Je, unaijua mikataba ya Haki za Binadamu ya Kimataifa ambayo Tanzania imesaini?

Je, unaijua mikataba ya Haki za Binadamu ya Kimataifa ambayo Tanzania imesaini?

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
MKATABA WA HAKI ZA BINADAMU NA HAKI ZA WATU WA UMOJA WA AFRIKA (MKATABA WA AFRIKA)
Kifungu cha 9 cha Mkataba wa Afrika kinalinda haki ya uhuru wa kujieleza na kutoa maoni:

1. Kila mtu atakuwa na haki ya kupokea taarifa.

2. Kila mtu atakuwa na haki ya kujieleza na kusambaza mawazo yake kwa kuzingatia misingi ya sheria. Tume ya Haki za Binadamu na Haki za Watu ya Umoja wa Afrika (ACHPR) ina wajibu wa kufasiri Mkataba huo. Tume hiyo imekuwa ikitekeleza wajibu huo kwa namna mbalimbali, ikiwemo njia ya kutoa Maazimio na Matamko.

TAMKO LA KIMATAIFA LA HAKI ZA BINADAMU (UDHR)
Kifungu cha 19 cha Tamko hilo kinasema: Kila mtu ana haki ya uhuru wa kutoa maoni na kujieleza; haki hii pia inahusisha uhuru wa mtu kuamini katika maoni yake bila kuingiliwa kwa namna yoyote, na uhuru wa kutafuta na kusambaza taarifa, maoni na mawazo yake kwa njia yoyote bila ya kujali mipaka.

MKATABA WA KIMATAIFA WA HAKI ZA KIRAIA NA KISIASA (ICCPR)
Tanzania imeridhia mkataba huu mwaka 1976, na hivyo inawajibika kisheria kufuata masharti ya mkataba huo. Kifungu cha 19 cha mkataba huo kinazungumzia uhuru na haki ya kujieleza:

1. Kila mtu atakuwa na haki ya kuwa na maoni na kuyaamini maoni hayo bila ya kuingiliwa kwa namna yoyote.

2. Kila mtu atakuwa na haki na uhuru wa kujieleza; haki hii itahusisha mtu kutafuta, kupokea, na kusambaza taarifa. kwa njia ya mdomo au maandishi, na bila ya kujali mipaka, kwa kuandika au kuchapisha, kwa njia ya sanaa, au njia nyingine yoyote atakayoichagua.

3. Utekelezaji wa haki zilizoainishwa kwenye aya ya 2 ya kifungu hiki kinaendana wajibu na majukumu maalum. Kwa hivyo, haki hiyo inaweza kuhusisha vikwazo mbalimbali, hata ambavyo ni vya muhimu na vitawekwa kwa mujibu wa sheria:

(a) Vinavyolenga kulinda haki na heshima ya watu wengine;

(b) Vinavyolenga kulinda usalama wa nchi au utulivu wa kijamii, au afya na maadili ya jamii.

MIPAKA YA UHURU WA KUJIELEZA
Haki za Kikatiba, ikiwemo Ibara ya 18, hazitatumiwa au kutekelezwa na mtu mmoja kwa namna ambayo itazuia au kuingilia kati uhuru wa watu wengine, au maslahi ya umma (Ibara 30(1)).

• Kuhakikisha ulinzi, usalama wa jamii, amani katika jamii, maadili ya jamii, afya ya jamii, mipango ya maendeleo ya miji na vijiji, ukuzaji na matumizi ya madini au ukuzaji na uendelezaji wa mali au maslahi mengineyo yoyote kwa nia ya kukuza manufaa ya umma; au

• Kulinda heshima, haki na uhuru wa watu wengine au faragha ya watu wanaohusika shauri lolote mahakamani, kuzuia kutoa habari za siri, au kutunza heshima, mamlaka na uhuru wa mahakama.

JamiiTalks
 
Upvote 0
Hii mikataba ya haki za kibinadamu ya kimataifa wakati mwingine haiendani na mila na desturi zenu, wakati mwingine tunalazimishwa hata mambo ya ajabu kama ushoga kisa hii mikataba ya ajabu.
 
Yaani mikataba mingi tunalazimishwa kufuata mila na desturi za mabeberu

Hovyo sana, Waafrica tujitambue
Hii mikataba ya haki za kibinadamu ya kimataifa wakati mwingine haiendani na mila na desturi zenu, wakati mwingine tunalazimishwa hata mambo ya ajabu kama ushoga kisa hii mikataba ya ajabu.
 
Huwa madikteta hawapendi kabisa kusikia mambo ya haki za binadamu. Nasikia hata mikataba ya Arusha ilitakiwa kuvunjwa ili wapate kufanya watakavyo. Mutharika wa Malawi anateseka sasa ameondolewa kinga ya kushtakiwa na anasuburi kuburutwa kizimbani siku yoyote.
 
Huwa madikteta hawapendi kabisa kusikia mambo ya haki za binadamu. Nasikia hata mikataba ya Arusha ilitakiwa kuvunjwa ili wapate kufanya watakavyo. Mutharika wa Malawi anateseka sasa ameondolewa kinga ya kushtakiwa na anasuburi kuburutwa kizimbani siku yoyote.
Safi sana..hii ni funzo kubwa kwa watu wote wanaojiona kama Miungu wangu.Watu wote wanaofikiri wako juu ya sheria....etc...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom