Bexb
JF-Expert Member
- Oct 24, 2016
- 715
- 1,619
Habari ya usiku wakuu, nawiwa kushare machache kuhusu mada tajwa hapo juu.
Watu wengi wamekua wakitamani ama kuwa na mpango wa kufungua kampuni inayotoa huduma za ulinzi katika maeneo mbali mbali.
Ni rahisi sana kwani mtu huweza kufanya shughuli hii akiwa binafsi ama kupitia kampuni na mahitaji ni kama ifuatavyo:
1. Kibali cha Polisi.
Hiki ni kielelezo cha kwanza na cha lazma ili uweze kufanilisha usajili wa kampuni ya ulinzi. Kibali hiki hutolewa na Inspeka Jenerali wa Polisi(IGP) na ili kukipata utaandika barua ya maombi hayo kwa kuanzia kwa wakuu wa polisi wa ngazi za wilaya, mkoa hadi kwa IGP mwenyewe.
Kujiunga na moja ya mashirikisho ya watoa huduma za ulinzi. Kabla ya mtu kifuatilia kibali cha IGP hapo juu ni lazma pia kupata uanachama wa moja ya mashirikisho kwani hawa hukutambulisha kwa IGP wakati wa kufuatilia kibali hapo juu.
3. Kusajili kampuni.
Baada ya kupata kibali basi hatua inayofuatia ni kusajili kampuni BRELA na huko ada zake hutofautiana kulingana na mtaji utakaoutaja.
Baada ya kusajili kampuni kuna 'Compliance' kadhaa ambazo unatakiwa kuzifanya hasa za kikodi kama ifuatavyo;
1. Kodi ya makadirio(corporate/provisional tax).
Hapa utajifanyia makadirio kwa iasi unachotarajia kuingiza kwa mwaka na baada ya kujikadiria basi kiasi hicho higawanywa na hulipwa kwa awamu nne kwa mwaka.
2. PAYE
Hii ni kodi ambauo utakua ukikusanya kwa wafanyakazi wako kwa niaba ya serikali kisha kuiwasilisha serikalini kupitia TRA. Kodi hii hulipwa na wafanyakazi ambao mishahara yao inaanzia kiasi cha 270,001 na kuendelea.
3. Skills development Levy.
Hii ni kodi ambayo inatozwa chini ya sheria ya VETA na huwa ni 4% ya gross payment ya kila mwezi.
4. Withholding tax on rent
Hii ni kodi ambayo utapaswa kulipa wewe au landlord wako(kulingana na makubaliano yenu) kuyokana na kodi ya pango unayolipa na kiasi husika huwa ni 10% ya thamani ya mkataba husika. Mfano, kama unalipa 10M kwa mwezi basi withholding tax itakua 100k na hii utapaswa kulipa kila mwaka kulingana na mkataba wako wa pango.
5. Leseni ya biashara.
Hii leseni hutolewa katika Halmashauri husika ambako kampuni husika ya ulinzi imesajiliwa na kufunguliwa. Gharama zake huwa ni 201k kwa mwaka.
6. Mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF).
Hii hupaswa kulipwa na mwajiti na mwajiriwa kwa pamoja ambapo mwajiti atachangia 10% na mwajitiwa atachangia 10% ya basic pay ya mshahara wa mwezi. Hapa mwajiri(kampuni ya ulinzi) itatakiwa kujisajili NSSF pia waajiriwa nao watatakiwa kujisajili huko.
7. Wokers Compensation Fund(WCF).
Huku pia kampuni ya ulinzi inatakiwa kujisajiri na gharama za malipo huwa ni 0.6% ya gross pqyment ya kila mwezi.
Kwa kiasi kikubwa hizo ni baadahi ya hints unazopaswa kuzingatia unapohitaji kufungua kampuni. Kama una swali lolote uliza hapa au nicheki
0755963775 calls/WhatsApp