Je, unahitaji mafanikio, uzima, uponyaji, ulinzi na baraka? Fanya hivi

Your browser is not able to display this video.
 
Zaburi 34:10 (NEN)
Wana simba wenye nguvu hutindikiwa na kuona njaa, bali wale wanaomtafuta Mwenyezi Mungu hawatakosa kitu chochote kilicho chema.
 
💡 Ee BWANA, sawasawa na ahadi yako katika Isaya 54:17, nakiri kuwa kila silaha itakayofanyizwa dhidi yangu haitafanikiwa, na kila ulimi utakaonishtaki utauthibitisha kuwa mwongo. BWANA, napokea ahadi hiyo katika Jina la Yesu, amen.
 
💡 Ee Baba, katika Warumi 8:37 umenena kwamba katika mambo yote, mimi ni zaidi ya mshindi kwa Yeye aliyenipenda. Nakiri ushindi katika biashara yangu, nakiri ushindi dhidi ya adui zangu, nakiri ushindi katika masomo yangu, nakiri ushindi katika kila eneo la maisha yangu, katika Jina la Yesu Kristo, amen.
 
💡 BWANA wangu, kama ulivyonena katika Zaburi 23:1, nakiri kuwa Wewe ndiwe Mchungaji wangu, na hivyo sitapungukiwa na kitu chochote. Napokea utoshelevu wako katika Jina la Yesu, amen.
 
Ujumbe mzuri sana. Ila maneno yaambatane na Imani.

Imani changanya na ukiri = Matokeo tayari.

Unaweza kukariri na kukiri lakini Imani yako isikubaliane na hayo unayokiri.

Watu wa Dini ndio mabingwa wa kukariri na kukiri lakini Imani yao ipo mbali na hayo wanayokiri.

Ndio maana Daudi alisema. Mawazo ya moyo wangu na maneno ya kinywa changu yapate kibali mbelezako Mungu wangu.

Mtume Paulo Alisema. Neno like lililosikiwa kwao halikuwafaa kwa sababu walipo lisikia hawakuli hanganya na Imani.

Hivyo basi Imani + Ukiri = Umejibiwa.
 
Watu wa Dini ndio mabingwa wa kukariri na kukiri lakini Imani yao ipo mbali na hayo wanayokiri.
Mungu awasaidie wakiri na kuamini ili waone ahadi za Mungu zikitimia katikati yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…