Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Mwenye full story ya kupotea kwa malela jmn kisa kitamu hichii

Story ya malela haina kisa kirefu.ni kwamba,

Alipotea akiwa na wenzake katika mchaka mchaka usiku miaka ya 80s,akatafutwa sana kama ujuavyo jeshi linavyosaka kilichopotea,lakini hola(hakupatikana),badala yake akawa anatokea kama mzimu katika kambi mbali mbali.

Ila hii ishu inasemekana iliwekwa ili kuwafanya kuruta wasipende kujitenga tenga,kwani kuna mzimu(malela),ulipotea katika mazingira ya kutatanisha,unachukua kuruta na kupotea nao.
 
Mwenye full story ya kupotea kwa malela jmn kisa kitamu hichii
Malela alikuwa ni dawiri aliomba kwenda kukojoa wakati wa mkesha,akaenda ila hakurudi akatafutwa kila mahali,mpaka serengeti, angani hakuonekana,wakapiga simu mpaka nyumbani kwao labda katoroka ili wajue lakini hakuwepo nyumbani kwao,wakafuatilia mpaka nyayo za miguu lakini ziliishia pale tu alipokwenda,hivyo ilikuwa ni kama vile alinyakuliwa ndio maana mpaka leo kambi zote tunaimba malela yukwapi tunamtafuta!
 
Malela alikuwa ni dawiri aliomba kwenda kukojoa wakati wa mkesha,akaenda ila hakurudi akatafutwa kila mahali,mpaka serengeti, angani hakuonekana,wakapiga simu mpaka nyumbani kwao labda katoroka ili wajue lakini hakuwepo nyumbani kwao,wakafuatilia mpaka nyayo za miguu lakini ziliishia pale tu alipokwenda,hivyo ilikuwa ni kama vile alinyakuliwa ndio maana mpaka leo kambi zote tunaimba malela yukwapi tunamtafuta!
Yep mkuu ilikuwa mwaka gani
 
Hapo nitapenda kuwakumbusha wale tuliokuwa wote pale Mafinga JKT Kombania F chini ya OC Rweikaza na yule afande invisible aliye julikana kwa jina la Master Follow-up. Tutamkumbuka afande kijana aliyeitwa Mwakyosi. Nakumbuka siku moja tuliamshwa saa kumi alfajiri kama ilivyokuwa kawaida kukata mifagio wakati tukielekea huko porini kukata mifagio kwa mchaka mchaka tuliambiwa twende tukiimba, nikaanzisha wimbo "...Siasa yetu hapana mbaya. Isipokuwa maafande ndiyo wabaya..." Jamaa kusikia mistari ile akaamuru wote kuchuchumaa chini na kuruka kichura chura.

Upande wa Afande Master Follow-up au Afande Mlimbila ambaye sasa ni marehemu, nakumbuka siku moja alimuuliza kuruta mmoja kwamba alipataje kovu lililo katika paja karibu na nyonga. Tamko lile lilizua kilio kwa binti yule na binti alikwenda moja kwa moja kwa CO T N Mlay kutoa taarifa kuhusu mauza uza aliyoyaona usiku ambapo alisema alikuwa akiota kuna mtu amevinjari naye usiku kucha na iweje afande atamke kuhusu kovu wakati ni kweli analo na alijuaje wakati hajawahi kuwa naye kwa makubaliano.

