Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Anaboa sana yeye mwenyewe hajui kwata amechoka ila anajua kutesa,ndo tulikuwa nae yule combania barumwina anaitwa jina lingine daah,
ila ukifuata anachotaka akutesi alikuwa anadeal na wasichana wanaoenda kwa service anawaadhil mbele ya combania
Aise ila jeshini nidhamu tu,Nikikuwa nikikaona naona kabisa nakafua bila shida ila basi tu,kuna yule private wa kike white mzuri lakini anaroho ya ibilisi nimemsahau jina
 
Alafu hapo utasikia..
Weee kadoji tuu umekimbiza mwili jina tunalo.. mamaye sitokaa nisahau aisee

Dadeeek!!! ulijiona mjanja kukumbiza mwili jina ukaacha nyuma?!! tuambie ulivyorudi hilo doso lake
 
Dadeeek!!! ulijiona mjanja kukumbiza mwili jina ukaacha nyuma?!! tuambie ulivyorudi hilo doso lake
Baba usinikumbushe maana nilikula kadebra la hatari kama sio vyeti vyangu ***** jeshi lao ningewaachia maana ule nziki nilokula wale washenzi walitaka kuniuwa nadhani
 
Mambo ya jeshini jamani hapana ,nakumbuka nilivyokua naambiwa kwenye mazoezi ya kwata 'Nanga huyu wa Demo kwa mwendo wa haraka mbele tembea basi nikianza kutembea watu wote hoi kwa kicheko sijui kwanini hahaaaa'
 
Ahahah nna namba yake ya simu bhan, huwa nafurahia sana nikongea nae nikakumbuka madoido yake hahah
Kuna Yule alikua sir meja wa D coy alikua na macho flani hivi, sasa yule alitukamata tumedoji afu tumelala kule HQ mike tulibeba dunia kama Masaa mawili sitasahau
 
Niwakumbushe. Nilipita 821 KJ Bulombora operation nguvu kazi 1983 - 84. Mkuu wa kikosi Kikoti
 
Baada ya kuuona uzi huu, ghafla nimemkumbuka Yesu!

Sio Yesu wa Nazareth, hapana. Ni kijana mmoja tu wa kichaga aliefanya muujiza akazawadiwa hilo jina!

832 KJ Danger Coy, OP miaka 50 ya jkt.

Tuliharibu kazi tukaanza kupewa doso mpaka mida ya saa nane usiku.

Ndipo huyu mshkaji wetu wa kichaga akaamua kutoka nduki kuelekea kusikojulikana.

Makamanda walikuepo arround wakamuunganishia, na wakamkamata.

Kilichofuatia ni kwamba wengine wote tuliruhusiwa kwenda kulala, jamaa ndo akala kazi mpaka asubuhi. Ikabidi apewe jina la Yesu kwa kujitoa mhanga kuokoa kombania nzima!

Pale Muhuga mess, afande aliweka simu juu ya TV then akakaa kuangalia mpira mbele kabisa ya TV. Kuruti waliiba simu na hakumuona mwizi. Afande alibaki anacheka!

Nakumbuka tulivyokua tunatoroka saa kumi za usiku kuja dar, na kurudi kambini usiku muda wa kuhesabiwa tumetimia.

Yes, nakumbuka totoz za kiskazini zilivyokua za moto.

Namkumbuka msabato aliegoma kufanya kazi siku ya sabato. Adhabu zote zilifeli kwa huyu jamaa, hadi getini kofia nyekundu walimshindwa. Good thing ni kwamba siku nyingine alikua anapiga kazi kweli kweli, shambani anabeba ndoo mbili kwa mpigo.

Nakumbuka mshkaji wangu alivyoibiwa simu akiwa anaichaji na ameishikilia. Alisinzia, kushtuka akajikuta ameshikilia chaja pekee!

Naikumbuka route match kilomita 30 kuitafuta Bagamoyo, achilia mbali mbio za kilomita 16 kila siku kwenda shamba na kutafuta kuponi.

Namkumbuka mshkaji kibonge aliekuja na mwili kama wa Le mutuzi akarudi na mwili kama wa joti.

Na mkumbuka kamanda Bafeni, baba hansi na service man maneno!

Mwisho nakumbuka nilivyopiga kwata kikakamavu mbele ya mkuu wa majeshi wa kipindi hicho General Mwamunyange.

Jeshi ni noma wakuu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…