Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Tupia tukumbukie enzi hizo compulsory tulivyokuwa tunagonga jembe,unaambaa na mraba takriban km 10.
 
ss wa mwaka jana maramba JKT mpo mujb wa sheria
 
Du kuchunga mbuzi bora kulima. Ni wasumbufu hakuna mfano.
 
Namtafuta afande wangu maìsha yangu yote nimekuwa mzee nimestàfu nina hakika kwa umri ule atakuwa amestaafu.
Alikuwa ni staff Sajenti by then 1986 Ruvu JKT aliokoa maìsha yangu malaria ilipanda kichwani akalazimisha gari main gate nipelekwe Tumbi Kibaha wakati huo kulikuwa na outbreak ya ķipindupindu na homa ya uti wa mgongo(meningitis ) kwa weledi wake akalazimisha gari itoke kama sìo leo ningekuwa RIP namtafuta huyu mutu alikuwa anaitwa staff Sgt Shelukindo
 
Ebhana!! Mkuu sahivi ruvu ikovizuri sana nami pia course yangu ya JKT nilipigia pale, chini ya kamanda niliyekua nikimkubali Sir Charles Mbuge: dah huy mister ni kati ya watu nnao wakubali saaana than normal katika jeshi la nchiyetu, huyu mkuu ni very systematic sana majuzi kapewa tengo kali sana na mkuu wa majeshi, dah hakika anastaili sana bna,

Brigedia charles mbuge always be strong, nakukubali sana mkuu.
 
[emoji24][emoji24][emoji24]pole sana mkuu, hakika kila binadam ni muhim hapa dunia, maafande wangu wa Roadgan, kuku coy, main get mamaangu mpendwa kamanda Mamuya mkuje huku, wananchi wazalendo tuko pamoja, I miss them very much..


Namiss sana hanching hanching position[emoji58][emoji58]
 
Maparachichi ya AA, mapapai ya AB, karanga za Mgombe hahahahaa miaka minne toka nitoke kule.
 
Naomba anayemjua huyu afande au yeye ani PM nakumbuka kuna Sgt Sahani,Mwambingu,Kidonge chekundu,Saidi au Yuda Iskariot,Mazani
 
Hahahahh mkuu umenikumbusha yale maeneo.....nimetoka kule 2014 ndy intake ya kwanza pale!!
 
838 KJ Maramba kuna Mkuu alikuwa anaitwa Mwakisyala ni hatari tupu,sikuwahi kumuona akikenua always he was serious!
 
Nakumba JKT RUVU operation vyama vongi 1993/93 alipotutembelea mkuu wa JKT na kushangaa tunakunywa chai na mikate yeye anakadai hajawai kusikia wala kuona askari wakiwa kambini wanakunywa chai.Nilikuwa Combania F vibwende ndiyo njia yangu ya kutoroka.Nyoka kibao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…