Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Nasikia Chita ndo uliikuwa mpango mzima, Mimi Oljoro tulikula bata kwa Maduma E Coy...
 
Wale wa 823kj msange tabora mpo? Siku hizi ni kuangushia tu hamnaga hata mkesha. Dah maisha yanaenda kasi sana nikipakumbuka hapa hakukuwa na amani hata kidogo na ukiwasimulia vijana wanaona unatania au unawatisha
 
Nasikia Chita ndo uliikuwa mpango mzima, Mimi Oljoro tulikula bata kwa Maduma E Coy...
Mkuu kama sikosei huyu afande Maduma ndiye alikuwa pia pale Maramba JKT (operesheni programu ya chama) B-Coy chini ya afande Mapunda aliyekuwa OC kipindi hicho CO akiwa afande Urio then akaja afande Lyaruu. Huyu Maduma alikuwa tall hivi, mweupe kiasi na nadhani alikuwa mgogo. Wakati huo alikuwa ni staff sergent na alikuwa na demu wake hivi kuruta bibi shamba akiitwa......Mara ya mwisho nilionana na Maduma mwaka 2006 akaniambia kwa wakati huo alikuwa ni mkufunzi wa mgambo wilaya ya Kinondoni. Kuna watu uwa siwasahau kama Narsis Mboya, Emmanuel Kabadi, Gumuso Ng'honholi, William Shija (akitokea Tabora), Joash Kunaga, Kagimbo, Deusdedit Buberwa, Denis Mbekenga(R.I.P.), Kachuli (muha, mbishi wa ukweli), mdogo wake wa kike na CO Lyaruu, Ernest Milinga (huyu alikaa sana pale zahanati kambini), Ernest Kaupunda(R.I.P), Jovin Kapinga, Kaniki, John Henjewele, Jasson Bagonza, Shauritanga, Elizabeth Kyoga, Kimoleta, Mussa Nyantaba, Arnold Buretta, Kajobi, Anna-Janeth Pius, Makaranga, Audax Mbelwa, Audax Makyao, Agnes Makyao, Mndeme, Benjamin Nyawela, Antony Mathew Mbuba, Lwambano, Arnold Mwaisumbi, Eliapenda, Kassim Ndossi, Mary Mshana, Anna Maluila (R.I.P.), Evelyne Mshigwa, Mwasiti Jumanne (Jumanne?), Aliko Mwakalindile, Rachel Kaduma, Hamis Madoheka, Hamis Bakari (mpiga maji na machachari kweli kweli-kuna wakati alipata pass akaenda kwao akarudi kambini na fimbo ya kaka yake mlemavu huku kalewa chakari), Zayumba, Humphrey Minja, Magnificent, Abel Ntupwa, Muhsin Salim Masoud, Mwang'ombe, Msafiri (akipenda sana kuimba nyimbo za Bob Marley, Lucresia Tarimo, Charles Morris, Fortunatus Michael Kambaragwe, Pantaleo, Peter Masika, William Davis na rafiki yake Shaaban Issa, Mlingo, Ferdinand Soka, Mwambuja, Renatha, William Jengo, Furaha Shayo, Mdingi, Fidelis Shirima, Lusekelo, Mlingi, wolfgang Pissa na wengineo wengi tu. Pia maafande kama Meshi, Waziri, Mnguluta (tonge nyama), Hussein, Pili (huyu akiwa bustanini B-Coy) Mwakalasya, Songela, Salamba etc.
 
Mafinga JKT Program ya Chama mpoooooooo! Tundu Lisu njoo na vile vituko vyako! Jamani Kanali Mlay yupo? Kafupiiii lkn kalikuwa machachari hako! Sauti yake inakwenda km 1! D-KOY kulikuwa na Sir Major aliitwa 'Nusu Mungu' Hatareee weka mbali na watoto!
 
Mafinga JKT Programme ya Chama wapi akina Mahoo, Alexandra Mmasi, Clement Mkusa, Conrad Shio, Majoro, Gilbert Chawe, Said Msina, Kivamba, Doris Mbuya, Emma karuesa, Elexandina, Hilda Lyatuu, Debora, Fransisca, Kalinga, Maimu(hatari kwa mahindi ya kukaanga) nk.
 
Wengine tulikosa jeshi kwasababu ya sheria kuwa ilishafutwa lakini hapo Same Secondary napo ilikuwa kama jeshi tu.

Kwa nini mkuu? kwa sababu ya yale maji ya kuchota kutoka stesheni ya treni au kwa sababu ya mwalimu Kavuye na Mziray?
 
Yaani jf ninaipenda nisipoisoma nitakunywa sumu juu yake lazima nipite kama sala vile.mleta uzi big up sana yani nimefurahi kuna story nilikuwa nimeshasahau.long sana.Na pia huu uzi tunachangia sisi watu wazima kama hiyo story ya mlimbila imenikumbusha mbali alikuwa shem wangu,ni kweli afande Urio alifariki.mie nakumbuka miaka 90 Ruvu JKT kuna dada mmoja Alice Kambona alikuwa fundi umeme kutwa nzima alikuwa anazunguka testa ktk nyumba za maafande kule bonde kwa ile njia ya short kati kutokea mlandizi.na ile mijoko maana kuli kuwa na nyoka balaa ktk ile kambi.dah siku nakutana na Alice bungando nikabaki nashangaa tu fundi umeme anasomea uuguzi tena.ila tukio ambalo lilikuwa baya zaidi ni kifo cha Abraham Maji aliengua moto ktk hanga kweli lilisikitisha sana.kwa wale wadada waomkumbuka Dr Omary(marehemu)aliwasaidia sana kuwapa ruhusa za uongo.cha mwisho ni ilie salam jambo afande.ilikuwa mateso lkn tulijifunza kama sasa tumbushana tunafurahi
 
haha EAGLE COY HAPA,,,kombania ya demo aseeh....juzi juzi tu hapa OP-MIAKA 50 YA JKT...wenyewe wanaite eti op malela...aseeh kukesha ni shida ukipewa hata dk 5 tano tu mnakoroma na kujamba kabisa
 
Hahaha..chupi ya vip, usiivae ukaendesha baiskeli.
 
No ila mademu kama kawa na hivyo wanakua wamepimwa UKIMWI

Mmh kupima c wanapimwa wanafunzi tu hao makamanda wanaotoa mafunzo kwani nao wanapimwa ikitokea umepata Demu kumbe mnashea kugegeda na kamanda wako c majanga hayo. Kinga muhimu jichanganye uikanyage miwaya. Gambe halina stress km hizo za magonjwa
Km gambe ruksa hata mi ningeenda ila tatizo umri umenitupa mkono
[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji38] [emoji38] [emoji38]
 
Hv Kwenye mafunzo hayo unaruhusiwa kupiga gambe?

Unaweza kunywa baada ya zile wiki sita.Unaweza kuvuta hata fegi ila uende eneo la peke yako usidisturb watu

Madawa ya kulevya,kuanzia bhang,mirungi,ugolo,kuber na unga hauruhusiwi ukikamatwa na afande mnaa akakupeleka kwa wakubwa unafukuzwa kesho
 
Wakuu kwanza nashukuru kwa thread hii..Mimi Nina swali kwenu mliopita jkt,je Mara MTU unapokuwa umeapply kujiunga jkt kwa wilaya yako,je no utaratibu gan hutumika kuwaita watu kwenye interview?msaada tafadhar wakuu,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…