Je, unajua tendo la ndoa ni haki katika ndoa na lisipotimizwa linaweza sababisha ndoa kuvunjika?

Je, unajua tendo la ndoa ni haki katika ndoa na lisipotimizwa linaweza sababisha ndoa kuvunjika?

Marichris

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2020
Posts
571
Reaction score
509
Iko hivi, ndoa ni mkataba kati ya mke na mume, na mkataba huo una masharti mengi ikiwemo haki ya tendo la ndoa, sasa inapotokea mwanandoa ananyimwa haki hii moja kwa moja mkataba unakuwa umevunjwa kwani masharti ya mkataba hayajatimizwa.

Haki hii ni lazima iwe imevujwa kwa makusudi bila kuhusisha sababu kama maradhi na kasoro za kimaumbile, ikivunjwa kwa makusudi inaweza kupelekea kuvunjika kwa ndoa. Hii ni kwa mujibu wa SHERIA YA NDOA 1971
 
Halafu Mkuu, sheria ya ndoa ya Tanzania hairuhusu Mwanandoa kuuza mali ya familia bila maridhiano na mwanandoa mwingine. Kwa maana kwamba Mali yoyote inayopatikana kwa nguvu ya wanandoa wote wawili na inayomilikiwa kwa pamoja haiwezi kuuzwa bila maridhiano ya wanandoa wote na haiwezi kuuzwa bila mke au mume kujulishwa na kuridhia hayo. Kifungu cha 59 cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kinaelekeza hayo
 
Pia sheria ya ndoa inaruhusu mke au mume kumiliki mali zake binafsi. Ina Maana kwamba ndoa haiondoi umilikaji wa mali binafsi kwa mwanandoa, kama mke au mume alikuwa na mali fulani kabla ya ndoa mali hiyo inabaki kuwa yake peke yake hata baada ya ndoa.

Mali zinazopatikana kwa nguvu ya wanandoa wote wawili hizo huwa ni mali za pamoja na zinamilikiwa na wanandoa wote wawili.
 
wife ana kibendi ni mwezi wa 4 unaenda hatoi tendo...sasa nifanyeje

na yeye anasema hataki maana anachoka.!

hivi tu nina ugwadu hatarii hataree; unanisaidiaje
 
Mbona hizi sheria za ndoa inaonekana za zamani sana? 1971 mpaka leo no updates.?
 
Afadhali kama yapo, maana naona kama my marriage strives in the past kwa hizi sheria ambazo hata nilikuwa sijazaliwa wakat zinatungwa
Mkuu kuna marekebisho yake ya mwaka 2002
 
Pia sheria ya ndoa inaruhusu mke au mume kumiliki mali zake binafsi. Ina Maana kwamba ndoa haiondoi umilikaji wa mali binafsi kwa mwanandoa, kama mke au mume alikuwa na mali fulani kabla ya ndoa mali hiyo inabaki kuwa yake peke yake hata baada ya ndoa. Mali zinazopatikana kwa nguvu ya wanandoa wote wawili hizo huwa ni mali za pamoja na zinamilikiwa na wanandoa wote wawili.
Naomba nifafanulie hapa;

1. Inakuaje wana-ndoa kumiliki mali binafsi wakati "ndoa" huwafanya kuwa mwili mmoja.

2. Ikiwa kila mtu (mwana-ndoa) anaweza kumiliki mali zake, ni wakati gani ambapo mali za mume au mke itatambuliwa kuwa ni "mali ya familia"?
 
1. Mkuu nyinyi kuwa mwili mmoja hakuwafanyi kama wakati mnaoana mlikuwa na mali zenu binafsi then baada ya kuoana zile mali ziwe sehemu ya mali zenu za ndoa, Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 58 cha sheria ya ndoa.

2. Mali yoyote inayopatikana kwa nguvu ya wanandoa wote wawili na inayomilikiwa kwa pamoja wakati wa ndoa yenu na hii mali haiwezi kuuzwa bila maridhiano ya wanandoa wote na haiwezi kuuzwa bila mke au mume kujulishwa na kuridhia hayo. Hii ni kwa mujibu wa Kifungu cha 59 cha sheria ya ndoa ya 1971 n1 marejeo ya mwaka 2002 kinaelekeza hayo.
 
Ningefurahi kama ungekuwa una quote kifungu cha sheria kwa ukamilifu wake (ili kujifunza zaidi).

1. Je ni sahihi kuamini kwamba, tangu tarehe ya ndoa mali binafsi za wana ndoa huwa ni mali za familia?

2. Je ikiwa nilichouliza hapo juu si sahihi, nini dhana ya uhitaji wa ridhaa ya mwenza kipindi anapotaka kuuza mfano ardhi? (Kwa sababu, Sijawahi kusikia wakati wa uuzaji eneo mtu akiulizwa ni "mali yako kabla au baada ya ndoa, ili iuzwe bila ridhaa)
 
1. Je ni sahihi kuamini kwamba, tangu tarehe ya ndoa mali binafsi za wana ndoa huwa ni mali za familia?
Mkuu Sheria ya Ndoa imeainisha haki mbalimbali za wanandoa. Kimsingi mke ana haki sawa na mwanaume katika ndoa.Baadhi ya haki zilizoainishwa ni pamoja na; Haki sawa kwa mwanamke katika kupata, kumiliki na kugawa mali yake. Haki hii ni kwa mali zote zinazohamishika na zisizohamishika.

Mwanamke ana haki ya kuingia katika mikataba, kushtaki na anaweza kushtakiwa, na pia Mwanandoa ana haki ya kuishi katika nyumba ya ndoa kipindi cha ndoa. Mwanandoa ana haki ya kumiliki mali binafsi na pia kumiliki mali kwa pamoja na mwanandoa mwenzake.Mali iliyochumwa kwa nguvu au jasho la wanandoa wote itahesabika kuwa ni mali ya pamoja katika ndoa.
 
2. Je ikiwa nilichouliza hapo juu si sahihi, nini dhana ya uhitaji wa ridhaa ya mwenza kipindi anapotaka kuuza mfano ardhi? (Kwa sababu, Sijawahi kusikia wakati wa uuzaji eneo mtu akiulizwa ni "mali yako kabla au baada ya ndoa, ili iuzwe bila ridhaa)
Mkuu pia Mali iliyo katika jina la mwanandoa mmojawapo itahesabika kuwa mali binafsi ya mwanandoa huyo.Sasa Dhana hii inaweza kukanushwa na mwanandoa mwingine kwa kuthibitisha vinginevyo. Mali iliyo na majina yote mawili ya wanandoa itadhaniwa kuwa ni mali inayomilikiwa na wanandoa wote kwa pamoja katika mafungu sawa.

Dhana hii pia inaweza kukanushika. Kwa maana ya Mchango wa mume/mke katika ndoa unaweza kuwa wa hali na/au mali. Mfano ni Kesi ya Bi Hawa Mohamed iliyotambua mchango wa mama wa nyumbani katika kutunza na kupatikana kwa mali.

Si ruhusa kwa mwanandoa kuweka rehani, kuuza, kutoa zawadi au kubadili umiliki binafsi wa mwanandoa mwenzake pasipo ridhaa yake. Pia mwanandoa hana ruhusa ya kumzuia mwanandoa mwenzake kumiliki mali au kugawa mali yake binafsi.
 
Kabisa lazima mkataba uvunjwe maana nimefunga ndoa ilinihalalishe tendo sasa akininibania kutakuwa hakuna mkataba tena hapo sawa nakuwa mseja na sio kingine.
 
Back
Top Bottom