihusuzo jela. ni mfano tu huu ila hizi hapa chini ni njia zangu amabazo mimi kwa ufahamu wangu nadhani tukizitumia tutaweza kuondoa mshikamano wa mambo mabaya kwenye maisha yetu (Mikosi)
  • Kujua Preferences zako
Ili kuondoa kushikamana na mambo mabaya maishani inabidi mtu ujitambue wewe binafsi unapenda nini hasa. Je unapenda Kuwa mwema? Unapenda kuiba?unapenda mwanamke wa namna fulani?unapenda mwanaume wa aina fulani nk nk.. ukishajua ukipendacho basi futa yale uyapendayo nawe yatakua yanashikamana nawe.

Hatima yako ipo mikononi mwako, usiache Nature ikuchagulie Hatima yako kwa vitu ambavyo hupendi. Hivyo basi tukisha tambua yale tunayoyapenda na kuayafuata tutaifanya nature ituletee yale pia mabayo tunayapenda.Hapo tutakua tumekwepa kufuatwa na mabaya.
  • Kujiondoa kwenye mikosi. (Kuclear Cookies maishani)
Jamani maishani huwezi kua smart muda wote Nature always win!!!, ipo siku utanasa tu. Sasa hapa labda tuseme umeshavuruga mambo maisha yamejaa mikosi na mabaya yanakuandama. Hapa sasa tutaangalia jinsi ya kuondoa hayo mambo.

1. Tutumie Chumvi na maji, Usishangae sio uganga wala uchawi. Chumvi ni dawa nzuri sana kwa binaadamu nadhani member wengi wameielezea sana humu, sina haja ya kueleza zaidi. Cha msingi chukua chumvi ile ghafi ambayo haijapita kiwandani changanya na maji kisha nuia unavyotaka kisha oga. Hata nabii Ezra aliambiwa na Mungu achanganye maji naNchumvi kisha kuwapatia wana wa Israel wajitakase, ndio maana kwetu RC kuna maji ya baraka yenye Chumvi.

Kama utakua karibu na bahari itapendeza kabisa wewe ni kwenda na kujitupa tu majini maana huko chumvi kibao

2. Mshirikishe Mungu unayemuamini hata kama ni mzimu, hapo inabidi uombe toba kabisa, mweleze mapungufu yako na mahitaji yako kua unataka kuwa mtu mpya, mambo mabaya hutaki kushirikiana nayo. Piga sala sana na ibada kadri uwezavyo. Almighty atakuelewa na kukusafisha uwe mpya.

Maisha bana is all about determing yourself akina mshana jr na wenzake, manabii na mashehe Sharifu wanatuibia tu kwa kuwa wanajua elimu tunayo kidogo, hatujitambui. Tujifunzeni kujitambua hatutasubiria kuombewa na nabii. Wao wanacheza na Psychology ambapo huko watu wengi ni watupu sa tunapigwa tuuu!!!

NOTE. Ahsante Mungu kwa yote uliyonijalia hasi umeniwezesha kuandika mada hii.
End....

Kama umepende Like, Comment then share kwa wenzio.

~Da'Vinci
el maestro.
Huu uzi sijui ulinipita wapi?
Nways nimeuelewa vilivyo


Sent from my 502SO using JamiiForums mobile app
 
Dah nimecheka kishenzi[emoji23][emoji23]yani mwandika uzi ye mwenyewe haelewi kaandika nini mimi ninani mpaka nielewe[emoji23][emoji23]
 
Be careful with what you think because Thought shape Reality. You're what you think and you will get what you think. What you seek is what you will get....Be postive no matter how physical world treat you.. You're only weak outside/physically. But inside you're so powerful spiritually. Draw out your spiritual strength to face the physical world.
You're inner strength start with postive thought.

Trust your Inner you!!

Coach Slamah Hamad mchango wako muhimu kiongozi [emoji3577]
I am greatly blessed by your wisdom. May God give you a long life[emoji2969]
 
Unaposema watu wenye mwili unamaanisha nini?? Ulitaka ufundishwe na watu gani??
Ooh namaanisha watu ninaowaona mfano wachungaji, padri, au wanaoitwa manabii nk. Kwa sababu wengi wao Mimi siwaamini, nabaki na maswali mengi kichwani, ambayo nikimuuliza kila mmoja anajibu kulingana na level ya ufahamu wake.

