Je, unajua ni kwa namna gani maks zako zinapatikana usaili wa kuzungumza bila upendeleo ikiwemo sekretariate?

Je, unajua ni kwa namna gani maks zako zinapatikana usaili wa kuzungumza bila upendeleo ikiwemo sekretariate?

Joined
Mar 23, 2023
Posts
93
Reaction score
108
👉One of the biggest concerns people have during interviews is the fear of being unfairly judged by the interviewer based on attitude and perception. Today, I will share how your marks are protected. Naaam!

Mchakato wa utoaji maksi umedhibitiwa vizuri kwa kiasi hasa pale sekretariate ya Ajira😁, kwani mwongozo wa utoaji maksi uko kwenye marking scheme iyo ni kwa any professional Recruitment Agency duniani. Jambo kubwa zaidi ni kuwa paneli ya usaili inaundwa na watu wanne hadi watano, na kila msaili anajaza maksi zako kwa kufuata muongozo huo kivyake. Hii inasaidia kupunguza au kuondoa upendeleo.

👉Kwa mfano, msaili wa kwanza anaweza kukupa maksi 88, wa pili 82, wa tatu 78, na wa nne 84, lakini kama msaili mmoja amekuwekea maksi 30, hiyo maksi ya 30 inakataliwa. Uwezo wako utapimwa kwa kutumia wastani wa robo tatu ya maksi zilizowekwa na waendesha usaili wengine.

Vile vile, kama wa kwanza amekupa 28, wa pili 32, wa tatu 35, na wa nne 27, lakini msaili mmoja amekupa maksi 99, hiyo maksi ya 99 pia itakataliwa. Badala yake, wastani wako utatafutwa kutoka maksi zilizopo katika kiwango kinacholingana.

Pia, msimamizi kutoka Sekretarieti ya Ajira anakuwepo wakati wa usaili ili kuhakikisha mchakato unaendeshwa kwa kufuata kanuni. Ikitokea umeonewa au umewekwa kwenye hali ya kupanikishwa, msimamizi anaweza kufuta mchakato huo na kuwataka waanze kukuhoji upya.

👉Swali linaweza kuwa, kwa nini maksi zinatofautiana? Hii hutokea kwa sababu, mara nyingi, waombaji hawajibu maswali kwa usahihi kabisa kama ilivyoainishwa kwenye marking scheme. Kwa hiyo, msaili anaangalia kama hoja uliyotoa ni sahihi; kama ni kweli, anakupa maksi stahiki. Hata hivyo, inaweza kutokea kwamba msaili mwingine anaona hoja hiyo sio sahihi au haikukidhi vigezo na hivyo anakupa maksi chache au 1.5 kwa kila hoja.

Jambo muhimu zaidi ni kwamba, katika paneli ya usaili, lazima kuwe na mtaalamu bingwa wa fani husika, ambaye elimu yake ni kubwa zaidi ya ile ya waombaji. Kwa mfano, katika usaili wa Bachelor, lazima awepo mtu mwenye shahada ya uzamili (masters) inayohusiana na elimu na somo husika ili kutoa hukumu ya mwisho. Ikitokea msaili mmoja amekupa maksi za chini sana, mtaalamu huyo anaweza kuelezea kama maksi hizo zinafanana na ukweli au la, na akitetea msimamo wake, maksi zako zinaweza kurekebishwa. Hata hivyo, mtaalamu huyo naye pia ana jaza maksi kivyake.

Maksi zinatolewa kwa kuzingatia maswali ambayo yana majibu yanayoweza kupimika. Kwa mfano, ukiulizwa utaje vipengele vitano vya lesson plan, kila hoja inaweza kuwa na maksi 2 – hoja yenyewe inakupa maksi 1, na maelezo yake yanakupa maksi 1, jumla 2. Kwa hiyo, ukiweza kutaja na kueleza kila hoja, utapata maksi 10 kutoka kwa kila msaili.

Unapoingia kwenye usaili, hakikisha unaonyesha uwezo wako. Hakuna maswali ya kukuvuruga ambayo hayahusiani na mada; maswali ni sawa kwa waombaji wote. Hakuna kitu kama msaili kuamua kukupa maksi 0 bila sababu. Zaidi ya hayo, sheria inamtaka msaili ambaye ana uhusiano na muombaji kutoa taarifa na kujiondoa kwenye mchakato wa usaili mapema, bila kuficha uhusiano huo.

By Josephat H
255656480968

IMG-20241004-WA0003.jpg
IMG-20241004-WA0002.jpg
 
Back
Top Bottom