Je, unafanyaje ukiwa umepigiwa full light barabarani?

Je, unafanyaje ukiwa umepigiwa full light barabarani?

Mtoa mada hapa sio Tu umeomba ushauri Bali ndivyo inavyotakiwa kufanya ukiwa unaendesha gari usiku yote ambayo umeorodhesha ndiyo njia sahihi ya kuepusha ajali Kwa kifupi wewe ni pia unajua kanuni ya uendeshaji usiku.

kwa kuongezea nyama ni hivi ukiwa unadrive usiku zingatia Sana mstari wa katikati hata kama utapigwa taa weka Akilini gari yako isivuke upande wa mwenzako.
pia soma eneo la mbele yako zaidi ya Mita 50 kujua jinsi palivyo hii itasaidia Sana kucheza na upande wako wa kushoto Tu bila kutoka nje zaidi.

na ukitaka kuwa master wa kuendesha usiku jaribu kipande cha DAR -MORO hapa kuna kila aina ya vituko kuanzia mabus,malori na magari madogo pamoja na ubovu wa barabara hapa kuna madereva wastaarabu,walevi na walio na mioyo ya plastic hawaogopi kifo wala KABURI
Usiombe umepigiwa full then barabara imemeguka meguka Yani vipande kama pale kipande Cha chimala ya mbeya ukipigiwa full huoni unatoka nje ya lami unapigiza shimo[emoji1]

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Unapunguza zako unawasha packing alafu unapaki pembeni kwa mda hadi mkubwa apite.ukijifanya unakomaa dereva kama mimi nina tone 32 nyuma nishaweka gari kati kati ya chaki niko gear ya 14 high kitu kina nesanesa eti nirudi kwangu ghafla ili tela ivute nichochore?hapana kwa kweli Mungu atanisamehe maana nikiangalia ushahidi hamna alafu ndio usiku wewe uko na ka ai esi tii kako watakuja kukutindua na tindo kukuokoa au kukupeleka kwenye kabati la mbeho
Je ukikutana na Lori mwenzio utamfanyia hivyo hivyo barabarani heshimuni kila mtu mkuu.

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Mkuu tabia ya mtu kurekebisha ni ngumu mno, but always Linda usalama wako, slow down,keep left, na dim taa zako, ukitaka kushindana naye unaweza poteza maisha, muda na utajiharibia safari yako, kupishana ni less than 4s!
Exactly mkuu Kuna jamaa angu alinipakia siku Moja tunaenda bagamoyo tumefika sehemu tukapishana na magari ya mchanga ilikuwa usiku mwenye Lori alipiga full jamaa macho yake mabovu mbele kidogo bumps hiyo tuliifukia nikamwambia anipe nimpokee.

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Mimi Huwa napunguza mwendo then nakeep left, Kuna wakati nilikuwa na gari flan hiv ilikuwa na full Moja Kali Sana utafikir spotlight, lazma anayekuja akubali kupunguza ndio tunaenda sawa
Wengine ukiwapigia full nao wanapiga Ili waone mbele wanapoenda.

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Mafuso na magari ya kokoto ndo wenye fujo.

Ila semis hawanaga noma. Ni wastaarabu sana.

Wanaoendesha vigari vidogo ndo pasua kichwa sasa. Hao anaweza asipunguze mwanga hata kama umemuomba apunguze.
Hakuna magari yenye mataa ya ajabu ajabu kama mafuso maurembo kibao na taa zao Kali Sana.

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Hakuna watu nawakubali kama madereva wa malori hawa jamaa Wanajitambua Sana mara nyingi usiku huwa ukiwaomba kupunguza taa wanapunguza tena unatakiwa uombe mapema ukiwa mbali ukiwasha taa zako mara 4 lazima atapunguza mwanga Tu na hata ukipunguza mwendo na kuwasha indicator ya kulia atabalnce gari yake asikugonge
Na hata ukipata shida hao ni likely kukusaidia kuliko wengine.
 
Hakuna madereva siwapendi kama waendesha malori....
Nilishapigwa full taa,zile zinakaa juu kabisa ya kibini aisee, aah wakuu mungu ni wakuabudiwa siku zote..
Zile za juu ya cabin ni kisanga mkuu [emoji119]
 
Kisanga hicho, inabidi kuwa mpole tu aiseee. Punguza mwendo na chukuwa tahadhari nyengine za muhimu. Muache aende tu
20221119_002511.jpg
 
Binafs huwa napigiwa pass yakupunguza mwanga ilihali nimewasha mwanga mdogo hii kitu inanichanganya sana ilinibidi niende kwa fundi akanambia ukipigiwa pass ww washa taakubwa in second kisha zima ili ajue kuwa ww hapo ndo upo kwenye mwanga mdogo, sasa nashindwa kuelewa kuwa nibadili bulb ama vipi mana nafeel ninavyowakera watu, gari yenyewe ni HILUX nimeipata hivi karibuni
Adjust beam. Gari nyingi za kisasa zinakuja na switch ya kuadjust beam ya taa ili ichague pa kulenga kama ni direct au ipige kwa kushuka kidogo.
 
Back
Top Bottom