Je, unafikiri hizi treni za SGR ndo zenyewe au tumepigwa tena?

Je, unafikiri hizi treni za SGR ndo zenyewe au tumepigwa tena?

Trillion karibu 20 kujenga reli mpya, halafu hawa wapigaji wanatuletea mabehewa na mavichwa kama ya miaka 100 iliyopita, washamba sana hawa au ni wezi wakubwa waliokubuhu, lakini unategemea nini maana huyu waziri mkuu ni muongo kuliko kiongozi yeyote kutokea katika historia Tanzania
Naunga mkono hoja, hili hata mimi nimeliulizia Hongera TRL kwa Mabehewa Mapya. SGR ni Reli Mpya ya Kisasa; Je, Mabehewa Haya ni Mapya ya Kisasa? Hakuna Ubaya Kutumia Mitumba, Ila Tuambiwe Ukweli!
P
 
Maelezi ya kadogosa yana mushkeli...mabehewa ya mwendo mrefu kwa sasa yanakuja kufanya nini wakati reli haijakamilika?tunataka mabehewa ya dar to moro ambao mradi unakamilika hivi karibuni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
*Ni yale yanayotengenezwa nchini Korea Kusini kwa ajili ya SGR

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo na kasi ya ujenzi wa mabehewa mapya kwa ajili Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania yanayotengenezwa na kampuni ya Sung Shin Rolling Stock (SSRT) iliyoko nchini Korea Kusini.

“Kati ya mabehewa 81 ambayo Tanzania inatengeneza kutoka kwenu, tayari 36 yamekamilika na yameshapelekwa nchini Tanzania na 45 yaliyobaki yanategemewa kukamilika Machi, 2023. Mabehewa haya ni ya daraja la tatu na yatatoa huduma zote muhimu.”

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo Oktoba 24, 2022 mara baada ya kutembelea kampuni ya SSRST inayotengeneza mabehewa na injini za treni nchini Korea Kusini.

Kadhalika, Waziri Mkuu amemkaribisha nchini Rais wa Kampuni hiyo Gye Shul Park aje kuwekeza nchini Tanzania kutokana na fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo mpango wa Serikali wa kuendelea kuiboresha sekta ya usafiri wa reli.

“Mnakiwanda kikubwa, teknolojia ya hali ya juu pamoja na utaalamu na watalaam kwenye eneo hili. Kwa sasa tuna mipango mikubwa ya kuendelea kuiboresha sekta hii ya usafiri wa reli, yapo maeneo tofauti kwenye mpango wa kuunganishwa na reli ya kisasa (SGR), nakukaribisha kuja kuwekeza kitu kama hiki Tanzania.”

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea kituo cha Seamul Undong ambacho ni taswira ya maendeleo ya Korea kupitia mpango wa kuviwezesha vijiji ambao unatekeleza mpango huo nchini Tanzania katika mkoa wa Morogoro (Pangawe) na Zanzibar.

Mheshimiwa Majaliwa alimshukuru Rais wa Kituo hicho na kumuomba kuendelea kutoa ushirikiano ili kukuza zaidi mpango huo na kufikia maeneo mengi zaidi.

“Mfumo huu kwasasa umekuwa wa kitaifa, ushirikishwaji wa Wananchi ni mkubwa, sasa tunataka tuikuze zaidi, haya maeneo ya Morogoro na Zanzibar tunataka yawe mifano, kwenye utekelezaji wa eneo hili”

Pia, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea kituo cha Ubunifu cha CEIC kilichopo kikichopo katika mji wa Pangyo


View attachment 2397781View attachment 2397782View attachment 2397783
Hayo ya kitambo tangu Adam na Eva walipokabidhiwa bustani ya edeni walipokulana tunda tu walipanda hayo matakataka kusepa eneo Hilo kwani walisha jua wamekichafua maana wote wawili walistukia wako uchi wakapanda hivyo hivyo na suti zao za Mungu maandazi wale
 
Back
Top Bottom