Kombania A kulikuwa na kiafande kinaitwa Mwashamba..ebwana hiki kijamaa noma kweli.
.Kwa Msange kombania B ilikua na maafande poa na tulikua tukishinda kila mashindano kuanzia kwata na shughuli nyingine nyingi namkumbuka Afande Sijali,Afande,Mrope,Swai.Pia namkumbuka Afande Wela wa kombania D huyu jamaa alikua katili wa kupindukia.Kwa upande wa wimbo naukumbuka wimbo huu oo msange...msange malaika....oo msange nitarudi
Duu, Mwashamba. Jasha kama unakumbuka, Msange pia alikuwepo Mwashamba Kombania A. Hawa ni mtu na ndugu yake. Mwashamba wa Msange alikuwa akipiga NYUMA GEUKA, anazunguka zaidi ya degree 180 halafu anarudi kwenye hiyo 180, na anapiga mguu. Huyu wa Msange alikuwa kaowa na hivyo hakuwa anajionyesha kupenda chini.
Msange nilikuwepo Operation ya Chama. Nilikuwepo Komb. A kwa Mohamed. Kama unakumbuka Makonde walikuwepo wawili, Mrope na Mohamed. Pia yule mchaga sijui Majani (walikuwa hawajaowa). Sisi tulikuwa 89/90. Tulifika CO akiwa Sanga na baadaye akahashimishwa na kuwa yule M-Mbulu nani sijui.
Afande wera, Muha yule lohhhh. Sisi tulipofika alikuwa kapoa sana. Nasikia alimfanyia unyama kijana fulani kumbe jamaa ni Medical Assistace, na jamaa akapangiwa kazi Kitete. Wera akaugua jino akaenda pale Kitete na kijana akamtoa jino zima akaacha bovu. Wera kichwa kikavimba na next day akarudi tena na jamaa ndiyo akatoa bovu. Ila mwaka wetu nakumbuka siku ya sherehe ya kutuaga walikosana na jamaa anayeitwa Shelukindo kwenye Disco.
Wera akachukua Ma-MP asubuhi na kwenda kumkamata. Basi ilianza urukushani na kwa sababu Shelukindo alikuwa kapanda, basi kazi ilikuwa ngumu. Shelukindo akiwa ndani la shati la kijana Mataka (Kijana wa Movie) alichaniwa lile shati, na Shelukindo alimchania Wera Suruali na tukagundua kuwa alikuwa ndani ya chupi VIP. Ila bahati haikuachia ipande kifuani.
Waikumbuka Mihogo ya pale Msange? Zile Zambarawe na Maembe ya pale? Kwa taarifa yako, unaweza kuiona Msange JKT ndani ya GOOGLE Earth. Na juzi nilicheka kusikia kuwa JOHN LEGGEND yule mwanamziki kutoka USA aliyekuwa Tanzania, kumbe alienda Mbola. Waikumbuka Mbola lakini??
Mrope nakumbuka alienda Dar, na kurudi akawa anasikiliza nyimbo za Reggae. Nikamuuliza hivi huyo ni Tosh? Akanijibu bila mkwara "Hapana, huyu ni Lucky Dube....."
Hivi ndivyo nilivyokuja msikia Lucky Dube. Niliporudi Dar, cha kwanza ni kwenda nunua Kaseti ya Lucky Dube. Mrope alikuwa hana shida na mtu. Mmakonde kapanda wala huwezi amini ni Makonde. Wamkumbuka Ngoma? Alimsotesha jamaa yangu mmoja aitwaye Sepetu hadi leo hii yule anasema akimuona atamdunda. Jamaa likuwa kaficha godoro msituni. Akirudi kikosini, Ngoma anampa Drill, jamaa akitoka hapo analala msituni wiki. Akirudi tena anapata Drill, na jamaa analala msituni wiki........ hadi akamaliza. Ehh, pia alikuwepo Afande Magwega. Siku za mwanzo unamuona usiku tu maana alikuwa anapenda sana kuimba. Magwega wa Chiguru...
Namkumbuka sana Kepteni Mrimba. Mkuu huyu wa Mafunzo ya kijeshi alikuwa very up-to-date. Mafunzo yake na lugha yake imefanya hadi leo hii nikumbuke alivyosema. Mkifika siku za mwanzo, Mpoleeee. Mkianza mafunzo ya kijeshi anakuwa Mbogo. Pana wakati ilikuwa tuende kuhudhuria mazoezi ya kijeshi ya DIvision ya Mirambo. Basi tukaanza tizi la kukimbia.
Tunakwenda hadi Miyemba na kurudi. Jamaa wakasema tuongeze Mbio ili tumkomoe. Basi yeye si kuwa alikuwa akikimbia kama sisi. Alikuwa akienda kama mwendo wa nyoka. Yaani akienda kichaka cha kulia, baadaye cha kushoto. MWisho wa safari akawa kakimbia zaidi kutuzidi sisi. Looo, kutoka hapo tukajua kweli Mzee hatumuwezi na cheo alikipata kwa haki.