Lakini nikifikiria Yusufu kule Misri alikuwa kijana tu, ila hakumuacha Mungu, na in kama vile kule hakukuwa na walimu au manabii wa kumfundisha, Ila bado Mungu alikuwa pamoja naye. Akina Danieli, Mishaeli, Hanania na Azaria walivyokuwa Babeli bila shaka pia walikuwa vijaba Ila walikuwa na elimu ya kina kuhusu mambo ya kiroho. Je, walifundishwa na nani?

Hivyo swali langu lililenga kutaka kujua kama naweza kujufunza mwenyewe mambo ya Mungu kwa kusoma vitabu vya dini, nikaelewa kwa kina kabisa bila kufundishwa na hao waluosomea vyuoni?
 
Gratitude mate...nipo tofauti na nionekanavyo. Knowledge is my my hobby and all thanks to the Almighty who made me to be this way [emoji3577]

Ukitaka kuanza kuzifuatilia utasema nikuelekeze yakuanza nayo. Maana nyingine zipo jukwaa la dini sijui Kama una Access
Mkuu nashukuru sana kwa kujali, walakini sina access na hilo jukwaa (la dini).
 
Tuanzie hapa....
...

Salute comrades
NB: bandiko hili nimetumia maandiko ya biblia hata kama unaona haikuhusu nakusihi endelea kusoma unaweza pata kitu.

Katika dunia yetu hii tumeona ni sentensi ya maneno kadhaa tu ndio imeubadirisha huu ulimwengu wetu na kuufanya uendelee. Unaweza kuona sentensi kama vile Newton’s laws of motion zilivyochangia maandeleo ya dunia yetu karibia asilimmia 50 ya maendeleo ya ulimwengu yanaweza kuwa yameletwa na hizo sentesi (laws) tatu za mwanasayansi Issac Neawton kiteknolojia, kiuchumi, pia katika mafunzo ya kiroho hizo laws tatu zinafanya kazi. Au unaweza kuona formula ya E= mc2 ya mwanasayansi Albert Einstein ilivyopelekea mauaji ya mamilioni ya watu huko Hiroshima na Nagasaki Japan, aidha mwanasayansi toka ugiriki Archimedes sentsnsi yake kuhusu kuzama na kuelea kwa kitu ilivyoleta maendeleo makubwa kwenye usafiri wa maji nk. Hivyo unaweza kuona kua hua ni sentensi au maneno ya mtu ndio yameleta makubwa hapa duniani baada ya kuchambuliwa na kufanyiwa kazi.

Swali alilouzaYesu wanafunzi wake linavyowasha taa ya kujitambua kichwani mwa binaadamu.

Luka 9:18-21 "Yesu aliwauliza wanafunzi wake kua je makutano hao wanasema ya kua mimi ni nani? Wanafunzi wake wakajibu yohana mbatizaji wengine wanasema wewe ni Eliya lakini petro akamjibu kua Ndiwe Kristo wa Mungu".

lengo la mada yangu ni kufundisha juu ya mtu kujitambua yeye ni nani (to know your identity), katika swali hilo alilouuliza yesu unaweza kuona ni swali rahisi tu lakini likichambuliwa limebeba ufunguo wa kufungua akili ya mtu kujitambua.
Maneno ya muhimu kwenye swali hiyo ni watu wanasema mimi kua ni nani? Yesu alipouliza swali hilo sio kwamba alikua anataka wamwambie jina lake hasha alitaka afahamu je watu wanamjua yeye ni nani, ndipo petro anamjibu kua ni Kristo wa Mungu. Je nawe ushajiuliza wewe ni nani na watu wanasema wewe ni nani? Twende nikupatie majibu.

Mimi ni nani?
Hapo ulipo anza kujiuliza maswali haya na ujijibu mwenyewe,
Je hivi nilivyo ndivyo natakiwa niwe? Yaani ukijiangalia tabia zako, matendo yako ndivyo unatakiwa uwe? Jibu unalo.

Watu wanasema mimi ni nani?
Ulishwahi kuona mtu Fulani akitaka kumchumbia binti Fulani anaanza kwanza kuulizia kwa watu wanaomfahamu kama vile majirani, mrafiki ni kwasababu watu wa pembeni wanakufahamu zaidi, je leo hii wewe memba mwenzangu wa jf mtu akiuyliza jirani zako kua wewe ni nani atajibu vipi? Je unatabia nzuri, unatabia mbaya, mpole, una hekima, mwizi n.k. jibu unalo mwenyewe.

