Hahahaha nimekumbuka mbali sana, I was in RUVU CTS enzi za Urio, Chota, jalala, nilikuwa mkuu wa kitengo cha Garage. niliwafufulia Scania lilokuwa limekufa fo so long time. Afande mmoja sebelo akanikumbuka kuwa nilikumfundisha kutengeneza magari sehemu ya Engine room Saab scania pale Pugu road. Akanidabua tukiwa tunarudi kutoka kulisha kuku. Just two days after I reported JKT. Tangu hapo Kombania wataniona wakati wa disco. Order ilitoka kwa CO. Niliyaona mengi. Mabaya na mazuri. Lakini yote yalilenga kumjenga na kumfanya mtu kuwa mkakamavu
Kama huna apetite basi jeshini unaweza kuazima apetite kutoka kwa kuruta mwenzio maana kulingana na maelekezo ya afande kukubha liyesoma Jangwani high school!! (mwanaume huyo!!) kulikuwa na kuruta wenye apetite mbilimbili.(He meang mess tin).
Kama vijana wa leo kitu walichokosa maishani ni experience ya JKT. kule kuna mizengwe, ulaghai, mbinde, uongo, kuzingiziwa, kuonewa, ujasiri,usawa,utii, amri, kejeli, uovu, mamlaka, upendeleo, ufuska, kila jema na baya unaloweza kufikiria utalikuta JKT. Hayo yote yalijiri ili kukuweka wewe kikuruti uwe mgumu! uone jinsi amabvyo ulimwengu ulivyo.
Ukiwa selule kama ni binti basi umechagua maafande wajipange ili wapate favor, Binti ukiwa mgumu basi Quater guard kila leo, adhabu zisizo na mpango haziishi. Lakini maafande wakishundwa basi wanakuacha na wanakuheshimu.. Au la Kama uko jikoni Basi PORORO kwa afande(Nakumbuka wakati mmoja master parade ya CO URIO--RIP)walidakwa maafande kibao na Vilambo!! mpka maofisa!
Nakumbuka tukiwa kuruta bado baada ya disco then MINAZI(Hapo vijana wa kiume huwasindikiza wasichana serengeti then they may kiss) Vijana wakirudi hangani basi kila mmoja anaeleza mekunywa denda lita ngapi!!
Mimi nilikuwa Danger coy( kwa Babu, mwambingu, na (kukubha-means craw)
mwambingu akiwania binti basi chakula cha jioni kula ni juhudi yako. Mtanyakua mpaka mkome!
Nakumbuka kulikuwa na jamaa waliweza kujongo kazi kwa muda wa miezi kadhaa bila afande yeyote kujua. ilitokea siku moja kukawa na kitengo 'kwa CO kutengeneza mlngo wa mbuzi' basi kila siku jamaa wana shoka , panga na msumeno kwa CO. Kumbe wanaishia Vibwende.
Kisa kingine binti mmoja alikwenda kulisha kuku, akeba mayai, basi kufika quater guard afande akaanza kukagua na kirungu akigongagonga mifukoni na katika kofia. huyo binti alipofikiwa agongwa kichwani wacha udelela wa mayai uanze kutririka kutoka kichwani!! Mie nilijifunza kunywa mayai mabichi JKT.
Another memorable ki kisa cha servicemen kutandika kitanda vizuri kumbe wamelegeza springs afande akija anadhani wako nje kumbe jamaa wanauturumua! no mchakamchaka!
Kisa cha kingine ni wapendwa tulikutana kwa muda mfupi tu kumuomba Mungu baada ya disco. badala ya kwenda Kula denda tuilkuwa tunakutana briefly kuomba. Afande mmoja alikuwa anmfuatilia mpendwa mwenzetu. Akaamua kula njama na Ma -MP wakaja wakatudaka na mashitaka ni kukutana nyakati za usiku mafichoni bila kibali kwa lengo la kupindua serikali. Mashahidi wakajitokeza wakiwa ni maafande. Mungu bariki Nilimconfront Urio na nikmweleza ukweli what happened. na alikuwa ananiamini kwani akitaka kwenda DAR basi nilikuwa naifanyia gari lake service. Akaamuru kufuta mashataka. Tukapona. JAMANI!!
It was funny and adventurous to be at Nationa service.