Kifo cha Master Follow-up: Siku hiyo kulikuwa na mkutano mkuu wa wakuu wa vikosi Ma-CO nchini wakati huo Mlimbila alipangiwa kulinda kituo kidogo cha JKT kilichoitwa Sao Hill ambako kulikuwa na mradi wa kuchoma mkaa. Jamaa akakaimu kazi hii kwa mtu mwingine yeye akabaki kikosini. Pale kikosini kulikuwa na afande mmoja Mngoni aliyekuwa na mkewe dogo dogo aliyeishi karibu kabisa na apartment au hanga la Mlimbila. Na afande huyu Mngoni alipangiwa kulinda geti dogo karibu kabisa na nyumbani kwake na inaelekea alishapata fununu za mtoto (Mkewe) kuvinjari na Mlimbila. Muda wa saa mbili usiku bwaloni kukiwa na dance la kumalizika kwa mkutano afande Mngoni akaaga kwenda nyumani kwake "kukagu". Inasemekana alifika akagonga mlangoni bila kufunguliwa, kisha akaenda kuchungulia dirishani na kumuona Mlimbila akiwa ameketi kitandani akiwa mtupu na mke wake afande Mngoni. Alilenga SMG kupitia upenyo wa dirisha na kumkuta Mlimbila katikati ya paji la uso kuona vile binti alikimblia sebuleni na kufungua mlango na kukimbia. Mngoni aliingia na kuuchakaza mwili kila sehemu kwa risasi. Alibakiwa na risasi kama tisa tu. Mwili wake ulipelekwa Mafinga Hospital kujazwa pamba ili angalau uso wake uweze kutambulika. Haya ndiyo nayakumbuka sana ninawakumbuka kuruta wenzangu akina Tarama Mamkwe, Ndubula Msaki, Rachel Mapande, na wengineo.
Bonge la story!
 
Maarifa,
Umenikumbusha mbali aisee. Nilikaa Mlandizi kama mwaka mmoja niki-pump maji kwenda Dar (Siku hizo NUWA). Nilipofika hapo siku moja boss wetu Mhandisi Kasiga, alikuja akatuambia tuvalie vizuri na twende kwenye sherehe ya WAFANYAKAZI wasomi kwenda kumuaga URIO. Basi sherehe ilifanyika Ruvu Secondary kwa mwalimu mkuu. Ndiyo siku nilikuja kumuona Urio. Jamaa likuwa charming wala huwezi amini kuwa ndiyo huyu mtu huwa nasikia kuwa mkorofi. Nasikia walikuwa hawapikiki na Makame. Wakati Makame anahamishiwa Mbeya na kumuacha Urio Ruvu, akasema mbele yake "... sintafuata chochote alichokuwa akifanya huyu Raia mla panya - Makonde...". Baada ya miaka kadhaa, Makame akaitwa Dar. Wakati akienda, akaamua kwenda Ruvu kuomba mayai. Urio kuona gari zuri akauliza nani huyo, wakamwambia Makame. Akaagiza MP waende wamtimue Raia aliyevamia Kambi ya Jeshi. Kumbe kufika Dar ndiyo anapewa cheo cha Mkuu wa JKT Tanzania. Nasikia cha kwanza kufanya ni kumpigia Urio simu kuwa "nakuhamishia hapa makao makuu..." Urio nasikia akacombine haraka sana na akarudi TPDF.
Unamkumbuka yule afande (Mtu wa Mbeya) aliyekuwa akishughulikia fedha pale Ruvu? Nasikia alikuwa akizika sana makuruta fedha. Watu wakizamia pale, anawapa form wajaze kuomba fedha za nauli. Mkikatwa bogi basi fedha anatia ndani. Ukimaliza JKT na kwenda kudai fedha, anakuitia MP wakutimue kwani wee ni raia. Huyu jamaa alikuwa TAJIRI baadaye na nasikia alikuja pata ajali na kufa kama sikosei Visiga? kama waenda Dar, akiwa ndani ya Pajero. Alikuwa akitamba kuwa kazika hadi fedha za marehemu waliokufa vitani Uganda, itakuwa nyie makuruta?
Ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga!
 
Huu uzi umekuja sasa hivi??? Bulombora mpo??? Operation Ujenzi, Combania C: Afande Makani Jamani hao watu!!! Yule Sargent aliyekuwa anabeba pistor nimemsahau jina aliua nyoka wakati serule wanaimba mimi nanga!!! Eee bwana we Majeshiiiii ilikuwa raha. Mnakutana kwenye Makuruma hall mnawasema ma Afande kwa CO, subiri mtoke mnaipata kuliko jana!!!! Makuruma ilijengwa kila intake ni makuti usifikiri ni jengo. Hata mahanga yalikuwa hayana madirisha tulikuwa tunaruka tu.
 
