Mkuu MMKJJ, maoni ni maoni tuu, mkusanyaji wa maoni, halazimishwi kufuata maoni ya wengi bali huongozwa na reasonableness ya maoni husika!.
Tume ya Nyalali, ilipokusanya maoni ile 1992, asilimia 80% ya wananchi walitaka chama kimoja kiendelee na ni asilimia less than 20% ndio waliotaka vyama vingi!. Kama tume zingefuata maoni ya wengi, where would we have been!?. Hivyo vyama vingi tulilazimisha tuu ndio wale asilimia 80% ya wakati huo wameendelea kuchagua chama kile kile!.
Kilichotoka sio katiba ni rasimu ya katiba tuu, hivyo there is ample room, tutoe maoni kuiboresha tupate japo "bora katiba!" japo tulitaka katiba nzuri, tunacholetewa ndicho hiki, lets make the best of what we get!.
Mimi msimamo wangu ni ule ule juzi, jana na leo!, "if you can't get what you want, just take what you get!", "moja shika sii kumi nenda rudi!", hii moja ndio fimbo iliyoko mkononi, ndiyo uiawayo nyoka!". Shika fimbo, uwa nyoka, shika hii moja iliyopo, ukishaimiliki, ndipo zifuate zile kumi za nenda rudi!".
Tutoe maoni, tupate katiba!, vinginevyo we'll be back to squire one!.
Pasco.
nimekuwa mpole ghafla, haya bhana!