Rafiki na ndugu/ wazazi wangu wanasema mimi ni nani?
Je mtu akija leo hii kwenu akauliza wazaizi wako nao wakasema ukweli kuhusu wewe bila kuficha kitu watasema wewe uko vipi, kuna watu wakiwa mbele za watu wanaficha tabia zao mbaya wakiwa mbali na kwao lakini wakiwa kwao wanatabia chafu. Mfano unaweza kuona msichana akiwa mbele za watu anakula chakula kidogo mno lakini akiwa kwao hadi anagombania chakula na wadogo zake.

Mungu anasema mimi ni nani?
Hivi ulishawahi jiuliza unahisi Mungu wako anafahamu wewe ni nani, je wewe ni mpole, mwenye dhambi, mchaji, mwenye hekima n.k. kumbuka kabla ya kutungwa kwenye mamba ya mama yako ulianza kutungwa kwenye fikra za Mungu kwahiyo anakufahamu zaidi unavyojifahamu. jibu unalo mwenyewe.

Kwanini nipo hapa duniani?
Ushajiuliza kwanini upo duniani nab ado upo hai na mzima wa afya wakati kila siku watu wanafariki na wengine ni wagonjwa hawajiwezi. Upo hapa duniani tumtumikie mungu na kumuabudu. Utafahamu kusudi lako (purpose) mungu kukuumba na kukuweka hapa duniani kwa kumcha na kumuomba Mungu. Zaburi 13.9, muhubiri 7:13

Nilitoka wapi?
Jiullize mimi nilitoka wapi? binnadam origin yake imegawanyika sehemu mbili. Kwanza mwanadamu anatoka kwa Mungu yaani kuumbwa toka kwenye fikra za Mungu hadi kuwekwa kwenye tumbo la mama yake. Pili familia anayotokea ndio chimbuko lake la pili hata akijitambulisha atasema anatoka familia Fulani lakini kiuhalisia anatoka kwa MUNGU. Mwanzo 1-1, Yohana 1:1-5

Je nifanye nini?
Baada ya kujiuliza maswali hayo hapo juu na kuona udhaifu wako ulipo juu ya kujitambua basi fanya haya ili kuwasha taa ya ufahamu ndani ya ubongo wako. Mwalimu wangu alikua ananiambia batani ya kuwasha taa ya kujitambua ndani ya ubongo unayo mikononi mwako uamuzi ni wako kuwasha upate mwanga au uendelee kukaa giza.
Fanya haya :-
Mche na kumuomba mungu
Jiongezee maarifa kwa kusoma vitu mbalimbali kila siku
Kusudia mwenyewe kutaka kujitambua
Tengeneza utofauti wako na watu wengine
Ongeza thamani ya kile unachokifanya
REFERENCE
Katika kuandika bandiko hili nimetumia rejea mbalimbali kama vuile.
Biblia ya Gideon Version
Katekisimu katoliki jimbo la iringa toleo la kumi na mbili 2013
Kitabu cha The purpose driven to life by Rick waren
Google

Written by
Da’Vinci
Oh mkuuu nashukuru sana kwa bandiko hili. Nitalisoma walau mara tatu ili kulielewa vizuri. Barikiwa mno.
 
Hii comment nilisahau.
Kweli kabisa inabidi ureset mind yako. Sahau kila kitu unachodhani unajua kuhusu Mungu na imani. World knowledge wala isikuchanganye.. Stand alone like an empty balloon and start filling it with new ideas.
Kwanza kabisa tafuta Katekism Katoliki kuna kaswali ya msingi kabisa katika imani yanaelezwa. Na sehemu ukiwa una dukuduku tafuta mtu unayeamini anaelewa muulize akuchambulie..

You can ask it at here too...✌️

Noted.
 
Nikikupa Zawadi ya Peni inakua ni mali yako. Maamuzi juu ya Matumizi ya peni hiyo ni juu yako, unaweza amua kutumia peni hiyo kuandika na kujisome ukawa Profesa...Au unaweza amua ukatumia peni hiyo kumtoboa machoni mwenzio.

