Je, unafahamu prenuptial agreement au mkataba wa ndoa kabla ya kuoana?

SHEVCHENKO

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2019
Posts
331
Reaction score
453
Wakuu kwenye pita pita zangu nimekutana na hii kitu inayoitwa prenup, ila nimeona nikama ina sound good.

Hivi kwa sheria za bongo hii kitu vipi ninaweza kuifanya au sheria hairuhusu??

Wanasheria wa jf mje mtuambie..

Nilivyoielewa kwa ufupi...

Prenup ni kifupi cha neno la Kiingereza Prenuptial Agreement, ambalo linamaanisha Mkataba wa ndoa kabla ya kuoana
Yani makubaliano ya maandishi yanayofanyika kati ya wenza wawili kabla ya kufunga ndoa, yanayoeleza wazi jinsi mali na madeni yao yataendeshwa, kugawanywa au kulindwa ikiwa ndoa itavunjika kwa talaka au kifo.
 
Mada nzuri sana hasa kwa Tanzania ya leo ambayo migogoro ya mali za wanandoa baada ya talaka au vifo imeongozeka sana na wanawake wengi wanatumia mwanya wa ''tumechuma wote'' au ''wanataka kumdhulumu mjane'' kupiga mali wasizochuma.
 
Hiyo ni kwenu nyinyi wakristo,sisi waislamu haituhusu sababu tunayo miongozo yote ya mirathi.
 
Hujaonyesha kama kisheria inatambulika
Nafikiri haitambuliki kwa hapa Tanganyika ila imeeleza kwamba ikiwa wenza wanaweza kukubaliana kwa matakwa yao bila kulazimishana wakaamua kuufanya upendo kuwa ndio kipaumbele chao na sio mali zao, basi wanaweza kutafuta mwanasheria wakaandaa hii document kwa pamoja na kuorodhesha mali zao ambazo hazpaswi kuwa sehemu ya ndoa
 
Hiyo ni kwenu nyinyi wakristo,sisi waislamu haituhusu sababu tunayo miongozo yote ya mirathi.
Vipi kwa waisilam mnashughulikia vipi wanawake ambao wanaingia kwenye ndoa kwa malengo ya kitapeli
 
Vipi kwa waisilam mnashughulikia vipi wanawake ambao wanaingia kwenye ndoa kwa malengo ya kitapeli
Sheria iko wazi, kama ulimuoa kwa halali haki yake ipo japo ni kidogo.
 
Sheria iko wazi, kama ulimuoa kwa halali haki yake ipo japo ni kidogo.
Hiyo kidogo ndiyo hawataki kuisikia sasa hawa wanaharakati yani ukishaingia kwenye mfumo tu kazi unayo
 
Sheria iko wazi, kama ulimuoa kwa halali haki yake ipo japo ni kidogo.
Japokuwa muongozo upo lakini wengi linapokuja suala la taraka na mirathi wanaenda mahakamani na sio bakwata!!
Huko mahakamani kuna makesi mengi ya mirathi za NDOA zilizofungwa kiislam.....

Uislamu ni kwenye kufunga NDOA na kula ubwabwa kwenye mali uislamu unawekwa pembeni
 
Swadakta sote tutafata Sheria mama ya nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…