Bob Manson
JF-Expert Member
- May 16, 2021
- 4,158
- 7,787
- Thread starter
- #21
Lakini mtu akiwa na tatizo na akikaa pekeyake mwisho anazidi kuwa na mawazo zaidi, yaani stress.Kuielewa quote nadhani inamaanisha
Mfano wewe ukiwa unapitia shida, una option ya kumuelezea mtu ili akupe ushauri lakini option nyingine. Ni wewe kukaa chini kutafakari hadi upate solution
Sasa inakuwaje unapokaa kimya kwa ajili ya tafakari huwa unapata majibu?.. Hapo inamaanisha badala ya kumsikiliza mtu, unakuwa unaisikiliza nafsi yako
Unakuwa una inner conversation baina yako na nafsi yako. Hivyo tafakari ni kitendo cha kuisikiliza nafsi yako inasemaje katika suala flani. Mm ndo nilivyoelewa
Stress au mawazo sio sawa na kufikiri kwasababu stress huambatana na hisia hasi kama maumivu na majuto.
Nadhani kufikiri ni jambo ambalo lipo katika upande wa hisia chanya na huambatana na hisia chanya kama kubuni, kupangilia mambo na kufanya maamuzi.