Mind ni Zawadi ambayo kila mmoja wetu amepewa...Uamuzi wa jinis ya kuzitumia Zawadi (Mind) hizi upo juu yetu. Hivyo tunaweza chagua wenyewe jins ya kutumia Zawadi hizi.
Maumuzi ni yako sasa je utumia Mind hiyo katika Postive perception au lah. Previous post nimezungumzia kwamba Thought shape Reality. So Tumia Zawadi hiyo katika mlengo chanya ili kupata yale yalio mema katika maisha yako na wakunzugukao.

To be continued....
Madini tupu. Tunasubiri mkuu
 
Be careful with what you think because Thought shape Reality. You're what you think and you will get what you think. What you seek is what you will get....Be postive no matter how physical world treat you.. You're only weak outside/physically. But inside you're so powerful spiritually. Draw out your spiritual strength to face the physical world.
You're inner strength start with postive thought.

Trust your Inner you!!

Coach Slamah Hamad mchango wako muhimu kiongozi [emoji3577]


You are so right Chief!

Meli haizami kwa sababu imezungukwa na maji ila inazama kwa sababu imeingia/ingiwa maji!

You are the artist of your own life, don’t hand the paint brush to anyone else!
 
Umetumia nguvu kubwa sana kuelezea kitu ambacho hakieleweki,sio kwamba hamna point, la hasha. Point zipo nyingi tuu lkn umeongelea vitu vingi kwa mpigo ambavyo havina relation.

Ungekuwa kwa daktari, angekwambia una circumferential thinking.

Unforgetable
Inaeleweka, itakuwa una kichwa chepesi
 
My humble personage bow before JF member's grandeur..No other memeber (in JF Intelligence) has ever the might neither nobility to wield not 200 Likes but 320Likes.The honor lies in my grasp.

#ThanksJF
 
✓✓Coppied kutoka Kwenye uzi wangu jukwaa la dini

Nyaraka zote za wakorinto zimeandikwa na Mtume Paulo ambae alikua msomi na ngulii wa mafundisho ya Kifarisayo chini ya mwalimu wake Gamalieli. [Wote tunajua yaliyotokea hadi kua mfuasi wa Kristo]

Kipindi hicho dini nyingi za kipagani zilikua zimejikusanya huko Korintho na miji mikubwa yote, maisha kwa wakristo wa huko korintho yakawa yana taabu sana kutokana na changamoto nyingi kutoka kwa wapagani. Hivyo paulo aliandika nyaraka 2 kwenda kwa wakorintho ili kuwatia moyo na kuwakuza kiimani lakini Paulo aliandika waraka fulani ambao ulikua wa kwanza kabisa kwenda kwa wakorintho Waraka huo ulipotea, haukufika kwa walengwa na haujulikani penye ulipo [1Kor 5:9-13].

Ikumbukwe alipoandika nyaraka za wathesalonike akikua anaishi Korintho.
Paulo aliopokaa Efeso walikuja watu kloe, Apolo n.k watu hao walimtaka Paulo aandike waraka mwingine kueleza na kushauri mambo mbalimbali. Hivyo Paulo aliandika waraka mwingine ambao ndio tunauita waraka wa kwanza kwa Wakorintho uliandikwa Pasaka ya Mwaka 57 Bk.

Baada ya kuandika waraka huo shida nyingine ikatokea korintho hivyo ikambidi kwenda korintho haraka, akarudi tena efeso na kuahidi kurudi tena korintho lakini yakatokea matatizo [2Kor 2:5-10,7:12]hivyo akabadili mpango wake wa kurudi korinto. Hivyo akaandika waraka wenye majonzi mengi kwenda kwa Wakorintho lakini Waraka huo nao ulipotea na haujulikani ulipo.

Baada ya kuvumilia taabu nyingi ambazo hata Kanisa Katoliki halizifahamu alitoka efeso (1KOR15:32, Mdo19:23-40). Hivyo akaandika waraka mwingine kwa wakorintho ambao ndio huu unaoitwa waraka wa Pili kwa wakorintho na mwenyewe Paulo aliweza kwenda Korintho kisha akarudi Yerusalem. Waraka huo umeandikwa mwishoni mwa mwaka 57BK.

HIVYO KWA UJUMLA.
Paulo kaandika nyaraka nne kwenda kwa Wakorinto ambazo ni...
Waraka wa kwanza kwa wakorintho uliopotea.
Waraka wa Pili uliopo ambao tunauita Waraka 1Wakorintho
Waraka wa tatu ambao ulipotea lakini uliwafikia walengwa.
Waraka wa nne ambao tunauita 2Wakorintho.
 