Jamaa mmoja alikuwa mwoga sana, anaogopa sana adhabu. Kama kawaida ya jeshi. ilikuwa ni lazima utandike kitanda vizuri kwa style ya jeshi, kila kitu, shuka, blanketi, kitanda mess tin, kwa dressing. Haya yote unatakiwa ufanye kabla hujapurukushwa kwa wito wa 'FOLEN'! Basi huyu jamaa alikuwa anatandika kitanda chake vizuri usiku tukitoka disco, halafu alikuwa analala chini! Tulikuwa tunamcheka sana, lakini baadae tukawa tunamuonea huruma.

Njemba moja alikuwa akizurura kutwa na sururu. Akiulizwa, askari unakwenda wapi, anasema ametumwa kazi na afande fulani. Tulikuwa tunamuonea huruma maana alikuwa anazurura kutwa na sururu baada ya kulala porini kama sie wengine wajongomeaji.

Tulijifunza kutomaliza kazi mapema, maana ukiripoti umemaliza kazi uliyopewa, unabambikiziwa nyingine. Tulikuwa na midomo yenye fridge, maana kama jamaa yako alikuwa zamu jikoni, akikuchotea nyama au wali kwenye mess tin, unatakiwa umeze haraka, hata kama ni vya moto kiasi gani. Ulitakiwa uwe mwizi sana, hasa wa kofia, maana kama umeibiwa kofia na hukuvaa, unapewa adhabu. Mimi nilizoea kuwaibia maafande kofia zao, maana ilikuwa ni rahisi kwao kupata nyingine.

Katika kombania yetu tulikuwa na wahindi wawili. Siku moja kwenye disco, baada ya wiki kadhaa za kukaa jeshini, mhindi mmoja akawa anatufundisha wimbo wa kihindi. Tulijifunza, lakini yule mwingine akawa anacheka sana,. Sisi tukadhani kuwa maneno ya wimbo ule yanachekesha. Kesho yake ilibainika kuwa yule Mhindi aliyetufundisha ule wimbo ametoroka. Yule mhindi aliyebaki akatuambia alikuwa anacheka sana maana maneno ya wimbo ni: Kwaherini, mimi kesho natoroka!

Siku moja kombania yetu ilikuwa zamu. Platoon yetu ikapelekwa kwa kuku. Kama kawaida, ukishafika huko unakazana kubugia kwa wingi mayai mabichi kiasi utakachoweza. Baada ya kumaliza kazi, tukachukua mengine, tukajaza kwenye mifuko ya combat. Rafiki yetu mmoja akachukua mengine akayaweka kwenye jungle hat yake, halafu akaivaa. Tukawa tunaondoka kutoka kwa kuku, tukiwa na dhamira ya kwenda kwenye jongomeo letu msituni. Mara tukakutana na ma MP. Kitu kilichotuponza siku hiyo ni kutokuvaa vizuri. Hatukufunga kamba boot, mashati hayakufungwa vifungo nk. MP mmoja akasema, 'Askari, simama. Mbona mmevaa kama askari wa kukodiwa?' Akamuita yule jamaa aliyevaa jungle hat yenye mayai. 'We, kuja hapa, mbona umening'iniza kofia? Njoo hapa nikuonyeshe namna ya kuvaa'!! Akashika kofia, akaishusha kwa nguvu ili aizingushe zungushe kwa nguvu kichwani. Lo, si mayai yakavunjika! Yakaanza kumwagika usoni mwa jamaa. Basi tukazingirwa tusikimbie. Tukasachiwa likapatikana karai zima la mayai. Tukapigishwa fang fang usawa wa Quarter Guard, tayari kwa kufungwa na kuwa court marshalled.

Muda huo ulikuwa mchana na chakula cha ma MP kilikuwa kimeletwa. Basi ma MPwote, isipokuwa mmoja, wakaenda kula. Ikatokea kuwa kitabu cha kuandikisha mahabusu kimejaa, MP akaenda kuchukua kingine. Wakati huo tupo kwenye baraza la Quarter Guard, bado hatujawekwa ndani. Kuona upenyo huo, tukaamua tutoroke. Mmoja wetu akakumbuka kuwa tumesahau karai letu la mayai, akalirudia, tukatokomea nalo msituni. Mchana ule tulikula vizuri sana mayai ya kuchemsha .

