Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Mkuu mafinga ni balaa nilikuwa b coy kuna afande anaitwa saa ya mkebe akiwa anataka muimbe mpaka sauti isikike kwa mtoto wake Tony alieko changarawe pia mkiwa fatiki ili upate tano lazima upige picha na ukimlipa pay unakula tano za nguvu, pia mkono wa chuma kabla hajaongea tayari kashakupiga kibao pia bila kupasahau shambani kwa mwamunyange full maziwa na mayai baada ya fatiki saa nne
Alikua anaitwa Solex huyu mwamba, mfupiii
 
Uzi huu wa zamani, lakini na mimi najikumbusha kidogo pale Makutupora
Waliniita Saadam siku zile ''operesheni miaka 30 ya uhuru wa Tanganyika''
Zabibu tulikula sana ,kisha tunapiga mswakikusafisha ulimi ,ili ukikaguliwe usionekane na rangi ya zabibu imebakia.

Wale maafande wa kombania B akina Mwashamba na Oc Mzee Ufinyu wali koma utundu wetu.
Tulkula sana Nyama za kuchoma na nyanya mbichi kwa Ugali uliokubuhu kwa ugumu.,Mambo yote hayo usiku.

siku moja kwenye mradi wa kufyatua matofali ya udongo alfajiri baada ya mchaka mchaka,kazi ya kuponda udongo kwa miguu imeaanza ,kila mtu matofali 200 kwa siku. shughuli ilikuwa pevu kwa sisi wazaliwa wa mijini hasa Dar.

lakini usipotimiza utapata kadebra ya push up kama 100 hivi au kichura chura kuzunguuka bweni.
ai see kazi kweli.

1463201226538.jpg
 
1991/92 kwa mujibu wa sheria
Basi Kule kwenye matofali kulikuwa bado kiza hivi. karibu yangu kulikuwa na kichuguu,ukikitazama kwa mbali utadhani binadamu.,basi Afande akaita, wee kuruta unafanya nini hapo! kimyaa , kurutaaaa,! kimyaaa,sisi tunacheka, afande kanyanyua tofali la udongo na kurembea kwenye kichuguu , Kimyaaa,sisi tuna pasua mbavu kwa kicheko.

Afande Munacheka nini ,mimi nita mpasua kichwa huyu kuruta ,kwani analeta ukaidi akavurumiza tofali jingine.

Kimyaaa
hatimae akaamua kukivamia kile kichuguu na tahamaki kumbe si mtu bali ni kichuguu,
Afande kaumbuka ,na makuruta kuzidi kupasuka kwa kicheko. Kwa kuwa ilikuwa bado kupambazuka ilimfanya aamini kuwe yule ni mtu na kumbe sivyo kabisaa. Ila sisi tulijuwa kuwa kile ni kichuguu
Mbavu zangu siku hiyo wacha bwana.

Ila kulikuwa na jama mmoja kutoka Mbeya nadhani aliitwa simfukwe, yeye ikifika saa 5 kamaliza matofali 200 anasepa. Huyu jamaa alikuwa mtu wa shokakweli kweli, Maanamimi sikuwahipo hata siku moja kutimiza matofali 200, sanasana nimejitahidi 70 shughuli ilikuwa si ya kitototo. hatimae nilikuwa fundi wa kujenga na kuezeka nyumba za jeshi.

Makutupora oyeeee
 
Hua natamani sana kulitumikia taifa langu, kwa namna yoyote ile.. ila sijawahi kufanikiwa.
Kwa nn camp za Kigoma zinaaminika kutoa vijana wa JKT wakakamavu kuliko kwingine?

Wale wa Bulombora mnakumbuka kwenda kucheza mpira Kaseke na roli halina taa?mkirudi jioni barabarani kwenye lile daraja bovu tunavuka kwa kuwasha njiti za kiberiti.

Nafurahi sana kulitumikia taifa hili. Jeshini raha jamani, yale mateso ndiyo mbegu ya ukakamavu wetu mtaani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waliopitia jkt 90/91 mnamkumbuka Alice Kambona alikuwa muda wote anatembea na tester fundi umeme?nilipokutana nae chuo kimoja cha medical,nilimkumbusha vipi wewe si ulikuwa fundi umeme jkt Ruvu akaanza kucheka tu.Maisha ya JKT raha sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JKT KANEMBWA,sintosahau shughuli ya kuandaa mashamba,
1.mnaingia kwenye chaka kubwa mnatengeneza fire break kwa fyekeo na jembe
2. mnawasha moto kwenye nyasi zilizo kauka na kuuzunguka usivuke fire break kwa ajili ya upepo
3.Mnadondosha miti yote kwa mashoka, mnachimba kuitafuta mizizi ya miti mnaikata mpaka miti idondoke.

Mwisho sitokuja kusahau somo la uchap, Moto unawashwa porini mnaamshwa saa nane usiku mnaenda kuuzima mpaka hasubuhi hamjamaliza.
Nyimbo za kupeana hamasa pia zilikua sehemu kubwa ya faraja wakati huo.
 
Bubu Msemaovyo,
Afande David Tibazuka tulikuwa tunamuita bigula wa combania c. Huyo master follow up sie tulikuwa tunamuita Kingo
 
Sanctus Mtsimbe,
Umenikumbusha mbali wewe kuruta wa 1985. Binafsi nilikuwa kuruta pale Makutupora mwaka 1972! Kuna mengi ya kukumbuka ikiwa ni pamoja na kuanzisha lile shamba la MIZABIBU pale JKT Makutupora. Alikuwapo AFANDE MUTU, waliopita JKT Makutupora wanamfahamu, yey alikuwa ana amsha makuruta usiku ukiwa mkubwa sana, kama saa nane au saa tisa na kuwahenyesha porini sana. Halafu katika operesheni hiyo - OPERSHENI TUMAINI,

intake yake ilikuwa ni ya Form Six wote isipokuwa kijana mmoja wa SEVEN, namkumbuka hadi jana lake, alikuwa anaitwa HAJI TENGENEZA! Intake hii ilikuwa na vituko sana hasa kwenye UMOJA NA USHIRIKIANO, ilikuwa zaidi. Ilifika wakati makuruta walikuwa wakijitayarisha kwa adhabu za aina zote

......iwe push ups au hata kwenda MAHABUSU. Kuruta walikuwa wanafanya PUSH UPS mapaka Maafande wanashanga, yote haya ni kwa ajili ya kuwa tayari in case unapewa hizo push ups kama adhabu. Makuruta walikuwa wanaomba hata kwenda MAHABUSU! Usishangae kwani JKT wenye priority ya kupata chakula kwanza ni wale walioko MAHABUSU, na JKT ukigoma kula ni kosa la kijeshi!

Hili jingine nisije nikalisahau kwani liliwashtua sana MAAFANDE wetu pale Makutupora. Unajua Dodoma ni kame na jua ni kali sana. Kuna siku moja afande mmoja akatoa adhabu ya "USAWA WA BOMBA", wakati huo badotuko kwenye Green Vest, siunajua zile wiki sita za kwanza!? Afande alidhani hiyo ni adhabu ya kuwakomoa kuruta na kuwachafua! Lo, aliposema ...

"kuanzia hapa hadi hapa USAWA WA BOMBA", alishangaa akaona karibu Kombania yote inaelekea USAWA WA BOMBA na kwenda kujigaragaza chini ya bomba la maji! Alishangaa hadi akatumia nguvu kuwatoa KURUTA USAWA WA BOMBA! Yako mengii, kwa leo nimalizie hapa.
 
Back
Top Bottom