Wakongwe wa Mafinga JKT (1980), Eagle Coy, Operation Tija hatutamsahau Afande Masoda, Kapteni Mangwembe na Sajenti Mungure. Kero ya pale ilikuwa baridi kali mno na unapangwa gadi Changarawe; Dah hakuna rangi utaacha kuona. Kingine ni kutokuwepo kwa viti au fomu za kukalia. Kila siku kwenye Chenja lazima ukae chini kwenye mchanga/vumbi sio kuchuchumaa i.e makalio lazima yaguse ardhi - Unachafukaje!!
Kero nyingine ilikuwa ni kufyagia asubuhi- kuna giza na mifagio tunaikata wenyewe kwenye kapori ka miti ya Miwati pembeni mwa barabara (smart Area). Hako kapori kalikuwa ni mahali pa kujisaidia haja kubwa wale wanaokuwa Kota gadi. Sasa kwa giza hilo huoni chini na utakanyaga sana mavi. Matokeo yake Mnanukaje mtakapoenda kwenye uji kwa mwendo wa kunyakuwa-nyakua..[emoji23]
Sali/Omba siku hiyo usikutane na Afande Nusumungu.... yupo "Heey! Zoezi limebadilika... Nyumaaa geuka'....." na ngarambe ndo inaanzia hapo.
...I love those Old Good Days .