Wakati wa usiku kwenye disco, tukaona kundi la ma Mp linakuja usawa wa kombania. Tukajua, leeo tumepatikana. Wakaongea na kamanda wa kombania, halafu muda si mfupi wakaondoka. Baada ya wao kuondoka,kamanda akasoma majina yetu na kutuita tutoke mbele. Akautuuliza, nyie mlikuwa kwa kuku leo? Tukamuambia ndio. Akasema safi sana, nyie askari wazuri sana, mmekamatwa, lakini mkaweza kutoroka, pamoja na mayai yenu. Huo ndio uaskari. Hatukupewa adhabu, disco likaendelea!
Nilichojifunza ni kuwa jeshini hakuna utaratibu wa kuishi...na huo ndio utaratibu!
 
Hebrew,

ha! ha! ha! ulikuwa RUVU combania F, kombania ya Mahepe, kombania ya Wajanja!! basi F kulikuwa na OC Luteni Mwakatumbula, Sir Major Babwetega "Mwiba", Staff Surgent Kinyaruhama "Kibuyu", Surgent Salamba, Volunteer Koplo Mwamasangula "Kamanda Mizinga", Afande Monica. pia alikuwepo Surgent mmoja Mhaya nimemsahau jina. Surgent Mwambingu pia alikuwa anakuja kubangaiza. F COY ilikuwa na watukutu wote na wasichana wote wazuri. Maafande waliamua kukomoa makuruta wa F COY lakini badala yake makuruta wakawa wagumu. lilikuwa linapigwa kwata la mfano na kufa mtu. Maafande walikuwa wanatoka maofisini kuja kuangalia kwata. Baadaye F COY ilihamishiwa Mgulani kupiga gwaride la miaka 30 ya uhuru. Afande Kitomari RSM wa Mgulani alitukoma makuruta toka Ruvu kwasababu ya utoro.

CO alikuwa Luteni Kanali Kanaeli Urio, 2IC Major Chotta, CI Major Nakuchema, Adjutant Captain Balala, RSM Warrant Officer II Situke.

JESHI LILIKUWA NI KUPOTEZA MUDA TU. SIKUONA FAIDA YAKE.
Nimecheka sana!
 
Mi nilikuwa mafinga A coy 87/88 nakumbuka pamoja na mambo mengine kuna mwenzetu mmoja ali act uselule (ugonjwa) mpakabhadi sisi wenyewe tuliamini, akawa mlinzi wa kudumu wa hanger kipindi chote cha ukuruta. Baada ya kumaliza mafunzo tulishangaa ni mzima wa afya na hivi sasa ni mkuu wa wilaya moja kwenye serikali hii ya Magufuli[emoji3][emoji3]
 
Nakumbuka nilimpiga ST sababu alinambia nideki choo nikaona hizi dharau nilimtandika mpaka military police wakaja daah nilipewa kichapo alafu nikawekwa mahabusu wiki mbili sitasahau mateso yale
 
Kitu kikubwa nilichojifunza JKT ni "Endurance".Hii imenisadia sana kuwa na uvumilivu wa hali ya juu hasa katika kipindi hiki ambacho "hostility" imetamalaki nchi nzima.

Enzi hizo Oljoro JKT ilikuwa 16 KJ, CO akiwa Colonel Adamu Mwakanjuki. Alikuwa muungwana sana kuliko watani zangu wengi wa kinyakyusa ninaowafahamu. Inawazekana ni kwa kuwa alikuwa mnyakyusa wa Unguja. Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.
 
Vibwende+ babu kombania D . nikiwa nanakima rc mongela, DC Richard kasesela Na akina Lt Colnel kalambi, hao walikuwa mabingwa wa ubangaizaji Ruvu!!
 
Back
Top Bottom