Katika vitu Mungu amenibariki ni kutokuwa na wasiwasi ninapojua nipo katika jambo au kitu sahihi.
Story iko hivi.
Miaka ya zamani nipo zangu JKT ndio nimefika hata intro. Hatujapitia tunasubiri mkuu wa kikosi arudi kutoka Dar es Salaam sina hili wala lile nimetoka zangu canteen naenda kwa mwendo wa kuruti (kukimbia kwa ukakamavu) nimepiga zangu green vest na kikaptula changu chini nina converse kali za kijani mpauko sina habari.
Naona hali si ya kawaida njia ya kuelekea uwanjani(master parade ground) hakuna watu kabisa na ilikuwa ni njia rahisi ukipita hapo unaingia kombania.
Nikajusemea moyoni labda watu wameenda kwenye fatiki acha nikaze mwendo nirudi zangu kulinda Hanga (sijui nimepatia ili neno) ,
Njiani nakutana na msoja amenuna mbaya begani yuko na bibi na bwana nikajiongeza kuwa huyu atakuwa afisa mkubwa mathalani Meja nikapunguza mwendo bana mikono nikatoa salamu kwa mbwembwe zote “Jambo Afande “.
Chuma kikageuka macho makavu hakikutoa mlio hata kidogo nilipoona amegeuka na kurudisha shingo nikasema Aaah kashaipokea hiyo nikachanganya miguu kama hakijatokea kitu mbio zikaendelea kuelekea kombania.
Nafika tu Sir meja wa kombania ananiambia kuruti umepita wapi? Bila ajizi nikamwambia maeneo ya uwanjani jamaa akashtuka akaniambia haukumwona mkuu wa kikosi! Kaubaridi kidogo kalinipitia nikasema eeeh nilimwona ila sikuwa nimemfahamu.
Ebwana kumbe siku ile alikuwa na kibarua na Level 3 walitinyanga sijui madudu gani jamaa walikula kazi pale uwanjani mpaka kombat zikawa za brown kesho yake wakawa Mbogo aliyejeruhiwa walitupiga tifu zito sana kwenye intro kama sikufa pale maisha yangu ni marefu sana .
Wakati mwengine nitawaletea jinsi nilivyokimbia mkesha wa six weeks na kutokomea porini nisijue naenda wapi [emoji23] .
Kuna wakati pia niliongoza kundi la majanga wazee wa kazi za hovyo hovyo nililipamba mpaka watu wakawa wanakimbia parade ya mwisho kuja kujiunga maana lilikuwa na watoto wakali pamoja na vibe za kutosha.
Mwisho wa siku nilipewa zangu B nadhani zoezi la shabaha lilinibeba nilipiga zangu range vizuri kwa kufuata maelekezo ya kukata pumzi na composure nikaosha jina mbele ya vigogo wa kambi.
Sent from my iPhone using JamiiForums