Sanctus Mtsimbe,
Umenikumbusha mbali wewe kuruta wa 1985. Binafsi nilikuwa kuruta pale Makutupora mwaka 1972! Kuna mengi ya kukumbuka ikiwa ni pamoja na kuanzisha lile shamba la MIZABIBU pale JKT Makutupora. Alikuwapo AFANDE MUTU, waliopita JKT Makutupora wanamfahamu, yey alikuwa ana amsha makuruta usiku ukiwa mkubwa sana, kama saa nane au saa tisa na kuwahenyesha porini sana. Halafu katika operesheni hiyo - OPERSHENI TUMAINI,
intake yake ilikuwa ni ya Form Six wote isipokuwa kijana mmoja wa SEVEN, namkumbuka hadi jana lake, alikuwa anaitwa HAJI TENGENEZA! Intake hii ilikuwa na vituko sana hasa kwenye UMOJA NA USHIRIKIANO, ilikuwa zaidi. Ilifika wakati makuruta walikuwa wakijitayarisha kwa adhabu za aina zote
......iwe push ups au hata kwenda MAHABUSU. Kuruta walikuwa wanafanya PUSH UPS mapaka Maafande wanashanga, yote haya ni kwa ajili ya kuwa tayari in case unapewa hizo push ups kama adhabu. Makuruta walikuwa wanaomba hata kwenda MAHABUSU! Usishangae kwani JKT wenye priority ya kupata chakula kwanza ni wale walioko MAHABUSU, na JKT ukigoma kula ni kosa la kijeshi!
Hili jingine nisije nikalisahau kwani liliwashtua sana MAAFANDE wetu pale Makutupora. Unajua Dodoma ni kame na jua ni kali sana. Kuna siku moja afande mmoja akatoa adhabu ya "USAWA WA BOMBA", wakati huo badotuko kwenye Green Vest, siunajua zile wiki sita za kwanza!? Afande alidhani hiyo ni adhabu ya kuwakomoa kuruta na kuwachafua! Lo, aliposema ...
"kuanzia hapa hadi hapa USAWA WA BOMBA", alishangaa akaona karibu Kombania yote inaelekea USAWA WA BOMBA na kwenda kujigaragaza chini ya bomba la maji! Alishangaa hadi akatumia nguvu kuwatoa KURUTA USAWA WA BOMBA! Yako mengii, kwa leo nimalizie hapa.