✓✓Coppied kutoka Kwenye uzi wangu jukwaa la dini

Nyaraka zote za wakorinto zimeandikwa na Mtume Paulo ambae alikua msomi na ngulii wa mafundisho ya Kifarisayo chini ya mwalimu wake Gamalieli. [Wote tunajua yaliyotokea hadi kua mfuasi wa Kristo]

Kipindi hicho dini nyingi za kipagani zilikua zimejikusanya huko Korintho na miji mikubwa yote, maisha kwa wakristo wa huko korintho yakawa yana taabu sana kutokana na changamoto nyingi kutoka kwa wapagani. Hivyo paulo aliandika nyaraka 2 kwenda kwa wakorintho ili kuwatia moyo na kuwakuza kiimani lakini Paulo aliandika waraka fulani ambao ulikua wa kwanza kabisa kwenda kwa wakorintho Waraka huo ulipotea, haukufika kwa walengwa na haujulikani penye ulipo [1Kor 5:9-13].

Ikumbukwe alipoandika nyaraka za wathesalonike akikua anaishi Korintho.
Paulo aliopokaa Efeso walikuja watu kloe, Apolo n.k watu hao walimtaka Paulo aandike waraka mwingine kueleza na kushauri mambo mbalimbali. Hivyo Paulo aliandika waraka mwingine ambao ndio tunauita waraka wa kwanza kwa Wakorintho uliandikwa Pasaka ya Mwaka 57 Bk.

Baada ya kuandika waraka huo shida nyingine ikatokea korintho hivyo ikambidi kwenda korintho haraka, akarudi tena efeso na kuahidi kurudi tena korintho lakini yakatokea matatizo [2Kor 2:5-10,7:12]hivyo akabadili mpango wake wa kurudi korinto. Hivyo akaandika waraka wenye majonzi mengi kwenda kwa Wakorintho lakini Waraka huo nao ulipotea na haujulikani ulipo.

Baada ya kuvumilia taabu nyingi ambazo hata Kanisa Katoliki halizifahamu alitoka efeso (1KOR15:32, Mdo19:23-40). Hivyo akaandika waraka mwingine kwa wakorintho ambao ndio huu unaoitwa waraka wa Pili kwa wakorintho na mwenyewe Paulo aliweza kwenda Korintho kisha akarudi Yerusalem. Waraka huo umeandikwa mwishoni mwa mwaka 57BK.

HIVYO KWA UJUMLA.
Paulo kaandika nyaraka nne kwenda kwa Wakorinto ambazo ni...
Waraka wa kwanza kwa wakorintho uliopotea.
Waraka wa Pili uliopo ambao tunauita Waraka 1Wakorintho
Waraka wa tatu ambao ulipotea lakini uliwafikia walengwa.
Waraka wa nne ambao tunauita 2Wakorintho.
Quote hiyo hapo juu hopefully hamjawahi kutana nayo
Mkuu asante kwa andiko hili nami ni mmoja wa ambao hatukuliona mapema..

Nina swali..
Tafsiri ya majina ya Jesus na God katika lugha za makabila yetu ilifanywa na nani? Tukianza na Jesus kuwa ndio Yesu na God ndio Mungu...

Mkuu nashukuru sana kwa kujali, walakini sina access na hilo jukwaa (la dini).

Madini tupu. Tunasubiri mkuu
 
Family, Duty and Honor..

Family comes first, kama kichwa cha familia unatakiwa kuwa pamoja na familia yako muda kuilinda, Kuihudumia na kuiongoza..You can't protect the family if you're not with the family.

Duty comes second...As Kiongozi wa familia Timiza wajibu wako katika familia kama kichwa wa familia anavyotakiwa kua..Hatma ya familia ipo mikononi mwako. Kama Kiongozi fanya wajibu wako uweze kuivusha KIUCHUMI,KIAKILI,KIIMANI NA KIJAMII.

Then Honor.. Ukiyatimiza hayo utapata heshima yako unayostahili kama kichwa wa familia. Utazeeka ukiwa una uso ulio na afya njema maana familia yako itakua mikononi salama mwa mtu uliyemrithisha maneno hayo. Family Duty and Honor.

We all want to belong to something...We belong to the family.. Our family that we care and love.
#Vinjiii
 
Back
Top Bottom