Tatizo la BRICS ni muungano ambao hauna misingi ya kipekee (common interests and values) ambayo inaziunganisha hizo nchi, tofauti na miungano mingine kama vile EU ama G7.
Tofauti zao ni kubwa sana kiasi kwamba inawawia vigumu kufikia muafaka katika jambo ambalo wote watakuwa na maslahi nalo.
Ukitazama mifumo yao ya kisiasa ya ndani, ni tofauti kabisa. Tukija kwenye malengo na maslahi ya kila mmoja, uhasama ni mkubwa.
Members wawili wenye uchumi mkubwa zaidi katika huo muungano (China na India) ni mahasimu wakubwa. Migogoro ya kimipaka n.k. imepelekea ugomvi wa muda mrefu.
Je, suala lolote lile linalohitaji muafaka ambalo litaonekana kuwa na maslahi zaidi kwa China, hasimu wake (India) italikubali? Na kinyume chake pia, China itaridhia?
Tofauti, uhasama na migogoro ya aina hii ni vigumu kuleta muafaka wenye maslahi ya pamoja.
Aisee eti tatizo la nchi za Brics ni muungano amabao Haina misingi ya kipekee amabyo inaziunganisha nchi hizo ofauti na EU pamoja na G7.
Dah.
Kuna watu mna akili sana aisee.
Yaani wewe jamaa una akili kuliko wataalamu wote wa nchi zote Tano za Brics,yaani wataalamu wa uchumi na mipango wa nchi hizo wewe umewazidi kufikiri.yaani wabunge wao,mawaziri wao,wachumi wao na wasomi wao waliokubaliana kuunda umoja huo kwako wewe ni weupe TU lakini wewe ambae naamini hata ukuu wa wilaya TU hapa kwetu huna.
Sasa ona maajabu.
EU ni muungano wa nchi zinazotokea eneo moja yaani ulaya.ingawa sio nchi zote za ulaya ni memba wa EU.
Pointi yangu hapa ni kwamba Kuna nchi ni wanachama kwa sababu TU zipo eneo hili,lakini ni masikini kuliko baadhi ya nchi za Brics.kwa hiyo sioni u special wa muungano wao zaidi ya kua wanatokea eneo moja
Mfano mzuri wa EU ni kama EA na AU.
Haya njoo kwa G7.
Huu ni umoja kama club TU na kimuundo umezidiwa hata na Brics amabo wewe unajitia kuuponda.ingawa unafanana kijiografia TU
Brics sio kama EU amabo wanatokea sehemu moja Brics imeanzishwa kwa kufuta uwakilishi wa maeneo .mfano kutokea Afrika,Amerika na Asia.
Sasa ona kituko Cha G7 hawa ni kama klabu TU.tunaambiwa ni umoja wa nchi 7 tajiri duniani.
Lakini ukiangalia Kuna nchi ziko ndani ya kundi hilo zimepitwa kiutajiri na baadhi ya nchi zilizo nje ya kundi hilo,mfano china Iko nje lakini imezipita nchi kadhaa za G7.
Urusi iliingizwa ndani ya kundi hilo,lkni ilipoitwaa krimea ikafukuzwa,Sasa hapa najiuliza kwa kuitwaa krimea Urusi ilifiriaiaka na kupoteza sifa?
Kimsingi kama iliingizwa kwa sababu ni tajiri,basi kuivamia Crimea hakuiondolei sifa yake. Ndio nikajua kundi hilo ni la kinafiki TU,mtuvmmoja akiamua Fulani aingizwe anaingizwa,mtu huyohuyo akichukizwa na mtu mwingine anaamua atolewe.
Hata hivyo kijiografia G7 inafanana TU na Brics,G7 Kuna nchi inatokea Amerika,nyingine Asia na nyingine Europe Haina tofauti na Brics.
Sasa wewe ndugu yetu unawezaje kuiona Brics Ina tatizo na haitafanikiwa?
Kama migogoro ya nchi za Brics ni issue mbona Hadi Leo wapo pamoja miaka karibu 20 Sasa?